Michuzi na wadau wa blog hii ya jamii,
Naomba kuwachokoza hawa ndugu zangu wachagga kutoka mkoani Kilimanjaro.Mada hii inawahusu watokao maeneo ya Rombo, Marangu, Kilema, Kirua, Old Moshi, Uru, Kibosho, Lyamungo, Masama, Machame, na Sanya Juu.
Kuna majumba makubwa na mazuri mno yamejengwa katika maeneo hayo, lakini wenye kumiliki hayo ma-Villa wako Dar, Arusha, Mwanza, Ulaya, Marekani, na kwingineko duniani.
Majumba haya hutumika tuu wakati wa krismasi au wakati wa misiba. Sana sana, mende na mijusi ndo 'wapangaji' pekee kwenye hayo majumba ya kifahari uchagani.
Je wadau, hawa wachagga waendelee kujenga majumba zaidi au vizazi vya sasa viachane na fikra hizi za majumba yasiyotumika vijijini?
Nawasalisha.
MDAU WA ARUSHA (Mzaliwa wa mkoa mmoja wa kusini)
Brother Misupu,
ReplyDeleteNapenda nimshukuru “mdau wa Arusha” kwa mtazamo wake dhidi ya wachagga…kwa bahati mbaya sana yeye anatoka “south” mwa TZ. Ila I think the point is kabila la wachagga was found under capitalism kind of system meaning uchumi wa wachagga uko based on a free market, open competition, profit motive and private ownership …kwa mantiki hiyo wachagga ni watafutaji sana na wako makini sana kwenye kutumia pesa zao (“to some point”).
Katika nchi za wenzetu zilizoendelea (capitalist countries) utakuta kuna kitu kinachoitwa “vacation home(s)” Baadhi ya watu wanamiliki hizi nyumba au wana-rent wakati wakitaka kwenda vacation.
Sasa kwa sababu wachagga niwatafutaji sana – they can afford kujenga/own a “vacation home” na kwa sababu wako makini sana kwenye ku-spend pesa yao – hawaoni sababu ya kwenda milimani na kukaa kwenye guest houses/motels etc.
Wachagga, correct me if I’m wrong.
Mdau toka Machame.
Si wachagga tu mdau...tembelea na Bukoba uhayani utabaki kinywa wazi kwa utakayoyaona...mahekalu kibao migombani lkn wenyewe wapo either mikoani au hata nje ya nchi.!!!!
ReplyDeleteNasikitika sana na fikra zako ambazo kwa kweli hazieleweki. Wewe mtu nyumba ni yangu! pesa ni zangu! inakuuma nini?
ReplyDeleteSijawahi kusikia Mchaga fisadi! mmejaribu kutoa mada kama "hakuna kabila wachaga" na bado mnaendelea kuchokonoa wachaga! hamuoni kuwa huo ni wivu??? kama umetoka huko masasi wee bwana kaa kimya tu..
WACHAGA OYEE!
malisa wa URU
sijui hasa inakuhusu nini kama umeombwa mchango wa kununua cement sawa unaweza kuja na hii hoja! otherwise utuache tulivyo hili ni suala la uwezo tu kaka! hujui kuwa wachagga ndio majews wa bongo? at some point lazima urudi home, sasa vipi kama home hakufanani na unapoishi kwa sasa?
ReplyDeleteKwanza nikupe pole kwa fikra potofu ulizonazo, kuna mheshimiwa amechangia hapo kiuchumi, napenda pia kumuunga mkono. Wewe unafikiri kama watu wangekua wanatoka mwakao waenda mijini jenga huko na kusahau walikotoka maendelea ya huko yangepatikana kivipi? Nataka nikupe mfano mdogo sana, kama serikali ina mpango wa kupitisha umeme ktk kijiji fulani na ktk kijiji hicho hakuna hata nyumba inayostahili kupata umeme maana ni nyumba za makuti, je waona umuhimu wa kupeleka huo umeme? Kumbuka maendeleo ya mtu huletwa na mtu mwenyewe, so toka kwenye fikra potofu, wachagga walijenga mahekalu , wanajenga na wataenda kujenga and that is one thing are proud about. They are proud because they know they have a resting place, where they go and get kitu roho inapenda during holidays.....
ReplyDeleteWachagga Ju, Ju, Juuu Zaidi!
