mdau wa kimasai akipatiwa huduma ya kwanza na wenzie baada ya kupigwa dafulao na daladala kwenye barabara ya kilwa rodi jana. hadi globu ya jamii inaondoka sehemu za tukio wanausalama walikuwa hawajafika na majeruhi alikuwa bado ana fahamu zake. sema hao jamaa zake walikataa kumsogeza ama kumkimbiza hospitali hadi trafiki waje wapime
mdau wa kimasai akipatiwa huduma ya kwanza na wenzie baada ya kupigwa dafulao na daladala kwenye barabara ya kilwa rodi jana. hadi globu ya jamii inaondoka sehemu za tukio wanausalama walikuwa hawajafika na majeruhi alikuwa bado ana fahamu zake. sema hao jamaa zake walikataa kumsogeza ama kumkimbiza hospitali hadi trafiki waje wapime

Uhai wa jamaa ndio muhimu kwanza kabla yakusubiri trafiki kupima.
ReplyDeleteHata hivyo ndio hali ya ufukara wa huduma zetu TZ. unapata ajali hakuna huduma ya haraka. polisi utasubiri masaa, ambulance nayo hivyo hivyo.
hata kama ulikua na majeraha ambayo yanaweza kupona lakini unakufa kwa kusubiri. watu wengi wanakufa kwa kupoteza damu nyingi.
Hivi TZ tuna huduma ya helikopta kuwawahisha mahututi hospitalini?
Rafiki yangu mmoja alikuwa akisema sote tuna ubaguzi ndani yetu. Tunawabagua wazungu, nao wanatubagua. Wanyamwezi wanaweza kuwabagua Waha nao Waha wakawabagua Wanyamwezi. Mara nyingi tunakuwa hatuuhisi ubaguzi huu hususan pale unapotokea miongoni mwetu (yaani "sisi" vyovyote utavyoichukulia). Miongoni mwa maneno yanayojitokeza bayana kwenye picha hii ni neno "Mmasai". Nafikiri Mmasai au Mnyawezi si muhimu sana kwenye maelezo ya tukio na picha hii. Fikiria kagongwa Mnyakusa karibu na Eiffel Tower na ikaandikwa kuwa ...mwafrika akiwa kagongwa... naamini mimi binafsi ningeona ajabu. Ingalitosha hapa kusema "mtu", "mwenda kwa miguu", au "mwananchi" vyote havina ladha ya ubaguzi...
ReplyDeleteyaani wewe nlikuona unazungumza mambo ya maana lakini tena naona wewe ni limbukeni kweli tena nafikiri upo nje ya nchi haujarudi nyumbani kwa miaka mingi,sasa kama unasubiri huduma kwa masaa hiyo helikopta itatoka wapi?hizo barabara zenyewe unazijua fatilia habari za nyumbani ni nyumbani tu usijisahau sana na box kisa likikuangukia helikopta itakuchukua kukupeleka hospitali unanikela kweli weee mwana
ReplyDeleteMichuzi rekebisha usemi sio ajali barabara ya kilwa rodi badala yake ungesema ajali barabara ya kilwa au ajali kilwa rodi
ReplyDeleteanon wa 2 we mmasai tu ndio maana..wanakuwa distinguished because they are different culturally,u can tell a masai anywhere but can you tell a nyakyusa or chagga person!?i dont think so..dont attack michuzi for no reason.
ReplyDeletehao wanaosubiria trafiki ambao wapo vijiweni wanakunywa kahawa,mpaka mtu wawatu atapoteza fahamu na maisha in general..kha!
hivi AAR haina helikoptas?
ReplyDeleteJamaa kanifurahisha sana anapofikiria ingefaa tuwe na helikopta kuwapeleka majruhi hospitali, good thinking for following an accident there is what is called the golden hour during which your chance of survival
ReplyDeleteis high if you get professional help, lakini si lazima upelekwe hospitali kwa msaada wa kwanza. Hapo Dar ingekuwa bora sana kama pangekuwa na Paramedics na pikipiki
Mjomba helikopta ya Yorkshire air ambulance (UK) baada ya kununuliwa na malipo ya marubani etc yahitaji £7200 kila siku
Hawa jamaa nao tatizo huwa hawali wakashiba. pia unakuta kutwa wapo barabarani vingunguti mpaka mwenge kwa miguu. usikute daladala lilimpitia karibu yake tu na ule upepo ukamzoa hatimaye chali. Masai vipi kutembea napo mnaendeleza mila...!! achane ubahili pandeni daladala.
ReplyDeleteAibu tupu Tanzania!
ReplyDeletemalisa
sasa we malisa,aibu tupu ya nini!?we mjinga nini..ajali zinatokea hadi marekani..aibu gani sasa?
ReplyDeleteAnon wa july 3 saa 9:38. Helikopta bongo ni muhimu. Pesa si tatzo bongo... Ikiwa serikali ina uwezo wa kulipa pesa nyingi za Richmond kila siku kwa huduma isiyotolewa, inashindwaje kulipa vijisenti hivyo £7200 kwa ajili ya maisha ya wananci wake?
ReplyDelete