Mkuu Michuzi,
Asalamu Aleikum
Bwana apewe sifa
Shalom
E bwana mie ni mdau mkubwa wa blogu hii ya jamii ambayo kwa kweli mfanowe haina, kwani pamoja na habari za motomoto na mapicha toka kile pembe ya dunia, pia kuna mada za kichokozi mno ambazo kwa kweli ni burudani na pia mafunzo tosha kwa wengi wetu.
Naomba nami unipe nafasi nipate kupata maoni ya wadau wako watukufu kuhusiana na hili swala nyeti mno la kutahiri.
Kama mjuavyo, wataalamu wanashauri wanaume kutahiri ili kujikinga na gonjwa hatari la ukimwi. Hivyo hivyo wataalamu hao wanakemea mila ya wanawake kutahiriwa ambayo wanaharakati huiita kukeketwa, wakitaja pamoja na mambo mengine, hatari ya hilo gonjwa.
Sasa basi, katika jamii yetu ya Kitanzania (sijui kwingineko mambo yakoje) kuna makabila ambapo kinamama wanaona mtu ambaye hajatahiriwa ndiye supa.
Naomba maoni wadau, na wewe mithupu usiibanie hii maana ni somo la kawaida kabisa katika jamii. si unakumbuka mambo ya baioloji shule?
Mdau Nyangwe


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...