Pascs - Kibosho
huyo wa kwanza hapo ndio katoa point ya maaana huyo anayejiita kuwa na mdau wa marangu. hata mimi ni mchaga ninayo vacation house moshi kama nyumba sio ngumu kujenga kule kwako kwanini usijenge.
ReplyDeletekwanza nyumba ni asset unajua?
tena asset kubwa tu
rekebisha mawazo uliyetuma hii
Mila na destruri za wachagga ndio sababu kubwa inayo wafanya wajenge kwao. Maendeleo kwa wachagga ni lazima uwe na nyumba. kijijini au mjini. Mimi ni msukuma nimeowa mchagga. Funzo la kwanza nililo pata kutoka kwa shemeji zangu, ni kujenga nyumba. Walitaka dada yao awa na kwake. I did it relactactly. Matokeo yake, hivi sasa nina fanya biashara ya kununua na kuuza nyumba. It works. Hakuna kitu kizuri kama kuwa na nyumbani. Nyumba yako mwenyewe. Mpaka leo na heshimu shemeji zangu.
ReplyDeletePamoja na kuwa nyumba hizo ni kama vocation home lakini nikwambie miji inapanuka sana. Huko unakokuita vijijini miaka inayokuja kutakua mjini tu...Angalia HIMO miaka 10 iliyopita na sasa hivi tofauti yake...kumebadilika sana...
ReplyDeleteJe ni wote wenye nyumba hizo hapo Himo wanaishi hapo...?? Wengi kwanza wanafaidiaka na nyumba zao kweli sasa hivi. Kuna wageni wengi wanarent sana hapo. Na hizo sehemu ulizozisema soon zitakua mijini na umuhimu wa kuwa na nyumba bora ndio utaufahamu..
Kila blog unayokwenda wachagga, wachagga mtatunyanyapaa mpka lini? Ila cha muhimu kabisa kumbukeni kwamba tunaendelea kudunda na kufanya mavitu yetu kwa nafasi!
ReplyDeleteKwani mlikua mnataka tujenge wapi??
Nkamangi.
tunaziita holiday home. huwa tunalala huko krismasi pekee yake. baada ya kuangaika mwaka mzima kwanini usiende holiday? nawakati sipo wanlala walimu wa my local school siyo mende. ila niwatu wanatafuta ajira uchagani.to make iteresting mwalimu mmoja ni mtu wa sumbawanga. maendeleo hayaji kwa mawazo kama hayo ya mchangiaji hapo juu
ReplyDeleteEvans,
ReplyDeleteNyumba inakuwa ASSET kama inazalisha pesa, lakini kama nyumba ipo tu inahifadhi mende na panya na badala yake inakula pesa ili kui-mantain basi hiyo ni LIABILITY si ASSET!
nOF KOZI NINA KIBARUA KUWAAMBIA KWAMBA ZAMA ZA MAWE NA MATOFALI ZILIPITA ZAMANI SANA. SASA HIVI UWE LAP TOP AU KOMPYUTA YEYOTE. LAP TOP IWE WORKING TOOL YAANI KIFAA CHA KAZI NA SIO PRIDING TOOL YAANI KIFAA CHA KUJISIFIA TUU KWAMBA UNACHO. the same as i phone au blackberry
ReplyDeleteNyumba nyingi zinakuwa ni faida kwa familia nzima inluding extended. Pia ni nzuri sana kwa ajili ya retirements kwani ukisha-hit miaka kama ya sabini maisha ya mjini inaweza kuwa kero kwako na nursing home TZ unaelewa hakuna hivyo. Na pia kama hutaki kuzikwa kwenye makaburi ya kinodnSo ukiwa mgombani maziwa, mayai, matunda , mchicha kila kitu kinakuwa ni karibu. Mijini siku hizi hakukaliki hivyo na uzee. Dar mbu wana uma sana ambapo "mndeni" kwenye kingo za kilimanjaro matatizo kama hayo hakuna. Ardhi ni rutuba you can imagine. Mito inachuruzika kutoka mlimani. Na watu wa huko nina experience zaidi na Rombo Mkuu ni watu poa sana. Ukikutana na mtu barabarani ni lazima umsalimie. Sinda ngoto mbe! kama ni mwanume au shamesha mani! kama ni mwanamama. Pia sehemu kama hiyo ndiyo inakuwa sehemu ya kuzikiwa badala ya kutegemea makaburi ya kinondoni.
