Hongera kwa kuendeleza libeneke la salamu kwenye blog yako pamoja na dhoruba za hapa na pale zinazokupata ukiwa safarini.
Mkuu jana nilikaribishwa kwenye menu safi na Host family wangu hapa Fukui , Japan .
Main dish ilikuwa samaki, kulikuwa na aina nyingi za samaki kuanzia wabichi , waliochemshwa na waliokaangwa.
Alinifahamisha kuwa samaki wabichi( huitwa sashimi kwa kijapani na huchovywa kwenye kimiminika kinachoitwa Shoyuu source ) ni wazuri kwa afya kwasababu hakuna madawa yeyote yale yalitumika kumkuza hivyo mwili wako unakuwa safe zaidi na pia husaidia kuishi maisha marefu zaidi.
Nilijaribu kumdadisi ni vitu gani vingine wanavyokula vibichi alinieleza kuna ni nyama ya farasi ,liver ya ng*ombe.Nimeambatanisha pia picha ya konokono wa baharini , sashimi na menu yenyewe.
Mkuu wa mkoa niliweza kula na tumbo halikuharibika hata chembe .
Sasa swali langu, je kule nyumbani especially watu wa pwani je wanayo destruri ya kula samaki wabichi ,
je ni eneo gani hasa ...? Na je, tunayo desturi ya kula nyama mbichi....?
naomba maoni ya wadau wa globu hii ya jamii ili waweze kunipanua kimawazo ...
ama kweli tembea uone ...
Mzumbe Boy ,
Fukui Ken ,
Japan
Hawa samaki wabichi wanatengenezwa kwa utaalamu na umakini wa hali ya juu ili kulinda afya ya mtumiaji,i.e hakuna uchafu n.k.Kuhusu faida yake kwakweli alichosema mwandishi ni sawa kabisaa. Na hapo hukutani na mambo ya mafuta sijui ya kupikia,chumvi....Na kuna kitu kingine wakati wa kula huyu samaki unamla na kitu kiitwacho "wasabi".
ReplyDeleteKwanza sisi watu wa Pwani hatuna jina la konokono wa baharini.Sisi tuna kitu kinaitwa "kome". Tunakula makome baada ya kuyapika.
ReplyDeleteHalafu hivi hao wajapani hao samaki wanaokula wanawaita samaki wapichi au samaki ambao hawajapikwa au wanawaita samaki tu.
Sisi watu wa pwani hatuli samaki ambao hawajapikwa kwasabau tukifanya hivyo tutakosa utamu wa samaki ambao ni kumla pamoja na kufyonza kichwa chake na miba.Sasa wajapani wanayakosa hayo.Pia sisi watu wa pwani tunapenda "kuunga" vyakula vyetu(kuweka spices na pilipili na mashengesha mengine). Sasa kama tutakula samaki bila kumpika au kumkaanga tutakosa kuweka jivyo vitu.
Sayonara.
Wasalimie jamaa wa nanihii moto.
Madau wa hapo juu ..umesema kuwa samaki unamkaanga ... scientifically means utatumia mafuta kumkaanga huyu samaki hapo ujue tayri unaongeza unnecessary cholestral into your body ..maisha yako hapa duniani yanakuwa mafupi. Ni vyema kula vyakula vya mchemsho zaidi vinavyotumia mafuta .
ReplyDeleteDr . Madinda
Okinawa, Jp
Onaka suita tabetai!!!
ReplyDeleteOishii!!!
ReplyDelete