Na John Nditi, Morogoro
WIKI ya Usalama Barabara imeanza kwa Mkoa wa Morogoro kukumbwa na jinamizi la ajali mbaya iliyopoteza uhai wa watu watatu papo hapo na wengine watatu kujeruhiwa na kulazwa katika Hosipitali ya Mkoa wa Morogoro baada ya Basi la Simba Mtoto kugongana na Lori la mizigo katika barabara ya Iringa- Morogoro.
Ajali hiyo imetokea katika eneo la Mbunga ya Hifadhi ya taifa ya Mikumi , karibu na Kijiji cha Doma, kilichopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Thobiasi Andengenye amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo .

Alisema ajali hiyo ilitokea Agosti 14, mwaka huu majira ya saa moja asubuhi kwa kulihusisha basi hilo aina ya Scania lenye namba T 820 AGE mali ya Simba Mtoto wa Tanga na ilkuwa imekodishwa na watu wa madhehebu ya dini ya Kikrsito kutoka Lilongwe nchini Malawi kuelekea jijini Nairobi, Kenya.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, basi hilo liligongwa ubavuni na Lori lenye namba T 680 AAB likiwa na Tela lenye namba T 626 AAB aina ya Scania mali ya Kampuni ya Flying Cargo , lilokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam kuelekea nchini Zambia.
Kamanda Andengenye alisema katika ajali hilo , Dereva wa Lori hilo, Aboud Hassan , mkazi wa Arusha alifariki papo hapo pamoja na Dereva wa Basi hilo, Amri Masimba , mkazi wa Tanga na abiria wa basi aliyetambuliwa kwa jina la Mary Chatahika ambaye ni mchungaji kutoka Malawi.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, abiria waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro ni raia wawili kutoka Malawi aliokuwa wakisafiri na basi hilo ambao ni Mrs Banda Mngoni (38) mkazi wa Lolongwe na Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzuzu cha Malawi, Mpasa Jabawe (25) na utingo wa Lori Daud Amani ( 22) mkazi wa Arusha.
Hata hivyo alisema hali ya majeruhi hao wanaendeleo vizuri na kuwa change cha ajali hiyo ni kutokana na uzembe wa Dereva wa Lori hili alipotaka kulipita gari jingine bila ya uangalifu na kusababisha kuliparamia basi hiko ubavuni eneo la Dereva na kusababisha watu hao kupoteza maisha papo hapo.
Panua barabara baba huko porni nafasi kibao ya kupanua all roads. Kod yaaenda wapiiiiiiiiii?
ReplyDeleteLondoner