mojawapo ya mabanda yaliyo kwenye maonesho ya sabasaba mwaka huu ni hili la mamlaka ya masoko ya mitaji (kwa kidhungu capital markets and securities authority) ambalo linasimamiwa na wadau hao pichani.kifupi, madhumuni makubwa ya masoko ya mitaji ni kusaidia ukusanyaji wa mitaji kutoka kwa umma wa wawekezaji na pia kuwawuzesha uahamishaji wa rasilimali kutoka kwa wenye mitaji kwenda kwa wenye kuhitaji mitaji hiyo kupitia soko la mitaji.
najua kwa wadau wengi hii ni kama lugha ya kichina ama kimongolia, lakini ukitembelea banda hilo utapashwa na kupashika nini faida za masoko ya mitaji ambayo ipo muda wote ila sema wadau wengi hawajaistukia.


dnamuona selenga kaduma na charles shirima,hongereni vijana kwa kuendeleza libeneke bongo land
ReplyDeleteShirima Charles bado mweupeeeee
ReplyDeleteLol! mlivyopania snap! mnajichekesha wenyewe kama mgeni alieishiwa mboga! enhe na mtueleze mambo ya NMB yameshafikia wapi..maana fedha hipo tatizo pa ku invest!
ReplyDeleteselenga umetoka kama kada wa chama, ila shirima kwa kweli yaani hapo na jinsi ulivyochomolea hiyo T-shirt umemuaribia sana mwana diplomasia wetu. eeeh!
mdau wa Doha
Chale ulitesa sana wakati ule ukiwa Arusha naona sasa umri unaelekea kukua,Vipi Maza ???
ReplyDeleteCAPITAL MARKET hamna warembo kila siku nyie tu ndio mnaonekana kwenye banda.....inachoshaaaa
ReplyDeleteJamani charles shirima, nanihii ndio ameingia mtini jumla? pole maana naona hata pete umevua. ndio maisha lakini.
ReplyDeleteNyie watu kama hamna mazuri ya kuandika kuhusu mtu,Msiandike.Usipende kumfanyia mtu kitu ambacho utamumiza roho.Hongera makaka wa capital Markets.
ReplyDeleteLini Soko La Hisa Tanzania mtaanza kusikika na kuonekana kila siku baada ya Taarifa za Habari za Televisheni mbalimbali nchini?Nani mwenye wajibu wa kupeleka habari zenu katika Masoko ya Hisa ya Kimataifa au katika Vyombo vya Habari vya Kimataifa kama vile CNN,BBC WORLD,SKY NEWS,RT,SIBC,na nyinginezo? Kwa wenzetu habari za kila siku za mwenendo wa soko la hisa ni muhimu sana kwa wawekezaji na kwa wafanyabiashara mbalimbali!Hapa kwetu ikoje?Au sisi watanzania tuna mfumo wetu peke yetu wa kuendesha uchumi? Hivi sasa Nchi wakilishi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki katika kupima mwenendo na mwelekeo wa uchumi katika kanda hii ni nchi za Kenya,Uganda na Mauritius!Vipi Tanzania mmelala wapi?Kampuni nyingi Tanzania zinaendeshwa kifamilia na kiswahili mno kiasi ambacho nyingi hazina sifa za kuingia katika siko la hisa.Lakini hebu tuanze na hizo chache basi.Biashara ya Hisa hapa nchini bado imedorora sana zaidi kutokana na uelewa mdogo sana kwa watanzania kuhusu biashara hiyo.Ili biashara ya hisa ifanikiwe lazima Riba za Mabenki hapa nchini zifanyiwe marekebisho makubwa sana!Vinginevyo hata baada ya miaka HAMSINI toka sasa,hali itabakia kuwa hivi hivi.Na wasomi katika Fani hiyo tunao kibao?
ReplyDelete