Mwanasheria mkuu wa serikali mh. Johnson Mwanyika akisoma taarifa kwa JK kabla ya kumpabidhi ripoti ya EPA jana Ikulu, Dar. kulia ni wajumbe wa kamati teule ya kuchunguza EPA, Inspekta Jenerali wa Polisi afande Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia rushwa Dr. Edward Hosea
JK akipokea ripoti ya EPA toka kwa Mwanasheria mkuu, Mh. Johnson Mwanyika
JK akiperuzi ripoti ya EPA mara baada ya kuipokea. amesema mapendekezo katika ripoti hiyo yatafanyiwa kazi chap chap na karibu kila mtu kiroho kiko juu kusubiri hilo libeneke.
Taarifa ya Ikulu kuhusu EPA
Jakaya Mrisho Kikwete leo (Jumatatu, Agosti 18, 2008) amepokea rasmi ripoti ya uchunguzi wa upotevu wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (External Payments Accounts - EPA) katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Kikwete amekabidhiwa ripoti hiyo na Mwenyekiti wa Timu iliyokuwa inafanya uchunguzi huo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson P.M. Mwanyika.Mwanasheria Mkuu huyo alifuatana na wajumbe wengine wa Timu hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali Saidi Mwema na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Edward Hosea.
Rais amewashukuru na kuwapongeza wajumbe wa Timu hiyo kwa kazi kubwa na ngumu lakini nzuri.
Rais, baada ya kuwa ameisoma na kuitafakari ripoti hiyo, ataitolea maamuzi katika siku chache zijazo, na taarifa rasmi ya maamuzi hayo ya Rais itatolewa kwa wananchi.
Timu hiyo iliundwa na Rais Kikwete Januari 9, mwaka huu, 2008 katika tangazo rasmi lililotolewa kwa waandishi wa habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo.
Wakati anaunda Timu hiyo, Rais aliipa muda wa miezi sita kukamilisha kazi yake, ambayo ilikuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa fedha zilizolipwa isivyo halali zinarudishwa.
Rais aliunda Timu hiyo baada ya kuwa amepitia Taarifa ya Ukaguzi wa Hesabu za Mwaka wa Fedha 2005/06 za EPA katika Benki Kuu Tanzania (BOT), uliofanywa na Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young, kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Kampuni hiyo ya Ernst and Young iliombwa na Serikali kuifanya kazi hiyo. Iliianza Septemba, 2007 na kumalizika Desemba, mwaka huo huo, 2007.
Rais Kikwete alikabidhiwa Taarifa hiyo Januari 7, mwaka huu, 2008 na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali.
Siku ya tatu, baada ya kuwa ameisoma na kuifanyia kazi, Rais aliitolea maamuzi Taarifa hiyo, ikiwa ni pamoja na kuunda Timu ya Mwanyika.
Imetolewa na
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Agosti, 2008

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. MAALIM ISSA POLE KWA YANAYOKUSIBU KATIKA SHUGHULI ZA MTANDAO WA “JAMII”. TUNASHUKURU KWA PICHA “MAHIRI” YA MHESHIMIWA “J.K” NA “WALIOMZUNGUKA”.

    USTAADH ..J.K.. NAONA “NYARAKA” ZIMEZUNGUKA KUANZIA “BUNGENI”, MPAKA ZIKAFIKIA “MIKONONI MWAKO”.…..MAMBO YA ”..SWAHIBA..” HAYO YAMETAPAKAA HUMO NDANI….GHABARI KUBWA !!!….. “..SWAHIBA WANAMARADHI..” NA DAWA YA MARADHI NI “..TIBA..”. LAKINI…..INASEMEKANA KWAMBA… “..KINGA NI BORA KULIKO TIBA..”… NA NANIHII….” IS ON YOUR HAND..”

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...