JK akisalimiana na rais wa International Conservation Caucus Foundation(ICCF) David Barron katika jengo la Rayburn building huko Washingto DC. Katika mkutano huo Mh. Baron alielezea mipango ya kujenga chuo cha uhifadhi huko A-taun. JK yuko marekani katika ziara ya kikazi kwa mwaliko wa Rais George Bush. Picha na Freddy Maro wa Ikulu
Hakuna maendeleo bila kutokomeza malaria – Balozi wa Marekani
Na Mwandishi Wetu
BALOZI wa Marekani nchini Tanzania, Mark Green amesema kuwa kamwe haiwezekani kwa Tanzania kupata maendeleo yoyote ya maana, bila kwanza kumaliza tishio la ugonjwa wa malaria na kuutokomeza ugonjwa huo.
Balozi huyo amesema kuwa ugonjwa wa malaria unaathiri mwenendo mzima wa maisha ya wananchi wa Tanzania, na kuwa kwa bahati mbaya sana, unasababisha vifo visivyokuwa vya lazima.
Balozi Green amesema hayo Jumatano, Agosti 27, 2008 wakati anamkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuzungumza kwenye majadiliano kuhusu hali ya malaria na athari zake kwa Tanzania kwenye Kituo cha Maendeleo Duniani cha Global Center for Development (GCD) mjini Washington, Marekani.
Balozi Green amesisitiza kuwa tofauti na mawazo ya watu wengi, ugonjwa wa malaria unabakia ugonjwa wa kwanza kuua watu wengi katika Tanzania pamoja na matatizo makubwa yanayosababishwa na ukimwi.
“Kwa bahati mbaya, hivi ni vifo visivyokuwa vya lazima kabisa kwa sababu vinatokea kwa sababu ya ukosefu wa raslimali. Tunazo habari zote kuhusu malaria na jinsi ya kupambana na ugonjwa huo, na jinsi ya kuutokomeza. Tatizo letu ni raslimali,” amesema Balozi Green.
Balozi Green ambaye alipata kuwa Mwakilishi katika Bunge la Marekani kwa miaka minane kabla ya kuteuliwa balozi amesema kuwa ugonjwa wa malaria ni ukweli wa maisha katika Tanzania.
Balozi pia ameelezea hadithi ya kufurahisha ya jinsi juhudi za kutokomeza ugonjwa huo zilizofanikiwa katika Zanzibar, na kusema kuwa hilo ni jambo la kufurahisha na kushangiliwa.
“Zanzibar imefanikiwa sana katika kutokomeza ugonjwa wa malaria. Ni eneo dogo na idadi ndogo zaidi ya watu,” amesema Green na kuongeza kuwa sasa changamoto ni kuhakikisha kuwa mafanikio ya Zanzibar yanadumishwa na kuhamishiwa Tanzania Bara.
Naye mmoja wa waanzishilishi wa CGD, Ed Scott anasema kuwa ameshangazwa kweli kweli na mafanikio ya kutokomeza malaria katika Zanzibar.
“Nimetembelea Zanzibar majuzi tu, na nikaonyeshwa vitanda vilivyokuwa vinalaliwa na wagonjwa wawili kwa wakati mmoja sasa viko wazi bila wagonjwa kwa sababu ugonjwa wa malaria katika Visiwa hivyo umepunguzwa kufikia asilimia moja tu ya wagonjwa wote visiwani humo,” amesema Scott.
Scott ametoa mifano ya jinsi nchi za Cuba na Panama zilivyotokomeza malaria kwa juhudi na nidhamu katika kupambana na ugonjwa huo.
Naye Rais Kikwete amesema kuwa kuna wakati alipata kuambiwa wakati alipotembelea mji wa Boston kuwa mji huo ulioko kaskazini mashariki ulitokomeza malaria mwaka 1956, ukweli ulioongeza imani yake kuwa hata Tanzania inaweza kutokomeza malaria kama itakuwa makini katika mapambano hayo.
“Hivyo hata sisi tunaweza, tukidhamiria. Na kwa hakika malaria inasumbua sana juhudi zetu za maendeleo kama alivyosema Balozi Green,” amesema Rais Kikwete.

nina wasi wasi na hiyo statement kuhusu znz. si kweli kuwa znz malaria ni 1% tu kwa hoja kuwa vitanda ni vitupu. ukweli ni kuwa waznz wengi hivi sasa wanatumia hospitali binafsi zaidi kuliko za serikali kutokana na huduma mbovu za hospitali za serikali. kwa hiyo kuwepo na vitanda vitupu mahospitalini ni jambo la kawaida kwa sasa.
ReplyDeleteaidha kuna zaidi ya 30% ya waznz wanaofuata huduma za afya tanzania bara kwa kuwa huduma huko znz haziridhishi. wakiwa bara huenda muhimbili, aga khan, tumaini, ccbrt nk. kwa hiyo takwimu hizo zilizotajwa haziwakilishi hali halisi ya znz.
ni kweli raisi wetu anajitahidi kutuletea maendeleo jamani,keep it up jk,nashauri jk akirudi kupigana na malaria pia aanzishena kampeni ya kupigana na uchafu pia,mana bongo ustaarabu hamna taka watu wanatupa ovyo tanzania bara na visiwani,suala la usafi likisimamiwa vizuri na wizara ya afya magonjwa mengine kama kipindupindu na maradhi ya matumbo yatapungua hata pnemonia yaweza kupungua.
ReplyDeletemungu ibariki tz na jk
Nani kakuambia hakuna maendeleo bila Malaria hapa kwetu. Lazima huyo aelewe Malaria ni Tropical disease,sasa anposema hayo anayosema yaani sinuelewi kabisa. Angeyasema maneno hayo Kibaki, Mseveni au Kabila ama Banda wa Zambia ningemuelewa, lakini wa kutoka USA??? aakh, aache utani, hajui kitu.
