WADAU WAPENDWA,
NINA FURAHA KUWATAARIFU KWAMBA BAADA YA MASAA TAKRIBAN 48 YA KWIKWI AMBAPO GLOBU YETU YA JAMII ILIPATWA NA KWIKWI KWA MATATIZO YA KIUFUNDI YA HOST WETU BLOGGER, HATIMAYE KWIKWI HIYO IMEMALIZIKA NA SASA LIBENEKE KAMA KAWA.
NAWASHUKURU WADAU WOTE KWA UVUMILIVU MKUBWA MLIOUONESHA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU, NA AHSANTE ZIWAENDEE WANAKIJIJI WENZANGU AMBAO WALIKUWA NASI KWA HALI NA MALI KUTUJULISHA NINI KINAENDELEA. KUWATAJA MMOJA MMOJA ITAKUWA KAZI NGUMU KWANI NI WOTE WALIKUWA SAMBAMBA NASI KATIKA HILI.
HIVYO NAWASIHI WANAKIJIJI WOTE MPOKEE MKONO WANGU HUU WA SHUKRANI, SINA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUWAOMBEA KWA MOLA AWAZIDISHIE MOYO HUO NA IMANI NA KUWAPA FANAKA KATIKA KILA MKIFANYACHO. AHSANTENI SANA.
TATIZO: ILIKUWA KWAMBA BAADA YA KUAMUA KUIFANYA GLOBU HII YA JAMII KUWA TOVUTI KAMILI NA KUANZA NA ANWANI MPYA YA www.michuzi-blog.com ILIBIDI KUBADILI PIA NAMNA YA KUENDELEZA LIBENEKE KWA NJIA IJULIKANAYO KAMA FTP PUBLISHING. SASA HOST WETU AILIKUMBWA NA MATATIZO YA KIUFUNDI NA KUSHINDWA KUUNGANISHA KILA POST KATIKA GLOBU HII.
HIVI SASA TATIZO LIMEPATIWA UFUMBUZI NA SASA LIBENEKE NI KAMA KAWA. ILE ANUANI YA michuziblog.blogspot.com ITASITISHWA NA KURUDISHWA STOO KAMA SPEA ENDAPO KUTATOKEA TENA MATATIZO KAMA HAYA. ILA KWA SASA ITASITISHWA NA TUTAENDELEA NA HII YA www.michuzi-blog.com
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2008

    Wanamaombi kutinga bungeni wiki ijayo

    2008-07-13 22:26:42
    Na Simon Mhina


    Kamati ya Umoja wa Makanisa ya Kikristo nchini, imemuandikia barua Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, ikimuomba awaruhusu waende Dodoma kulizunguka Bunge kwa ajili ya maombi na kusisitiza kwamba hawaamini taarifa iliyotolewa na Polisi kwamba unga uliopatikana ndani ya jengo hilo haukuwa na uchawi.

    Kadhalika, Kamati hiyo imewashauri mawaziri na wabunge wenye hirizi kuzisalimisha kwao kabla ya kuanza maombi kwani wanaweza kuumbuka.

    Pia Kamati hiyo imesema hatua ya Naibu Spika kufunga mjadala kuhusu `unga wa uchawi` haiwakatishi tamaa kufanya maombi hayo.

    Kamati hiyo imesema taarifa ya polisi imewachanganya na sio sahihi kwa sababu dola haiamini mambo ya uchawi.

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamti hiyo, Askofu Isack Kalenge alisema uchunguzi huo wa Polisi, Mkemia Mkuu, Bunge na Usalama wa Taifa ni batili kwa kuwa vyombo hivyo ambavyo viko chini ya serikali, havina uwezo wa kutambua uchawi.

    Askofu Kalenge, ambaye ni kiongozi wa Kanisa la Pentekoste International, alisema wanaamini kuwa bado uchawi upo bungeni na wabunge wengi wanateswa na nguvu hizo za giza.

    ``Uchawi ni jambo la kiroho, haliwezi kupimwa kwa kamera wala uchunguzi wa Mkemia Mkuu, tunaamini tatizo la uchawi bungeni halijapatiwa ufumbuzi, tunakwenda Dodoma kulimaliza tatizo hilo ili lisitokee tena,``alisema.

    Akizungumza katika mkutano huo, Mchungaji Wilbert Ngowi alisema kamati hiyo haiwezi kufumbia macho taarifa hizo, kwa vile zimeliaibisha Taifa.

    ``Umefika wakati sasa kanisa liseme yale ambayo lilikuwa linayafumbia macho na lifanye mambo ambayo yalikuwa hayafanyiki, japokuwa hatua hii inaweza kutafsiriwa kwamba tunachanganya dini na siasa, lakini si vibaya.

    Kuanzia sasa tumeamua kuchanganya dini na siasa kwa sababu maandiko matakatifu yanasema kufanya hivyo sio dhambi,``alisema.

    Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mchungaji Christopher Mtikila alisema iwapo watapata ushirikiano wa Spika wataenda bungeni wiki ijayo.

    Akifafanua, kiongozi huyo alisema wamemuomba Spika awape kibali cha kuingia bungeni kuwaombea wabunge na `kuharibu` nguvu za giza zilizojaa humo.

    Mchungaji Mtikila alisema kabla hawajatia mguu Dodoma, wanawataka Wabunge, mawaziri na yoyote ambaye anatembea na hirizi aisalimishe kabla hawajaanza maombi.

    ``Ni matarajio ya Kamati kwamba wabunge wazalendo, hususan wale ambao hawatembei na hirizi vibindoni, watafurahia kazi hii njema ya watumishi wa Mungu yenye lengo la kuwaponya,``alisema.

    Kiongozi huyo alisema iwapo watakataliwa kufanya mambo hayo, watalizunguka jengo la Bunge hilo na kurusha `makombora ya sala` na kuahidi kwamba hakuna mwanga wala hirizi itakayosalimika.

    Aliahidi kuwa wabunge na mawaziri, ambao ni wapenda uchawi, wataumbuka vibaya kutokana na sala hizo.

    Alisema tayari waumini mbalimbali wameshaanza kufunga kwa ajili ya kujiandaa na sala hiyo.

    Alisema hawatarajii upinzani kutoka kwa Bw. Sitta kwa sababu hivi karibuni Spika huyo alinukuliwa akiwataka viongozi wa dini, kuliombea Bunge kutokana na kuwa katika wakati mgumu.

    ``Sisi tumeamua kwenda kuliombea Bunge kama alivyosema, ila sisi tutaenda na mamlaka makubwa, ambayo yatasambaratisha kila roho chafu.

    Sisi wenye macho ya kiroho tumejua kwamba pale ndani pametundikwa kila aina ya uchawi, lakini hakuna hata mmoja ambao utasalimika,``alisema.

    Akizungumza na Nipashe jana, Spika wa Bunge, Bw. Samweli Sitta, alisema bado hajapokea barua hiyo.

    Hata hivyo, Spika alikataa kuzungumza iwapo atawaruhusu kutekeleza azama yao hiyo mara atakapopata barua yao.

    ``Hilo unalouliza ni jambo jipya, lakini siwezi kulisemea kwa vile sijapata barua yenyewe. Ni vema ukaandika zaidi maoni ya hiyo kamati,`` alisema.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2008

    Michuzi kuwa care siku nyingine ukitubemenda tena tunaandamana

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2008

    Nilikumisi.....!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...