ReplyDeleteby half mchaga
Wadau,
ReplyDeleteMimi sio Mchaga lakini nawaunga mkono ndugu zangu wa Kiboroloni na Kishumundu kwa jitihada zao. Kwa kujenga majumba kwao wanainua uchumi huko kwao maana hizo nyumba zinajengwa na mafundi wanaopatikana huko huko kwao. Sidhani kama hizo nyumba zinakuwa makazi ya mende, lazima kuna japo mtu anazilinda. Kwa hiyo nyumba hizi zinasaidia kupunguza makali ya tatizo la makazi nchini.
Mdau aliyeuliza swali hili anatatanisha. Kwa nini anahoji kwa nini watu wanajiletea maendeleo? Au ndio yaleyale tunataka misaada tuuuu?
Hongereni Wachaga. Hata sasa hivi napiga hesabu nipate Manka nikae naye atanihamasisha kimaendeleo zaidi.
Michuzi post zakizushi uwe unazitia kapuni...haya mambo ya makabila yameanza lini??? mara hakuna kabila wachaga, mara sijui wachaga mafisadi mara wanajenga mahekaru hayakaliwi....Michuzi kuanzia leo nakuomba uachane na post kama hizi...hazijengi wala kuchangamsha...njoo unguja uone mahekalu na wenyewe wapo, uk, us, muscat, dubai na kurudi huku kwa leisure labda kila baada ya 5/10yrs unless kuna msiba au dharura nyingine...ndugu zangu wanyamwezi ndo wamekalia haya majumba kama walinzi...umenisoma?? kwahiyo habari za wachaga ni ufinyu wa fikra na uvivu wa kufikiri ufanye nini ili utoke kama wao matokeo yake mnaanza majungu japo kunahistori za hawa jamaa kuwanyonya wenzao mfano mama mkapa kamjengesha ben majumba ya kifahari kwao wakati masasi choka mbaya, salma salimin alikusanya wachaga znz na mpaka kanisa katoliki znz parokia zote maaskofu na mapadre, masisy, makentista ni wakulekule, salama na wenzie wamemnyonya salimin baada ya mzee kuachia madaraka na kuchoka bi mkubwa kampa kibuti.....mwl nyerere angalia kondoo wako wanapoelekea sipo na Michuzi nataka ukemee tabia hii ya kuzungumzia makabila.
ReplyDeleteMdau Mareare...Mji Mkongwe
Kaka michuzi sasa naona watu wamekosa mada za kuleta hapa!! Nimweleze tu huyo ndugu yangu kuwa sisi wachaga hatuna ile kujionyesha kuwa mambo safi huku huna kitu, unakuta mtu mjini anavaa suti na tai na kuponda starehe wakati nyumbani kwao hata kibanda cha makuti hana!! kijana wa kichaga kipimo chake cha maendeleo ni 1)ana nyumba? 2)ana gari? bila kujali anafanya kazi gani na mengineo!!
ReplyDeleteatakayebisha abishe, wachaga tu juu!!!
Nkya A.town
Jamani tuacheni wachagga, we are the 'chosen tribe". Mbona nilienda machame nikakuta majumba kibaao na yote yanakaliwa na wenyewe. Kama hawaendi moshi daily, wanatoka arusha weekends. Ila wale wazee wa Machame wanaisha aisee vijana wacharuke sasa waendeleze waliyoanza wazee wao. Reginald Mengi tu ndo hajajenga kule, labda alipewa kiamba kidogo....
ReplyDeleteNafikiri unafahamu kabisa kuwa Senti ni maisha ya mtu hasa katika maisha ya sasa...Bila senti, huli, huvai, hutibiwi, hunywi..Hivyo hao wachaga wanapenda kwao ndio maana wakaimarisha kwao katika kujenga mji wao..lakini wanaenda katika biashara mikoa mingine kutokana na kufuata senti..Kama ujuavyo wachaga ni watafutaji hodari wa senti hivyo Mkoa wa Kilimanjaro sio mkoa wenye mzunguko mkubwa wa pesa ndio maana wanakuja Dar es Salaam au Mwanza ikiwa ni moja wapo ya mikoa yenye mizunguko mikubwa ya pesa kutokana na kuwa na Population kubwa ya muingiliano wa watu kutoka Nchi tofauti na mikoa tofauti...Kwa hakika Mkoa wa kilimanjaro maisha ni cheap kiasi chake ila ni ngumu kupata pesa hili linafahamika...Hizo nyumba ziache zipendezeshe mkoa na watoto wakae.
