sehemu ya barabara ya old bagamoyo road, kuchepukia mbezi beach, sasa ina lami
vibabajaji ni vya kumwaga barabara ya kawe. dala tu umefika kwako
barabara ya kawe road kupitia mbezi beach
hapa ni pale darajani palipokuwa korofi sana enzi za mafuriko. sasa ni tambarare. mtu ukitaka kwenda africana huna haja tena ya kupigana pasi na madaladala kule barabara ya lugalo


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Michu ile Africana vipi?, ndio haikufunguliwa tena mpaka leo?

    ReplyDelete
  2. HII NI ILE BARABARA INAYOPITA CHINI KWA CHINI KAWE HADI KWENYE MTO NA MBEZI BEACH CHINI KARIBU NA BAHARINI KUPITIA MAGOROFA YA B.O.T. HADI UNAKUTA BARABARA YA KWENDA AFRICANA? NAOMBA KUJUWA KIDOGO.

    ReplyDelete
  3. Madau namba mbili hapo juu....ulichohoji ndilo jibu lenyewe haswaaa....MWENDO MDUNDO MPAKA BOT FLATS......HALAFU UNAENDELEA KUYOYOMA MBELE KWA MBELE...Mzee Abson ndani ya nyumba unampita mbele ya nyumba yake ..... Na pale baharini ambako magari yalipaswa kuvuka bahari ni imebaki historia ni daraja la nguvu limewekwa....kwa ufupi HABARI NDIYO HIYO.....ila hayo magari...na huo moto wake....tahadhari za haraka sana zinabidi zichukuliwe.....speed ni 180 na kuendelea...NI HATARI TUPU!!

    ReplyDelete
  4. Inasikitisha, barabara zinavyojengwa sijui hao planners na engineers wanafanya nini, hapo sijaona sehemu ya watembea kwa miguu,iliyojengwa, ni rahisi sana mtu kugongwa na gari hapo, wala hakuna sehemu za wavuka barabara. Yaani ni hivyo hivyo kwenye barabara za kibongo, namna hii tutasonga mbele kweli? Au barabara zinatengenezwa kwajili ya magari tu?

    ReplyDelete
  5. ni aibu eti bongo tambarale, kwa wachache na walio wengi wanasurubika.

    hakuna haki za wanyonge ila wao wenyewe tu tembeeni nchi za wengine muone mtembea kwa minguu anahaki kuzidi mwenye gari,

    sasa wazee,walemavu na watoto wanapita wapi au?? madereva nao bangi mtu yaani nchi ipoipo tu inaendeshwa kisera ukiongea unamwangiwa tindi kali ufe watu waendekeze libeneke.

    halafu watu wamezoea basi wanaona yale ndiyo maisha masikini inasikitisha kweli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...