
Ndugu yangu Michuzi,
mie ni mdau mkubwa wa website hii yetu ya jamii na ninaithamini sana kwa jinsi inavyotuhabarisha na kutuelimisha kwa haraka.
Naomba chondechonde unisaidie kuiweka website ya shule yetu mpya na changa hapa Tanga mjini inayoitwa Toledo, lakini inayofanya jitihada kubwa za kuitumia teknolojia katika kuhabarisha na kuelimisha jamii, na kuifanya shule kuwa jirani sana na wazazi na jamii kwa ujumla.
Website inaitwa
Mwalimu Mkuu
Samwel Ndauka
Mwalimu Ndauka!
Asante sana kwa ujumbe mwanana na hongera kwa hatua hii ambayo ni mfano wa kuigwa.
Nikijaaliwa kutembelea Tanga nitafanya juu chini nije kuwatembelea na kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya kisasa ya kupasha habari.
Natumai wengine wataiga mfano huu ili kufanya maisha yawe rahisi kama ilivyo azma ya teknolijia hii adhimu.
Pamoja na kutoa changamoto kwa wengine katika taasisi mbalimbali kuiga mfano wa Toledo, nakaribisha wadau kama Mwalimu Ndauka kutangaza tovuti zao katika globu hii ya jamii bila malipo yoyote.
-Michuzi


Hooongereni sana...Huu ni mfano wa kuigwa na shule zote. I hope mtaweza kuwafundisha hata hao wanafunzi kuwa webmaster ilikupunguza gharama za kuajiri one. Manake nimeona website nyingine zinazoanzishwa za shule huwa hawaupdate wala kuchange kitu chochote toka ikishafunguliwa ndio basi tena
ReplyDelete