HAPPY BIRTHDAY MDAU MICHUZI!
Yaani tarehe yako ya kuzaliwa ndiyo tarehe yangu ya kufunga ndoa! Ndoa yangu leo imetimiza miaka 11! ni furaha kubwa kujua siku hiyo inahusiana na mkuu wa wilaya ya nanihii...

Ngoja nikupe Interesting facts kuhusu family yangu na celebrities!

Birthday ya mai waifu e wangu na Nelson Mandela zinafanana- 18 July
Mwanangu wa kwanza alizaliwa tarehe ya siku Mandela alipotoka jela- 11 February. Tarehe hii pia Mike Tyson alipigwa kwa mara ya kwanza kabisa katika historia, na James Buster Douglas.

Mwanangu wa pili alizaliwa siku ambayo mechi ya kwanza katika historia ya fainali za kombe kombe la dunia ilichezwa- 13 July

Wototo wangu hao wawili walibatizwa siku ya birthday ya Barack Obama- 4 August.
Ndoa yangu imefungwa tarehe ya Birthday ya Issa Michuzi- 28 August
Naona hii ni dalili ya ngekewa kwangu!
Mdau Sweden
-----------------------------------------
Mdau wa Sweden pamoja na wadau wote
napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa mpigo (sio rahisi kutaja mmoja mmoja) wote mlionitakia hepi besdei njema kwa njia mbalimbali, ya email kama hiyo ikiongoza kwani hadi sasa ikiwa ni saa kumi jioni hapa dodoma nimepokea takriban email 1800 toka kila pembe ya dunia kunipongeza kwa siku yangu hii ya kuzaliwa.
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia kufikia siku hii kubwa (umri kapuni, hahhaa, noma kutaja...) na pia kwa kunipa bahati ya kuwa na wadau kila pembe ya dunia. Ni bahati ambayo naiheshimu sana na siruhusu kamwe iiingie kichwani. Nabaki kuebdeleza libeneke kwa unyenyekevu mkubwa kwa wadau wote.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Mimi naomba kujua besdei ya hiyo tisheti na sio mwenye tisheti!

    ReplyDelete
  2. Happy Birthday mzee mkubwa. May you live to see your great grand children.

    Naona fulanazzzzz iko in full effect.
    I will be in Dar soon. Nitakutafuta nikupe zawadi.

    Thanks for all your good work in keeping us, in the diaspora, informed.

    ReplyDelete
  3. Hongera Bro Michu kwa kuendelea kuwa kibabu na kuongezea utamu siku ya tarehe 28 August ni siku muhimu katika historia ya marekani kwani ni siku Martin Luther King Jr alitoa hotuba yake ya I have a Dream..........Naona wewe ni mtu wa ngekewa tu

    ReplyDelete
  4. This is lukwa and bro just have funny and god bless you

    ReplyDelete
  5. The secret of staying young is to live honestly, eat slowly, and lie about your age

    MODESTA WATUGURU

    ReplyDelete
  6. JAMANI, SI TUTAFUTE NAMNA YA KUMPA ZAWADI MZEE MZIMA? HUTU TUMANENO KWELI ATASHIBA? MICHU, TWAMBIE ZAWADI ZILETWE WAPI?

    AIKA KISAMO

    ReplyDelete
  7. Hey! happpy birthday my brother. How aold are you?

    Manake mimi nilikua kila siku 21 again mpaka nikachoka but since nilivyo hit 30 yrs birthday yangu knimeamua kuminus badala ya kuadd you know......sasa hivi I am 25 yrs old. and last year I was 26 teh tehehehehehhhh

    Hongera kaka yangu just know that 40 ni new 30 okay ....

    ReplyDelete
  8. Mashallah Issa Michuzi Mungu akujalie maisha mazuri inshaallah. akutolea mazambi na akuepushe kwenye azabu za kaburi inshaallah ukae vizuri na mkeo na wanao inshaallah happybirthday michuzi. Mwanao Kaaziniwa au kabarikiwa sijaelewa hapo? Dk zinaenda ni nyongeza Anfield na birthday ya michuzi inatakakuharibika hapa extra time dk ni ya 26 hiyo na sec kazaa La LA Babel anageuza ila nafasi inaonekana inapotea Babel bado anapiga cross Kuyt Anagonga nyavu pembeni Ah Ala kumbe Kuyt anampa zawadi michuzi Gooooooooooooooooal. hahaha mdau Mzaramo K,koo Inshallah uzidi kufanikiwa weka Nia. Ila nakuomba jibu langu inshallah unijibu kabarikiwa au kaaziniwa?

    ReplyDelete
  9. Kesho (Ijumaa) ni besde ya Michael Jackson. Atafikisha miaka 50

    ReplyDelete
  10. hebu wadau wenzangu mnaweza kuagulia kaka michuzi anamiaka mingapi?mie naagulia miaka kama 45.eti vipi kaka michuzi nimepata au nimekosa? kama nimekosa nakupa mji nenda makka ukahiji ukirudi utuletee zawadi ya kitishart kama chako wadao wote tuwe sarsare.

    ReplyDelete
  11. Nami naomba kuungana na wadau wote ulimwenguni kukutakia hepi bethidei njema yenye baraka na fanaka tele. You make our days kaka. Mungu akupe wingi wa siku za mafanikio hapa duniani. We love you

    ReplyDelete
  12. HAPPY BIRTHDAY.LINDA BEZUIDENHOUT HERE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...