Mabingwa wa mchezo wa pool nchini Shoko Pool ya Kinondoni wakiwa na kombe lao na mfano wa hundi ya mkwanja walioshinda ambapo walijinyakulia kitita cha Sh.2.5m wikiendi iliyopita katika fainali zilozfanyika ukumbi wa diamond jubilee hall.
Washindi wa pili katika mashindano hayo ni Afrikan ya Mbeya ambao wamepata Sh. 1,750,000 washindi wa tatu ni Twiga ya Ilala ambao wamejizolea kitita cha Sh. 1,250,000 mshindi wa nne ni Royal ya Mwanza ambao wamepata Sh.1m.
Washindi wa tano hadi wa nane katika shindano hilo wamejinyakulia Sh. 500,000 kila mmoja wakati mshindi wa tisa na wa 10 wamepata shilingi 250,000 kila mmoja.
Mbali na zawadi hizo mshindi wa kwanza pia amejinyakulia kikombe na medali ya dhahabu huku mshindi wa pili akipata ngao na medali ya shaba.
Mashindano hayo yalianza mwezi mmoja uliopita na kufikia fainali zake Jumapili usiku kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee na yalishirikisha mikoa 10 ya Tanzania bara.
mashabiki wa shoko pool wakisherehekea ushindi wa timu yao
gemu la fainali katika ukumbi wa diamond jubilee hall
gemu likiendelea
WACHEZAJI 10 wameteuliwa kuunda kikosi cha timu ya taifa ya pool itakayoshiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa pool baadae mwezi ujao.

Kikosi hicho cha wachezaji 10 kimeteuliwa usiku wa kuamkia jana muda mfupi baada ya kutangazwa bingwa wa taifa wa mchezo wa pool katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia jana kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.

Shindano hilo ambalo lilishirikisha mabingwa wa mikoa mbali mbali ya Tanzania bara timu ya Shoko Pool Clab ya Kinondoni 1 iliibuka kidedea baada ya kuifunga Africana ya Mbeya mabao 4-2.

Akitangaza majina ya wachezaji watakaounda kikosi hicho Meneja wa bia ya Safari Fimbo Butallah ambaye ni wadhamini wakuu wa mashindano hayo aliwataja wachezaji hao kuwa ni Omary Obiara (Ilala), Rajabu Matumla (Kinondoni 2), Rahim Kajuna (Temeke), Ismail Jumanne (Kinondoni 2), na Francis Dogo, Iddy Abbas, na Omary Akida (Kinondoni 1), Mohamed Jumanne (Mwanza) na Colonel Jumanne kutoka Arusha.

Butallah alisema kikosi hicho kilitarajiwa kuingia kambini jana kwenye hoteli ya Manyara iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam kwa siku tatu na kesho Jumatano jopo la majaji litakaa na kuteuwa wachezaji watano watakaoshiriki mashindano ya Pool nchini ya dunia nchini Uswisi mapema mwezi Agosti




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...