ReplyDeletebinafsi ningeona angemueleza rais wetu ya kuwa "HAKUNA MAENDELEO BILA KUTOKOMEZA UFISADI" yaani ningempa tano sana. Kwetu sisi malaria ni kama binamu tu tunaishi naye, japo sikumoja moja anachukua maisha ya ndugu humuhumu ndani, ila maendeleo yaani binamu huyu haingilii na hahusiki kabisa. Ni sisi weenyewe na roho zetu za ubinafsi, ufisadi ndizo zinatukwamisha. Nasema kama ndugu yetu huyu "MALARIA" anatukwamisha basi ni kwa aslimia kidogo sana. UFISADI jamani!!!!!
Ninakubaliana kabisa na anony hapo juu kuwa Balozi Green na Rais JK wasipotoshe ajenda tuliyo nayo. Malaria mkoloni aliikuta na akaiacha alipomaliza kazi iliyokuwa imemleta, na tukawa bado tunapiga hatua za maendeleo. Kizingiti kikubwa cha maendeleo ni hii NDOA kati ya UFISADI (ubepari uchwara vya nchini) na UTANDAWIZI (ukiongozwa na hao hao mabepari wa kimataifa).
ReplyDeleteNi kweli Maadui watatu wa Maendeleo ni Umaskini, Magonjwa na Ujinga. Lakini RUSHWA, UFISADI, TAKRIMA na KUWALINDA WALA RUSHWA NA MAFISADI NDIYO ADUI MKUBWA. Hebu fikiria hizo pesa za EPA, fikria IPTL na mabilioni yanayochotwa toka serikalini, RICHMOND, Mikataba mibovu ya Madini, Matumizi mabaya ya pesa za umma mfano magari ya kifahari kila kona serikali, TAX HOLIDAYS na misamaha mingine ya kodi, zabuni na malipo hewa... orodha ni ndefu sana. Mambo haya ndiyo ADUI MKUBWA WA MAENDELEO. Naamini kabisa kuwa pesa tunayopoteza kutokana na ubadhirifu au kuoneana haya katika kuwawajibisha mafisadi au rushwa au kuiba ingeweza kumaliza matatizo tuliyonayo. Kutowawajibisha mafisadi si uliberali wala kulinda haki za binadamu. Ni USALITI na DHULMA kwa wavuja jasho wa Tanzania. Huo ndio ukweli.
ReplyDeleteHaikuwepona na katu haitokuwepo haja au sababu ya Tanzania kuwa na KUENDELEA kuwa ombaomba (nayo ni maendeleo tukifuata falsafa za 'Kimtizamo') kama Matonya ili hali tunao uwezo kutatatua matatizo tuliyonayo kwa kiwango kikubwa iwapo tutatumia raslimali zetu na vyanzo vyetu vya mapato kwa hekma na busara. Kuigeuza nchi ombaomba ni kujidhalilisha. Ni fedheha. Ni aibu. Ni soni. Kwa nini tufikie hatua ya kuwa ombaomba kiasi hiki?
Nimesoma kuwa serikali itasaini mkataba na Marekeni ili Marekani isimamie Nishati na Maji ya nchi yetu. Tumefika mahala pabaya kabisa. Basi waiteni waendeshe nchi ileweke wazi kabisa tena dhahiri shahiri kuwa sasa sisi ni koloni rasmi. Iko wapi falsafa ya Mwalimu Nyerere ambayo mliahidi kuitumia kujenga nchi?
Umefika wakati sasa wa kuyarekebisha makosa haya ama sivyo kizazi chetu na kijacho na vijavyo vitarithi matatizo makubwa. Majuto ni mjukuu. Tusifikie mahali hapo. TANZANIA BILA UMASIKINI INAWEZEKANA. TANZANIA BILA KUWA OMBAOMBA INAWEZEKANA. TANZANIA BILA RUSHWA NA UFISADI INAWEZEKANA. WAKATI NI HUU. Tuanze sasa. Mungu Ibariki Tanzania. Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
Yaani inafungwa safari hadi marikani kwenda kudiscuss namna ya kutokomeza malaria? Mbona tuna wataalamu kibao hapo Muhimbili ambao wangeweza kudiscuss issue hii bila ya kutumia gharama kibao?
ReplyDeleteTanzania will remain poor forever!!!!
Bw. Michuzi ninaomba kutoa pendekezo kwamba kwa mada zenye maana kama hii na wachangiaji wanatoa maoni mazuri kwa lugha ya kistaarabu, je unaweza kutumia uwezo wako wa kuwa mkuu wa nanihii ukafikisha maoni haya kwa washauri wa Rais wetu. Utamaduni wo wote huwa una mahali unapoanzia na serikali huwezesha kuujenga. Huu utamaduni wa Watanzania kutawaliwa na fikira za kuomba misaada, katika mjadala wo wote wa maendeleo hadi bungeni lugha inayotawala ni 'wafadhili', 'wahisani' tunaweza kuupiga vita na tukaamua kuuzika. JKNyerere aliuita 'utegemezi'. JK akianzisha mchakato huo, historia itamkumbuka. Lakini mchakato huo una gharama zake, mojawapo ni kwamba atapoteza marafiki zake ambao ni mafisadi. Haiingii akilini tuna pesa za umma hapa ambazo the so called wajanja wanajichukulia watakavyo, kisha tunakwenda Marekani kupokea msaada wa vijisenti ambavyo haviwezi kutosheleza hata mahitaji ya shule moja.
ReplyDelete