ReplyDeleteWewe mdau wa July 15, 2:52a.m. unatafuta balaa.Eti uoe mchaga ili akuhamasishe maendeleo. Utamuoa na atakuhamasisha maendeleo ila ukishakuwa tajiri anaku''kill'' na kuchukua kila kitu, shauri yako.Bora utafute kabila lako
ReplyDeleteMshauri wa bure.
Jamani! Mnateseka na kabila la wachaga hadi mankosa usingizi. Wachaga tunapenda kwetu na kwetu ni kwetu sio kwenu. Kuna kiongozi mmoja mtu ambaye tunatabia tukimuona tunasema wa maana na heshima zake kisa madaraka. Yeye alikuwa mwenyeji wa huko kwa mtoa mada huko. Alikufa, zile suti alizokuwa navaa town DSM na magari aliyokuwa akitembelea bila aibu akasema nikazikwe kwetu nikifa. Walipofika na maiti na mizigo ya wafiwa maana serikalini ni lazima kuachia nyumba ya watu. Walikwenda wakapiga hema wakazika wafiwa wakalala kwa jirani, jibaba nzima marehemu hana hata nyumba ya udongo. Jamani kwetu uchagani tumekataa hilo kabisa kwetu ukifa lazima tukate mgomba tukizike na watu wapate soda toka frijini, apige pasi, waoge maji moto, jiko la umeme au gas kwani umeme hadi msitu wa Mlima kilimanjaro. Kwa kifupi tukishapata shida utotoni hatutaki shida uzeeni tunapenda kuzeeka kwa raha na mahali penye hewa.
ReplyDeleteKaka zangu wa kichaga, msijazwe pumba kichwani, janja yao ni ili mujisikie mali sana muache kuchacharika, Kazeni uzi, jengeni kama baba zenu, walikuwa hawachagui kazi, siku hizi kuna vijana wengi sana wa kichaga ile culture ya kufanya kazi kufa na kupona imekwisha, wamebaki kujisikia tu mali, kumbe urithi tu.
ReplyDeletemwenye sikio asikie, uchagani kumejengwa kwa kazi ngumu, si kwa maneno na kujiona mali.
Wachaga wengi ambao wamekuta wazazi tayari wana mali, wanashindwa kujishusha na kuchapa kazi, wanaishia kurithi tu! hawana jipya la maendeleo
Watu hawawafahamu Wachagga, wanawaona tu. Turudi kwenye historia. Miaka ya 1890 Mangi Rindi toka Uchaggani aliwaomba Waingereza kujenga shule Kilimanjaro tena aliowaomba akawatumia na pembe za ndovu. Alionyesha vile alivyotaka elimu.Wachagga wanapenda elimu.
ReplyDeleteMiaka ya hiyo hiyo Wamasai walimkuta Mangi Marealle wa Marangu aliyejulikana kama Ndegoruo Kilamie akifanya kazi na watu wake wakampa jina Melyari yaani mchapa kazi jina ambalo Wajerumani walikuja ita Marealle.Wachagga ni wachapa kazi.
Mzungu wa kwanza kufika ukanda wa barafu wa Mlima Kilimanjaro alishuka na barafu na hapo hapo wenyeji ambao ni Wachagga wakafikiria kuiuza kama dawa. Wachagga ni 'enterprising'.
Kujenga nyumba kule kwao ni kwamba ndizo nyumba zao. Unataka warudie tembe? Yaani ni jamii iliyoendelea zamani sana. Kwa hiyo mjadala wa Wachagga na nyumba zao vijijini kwao usikupotezee muda bro.
AR toka Dar.
Nasikia wachagga hasa "wababa" ni wezi?(Narudia-Nasikia sijawahi kushuhudia).
ReplyDeleteBy David Villa back from Holiday
duh...hii imenifurahisha sana!
ReplyDeleteEti..."Wachaga ni Jews wa Bongo"...mbavu sina....kwi kwi kwi
ReplyDelete