Baada ya matokeo ya jana pale Neshno, katika kindumbwendumbwe cha Kagame Cup, ya Simba kuilaza Vitalo kwa bao 1-o na Tusker ya watani wetu wa jadi kuhitimu kuingia robo fainali kwa karamu ya magoli 5-0 dhidi ya Benadir ya Somalia, msimamo wa michuano ya robo fainali ya Kombe la Kagame umetawaliwa na Jumuiya ya ist Afrika Mashariki kama uonavyo hapo juu.
globu hii ya jamii inamsaka katibu mkuu wa jumuya hiyo balozi juma mwapachu atie baraka zake kwa kunena japo kiduchu ya jinsi anavyoona vijana wake wanavyoliendeleza libeneke la kabumbu katika anga hizi...

ukipiga chabo kwenye hilo jedwali utakuta Neshno patakuwa padogo kesho Jumanne!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...