Ndugu MICHUZI,JIACHIE,TZUK,MJENGWA NA HAKINGOWI
watanzania wote wa kila pande za dunia wanakufuraia kwa kuanzisha mtandao wenye habari motomoto za kote duniani na tukiamngalia namba ya watanzania wanaoingia katika blog yako ambao karibu wanafika millioni 5 hiyo inaonyesha ni jinsi gani ya kazi nzuri unayo ifanya. tunakushukuru saana.
Tatizo kuna mtu tumeanza kumtafuta na tunaomba wananchi na watanzania wema,wastaarabu wajitokeze na kutuambia huyu mwenye blog ya utamu ni nani ? na anaishi mji gani? ili hatua za kisheria zichukuliwe zidi yake haraka iwezekanavyo. huyu jamaa yuko hatarini kuwatia matatizoni nyie wote wenye blog zenye mambo mazuri kama mfano hakingowi, jiachie,tzuk na blog,mjengwa na nyingine nyingi tu.
huyu jamaa amekua anaweka picha kwe nye hata blog zenu halafu anaziweka kwake za watu bila idhini za wenyenazo na hana haki ya hizo picha ,amekua anahusika ubadilishaji wa picha za watu na kuwaonyesha wakiwa watupu,huyu jamaaa,amekua anawacha watu watukanwe na kwa vitendo kama hivyo polisi wanaommba msaada wa wananchi waishio tanzania kumuweka hadharani ili achukuliwe hatua endapo hata toa picha za watu wote kwenye blog hiyo ya kipuuzi.
Kwa upande wa watanzania waishio Marekani na U.k nao wanaendelea na uchunguzi wao maana watanzania waishio hizo pande mibli za dunia ndio wamekua saana wanawekwa kwenye hiyo blog kwa ajili tu ya kukashifu watu wasio hata wafahamu.
tunaomba msaada wako tumtoe huyu mtanzania asie kua na heshima kwa jamii ya kitanzania.kwa kuweka upuuzi wake tayari kuna ndoa zimevunjika na zingine zikiwa na migogoro mikubwa hivi sasa tunaomba msaada wako na utuwekee tangazo hili mwenye taarifa yeyote kuhusina na swala hili wasiliana nasi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 31 mpaka sasa

  1. Broo mimi naona ungetafuta kazi nyingine ya kufanya maana sioni point ya muhimu uliyosema so wakiNA HAKI NGOWI NA MJENGWA NA TZUK muwachukulie hatua za nini zisizokuwa na mpango wa maana???First kabla hujaongea jaribu kufikiria nini sio kwamba tutaogopa kukuambia kwa vile polisi au vipi hiyo kazi yako sisi haituhusu kabisa ila hizo blog ulizotaja naona kama hazihusiani kabisa na UTAMU so ingekuwa vizuri zaidi kama ungefanya utafiti wa maana ila sio kuwaingia wakina NGOWI na wengine kwenye maswala ambayo hayawahusi...Pia mimi kwa mtazamo wangu ni kwamba huyu utamu sidhani kama anaweza kuwa BONGO,,U.K AU U.S maana asingeweza kufanya hivyo vitu ila fanya utafiti wa kina zaidi ila ukisema uchukulie sheria mkoni kwa vile zile blog zipo pale sioni kama utakuwa umeongea point hapo na pia sidhani kama kuna mtu atakusapoti hapo....

    ReplyDelete
  2. mbona haujaweka jina lako....na wewe unamuogopa jamaa nini? tanzaniadodoma ndiyo nini?

    ReplyDelete
  3. Usahuri wangu ni kwamba tumeni email kwenye kampuni la Google kueleza duku duku zenu na wao wataifunga hiyo UTAMuuuuuuu blog.


    Email yao ni: gmail-abuse@google.com

    ReplyDelete
  4. Nilisahau ...pia munaweza tuma malalamiko kwenye website hii
    http://help.blogger.com/?page=troubleshooter.cs&problem=&contact_type=Spam&Submit=Submit

    ReplyDelete
  5. Mjinga wewe wa juu na wewe wa pili, amesema wasiliana nasi unataka jina? Nasi na sio nami, au unataka majina mangapi? Pia kazi ya kipolisi haifanyiki udhaniavyo, yani aandike ni polisi gani asa uyo anayetafutwa si atakimbia.
    We unaonekana ni mdau wa Utamu na ujinga wake, utachomwa tu huna lolote.
    Mi sifahamu utaratibu ila kwa Google hawaEndorse wala Kureview content lakini wanasema wakifosiwa na vyombo husika wanaweza, huyu jamaa anahatarisha amani lazima abanwe. Period.!

    ReplyDelete
  6. Ebana we mgeni kwenye teknolojia au?
    mbona rahisi sana ku-track mmiliki wa website yuko wapi?

    Badala ya kuomba msada kwa wadau wa blog tangaza tenda na utoe dau la maana, nakuhakikishia ndani ya masaa 24 huyo mtu anapatikana.

    ReplyDelete
  7. Alaf ukitaka kujua watanzania wengi tulivyokuwa ma perverts chekshia watu kibao watakavyomtetea utamu manake wanajua ikifungwa watakosa sehemu ya kwenda kula chabo.

    ReplyDelete
  8. nimetembelea hiyo blog ya theutamu na kugundua yafuatayo.

    Kwanza, zile picha za wabongo (hasa zile zinazoonyesha wako kwenye parties etc), zinaonyesha wazi utulivu ni zero, ingawa kwa kiasi fulani naweza kukubaliana na usemi "dont judge a book by its cover".

    Pili,zile comments zinazotolewa kule ni za watanzania nyinyi nyinyi mnaoishi hko ughaibuni kwa kuwa mnajijua maisha yenu. Mule mnatolewa hata siri za wengine za chumbani, unanikumbsha wimbo wa wagosi wa tanga kunani pale wanaposema "watu wajua mpaka siri zako za ndani, sijui habari hizi wameambiwa na nani". Sasa sijui huko UK na US kumegeuka Tanga?

    Tatu, nimetembelea hizo blog nyingine za hakingowi, tzuk na nyingine, zile picha za utata zilizoko kwenye theutamu hazitoki kwa hizo blog zilizotajwa kama tuhumiwa. Hii inaonyesha nini? Inaonyesha kuwa majority ya picha za kwenye utamu zinatoka kwa watanzania wenyewe waishio huko US na UK, inayomaanisha kuwa kuna magomvi makubwa between wabongo kwa wabongo waishio huko. Hasa wanawake, tena kwa visa vya kuchukuliana wanaume.

    Conclusion ni kwanza watanzania muishio nje pendaneni. Mkipendana theutamu hatapata picha za kuweka kwenye blog yake.

    Au ni kweli kuwa maisha yenu ya huko ni machafu sana mnaona haya sasa tuliobaki huku tunayajua sasa?
    Kumbukeni dunia ni kijiji sasa.

    Namaliza kwa ku quote msemowa kaburu mmoja katili enzi zile za ubaguzi wa rangi, alisema na nukuu:
    "black people are more racist than white people, because black people are racist toward other black people"

    ReplyDelete
  9. ANON WA KWANZA HUJAMUELEWA HUYO JAMAA. YEYE HAKUSUDII KUWA HAKINGOWI MJENGWA NA TZUK WANA UHUSIANO NA UTAMU, BALI ANAKUSDUIA KUWA HIZO NI BAADHI YA BLOG ZANYE HESHIMA NA ZINZOKUBALIKA IKIWEMO YA MICHUZI. HIVYO UNAPOCOMMENT SOMA KWANZA HABARI UIELEWE.

    PILI HOJA YA HUYO JAMAA PAMOJA NA KUTOTAJA JINA LAKE LKN NI YA MSINGI. KUNA HAJA YA WALE WANAOWACHAFULIA WATU MAJINA YAO KUCHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA. MIMI NADHANI NJIA NI RAHISI YA KUMPATA MHUSIKA IWAPO WATAULIZWA WALE WENYE MITANDAO AMBAYO PICHA ZAKE HUWEKWA KWENYE UTAMU KAMA GLOBAL PUBLISHERS. WAULIZWE HIZO PICHA ZAO KUTOKA KATIKA MITANDAO YAO ZINAWAFIKIAJE UTAMU LABDA WAO WATAKUWA NA MSAADA MKUBWA WA KUMPATA HUYO UTAMU MWENYEWE.

    ReplyDelete
  10. UTAMU,yuko afghanistan,analindwa na TALIBAN,kazi kwenu

    ReplyDelete
  11. UYU ALIYETOA TANGAZO NI UTAMU MWENYEWE YUPO KWENYE HARAKAT ZA KUJITANGAZA KWA NJIA AMBAYO AMUWEZ MTAMBUIA

    ReplyDelete
  12. wewe mdau wa kwanza kabisa mimi naona wewe ndiye hutumii akili, unakurupuka tu bila kusoma na kuanza kulalamika...jamaa adadai kwamba "....huyu jamaa yuko hatarini kuwatia matatizoni nyie wote wenye blog zenye mambo mazuri kama mfano hakingowi, jiachie,tzuk na blog,mjengwa na nyingine nyingi tu...." na hajasema kuwa hizo blog zina uhusiano na huyo mpuuzi. kwa habari nilizozipata ni kwamba watu tayari wanamfanyia kazi huyu jamaa Tanzania, na hata kule USA inasemekana wameshamripoti kwenye vyombo husika, na watu wote wanaotuma comments za kutukamna watu watatafutwa...inasemekana kuwa watu wanakwenda Library ili kutuma hizo comments ila wanasahau kuwa wanatumia kadi zao za Library kulogin kwenye kompyuta (hii ni kwa watu wa USA)....anyway, jamaa atapatikana tu...ila kama kuna mtu anamfahamu, basi siyo vibaya kutoa taarifa...siku zote za mwizi huwa ni 39.

    ReplyDelete
  13. Jamaa anakosea pale anapochukua picha za watu walio uchi kwenye tovuti za ngono na kubandika sura za watu wengine...lakini mimi ninawalaumu watu wanaomtumia picha hizo kutoka washington DC na UK. mambo wanayoyafanya watu wa huko yanatia aibu sana. wanatukana hata watu wazima si laana hiyo jamani? kuweni jamani tunawategemea nyumbani.

    ReplyDelete
  14. EXCUSE MY FRENCH.

    Ndugu mheshimiwa uliyeomba msaada wa kumjua utamu na hatimaye kumdhibiti naomba nikusaidie kidogo.

    Usijaribu katika maisha yako, kuwaonyesha watu wewe ni limbukeni kiasi gani.

    Kabla hujaingia kwenye blog, kuna onyo kali sana kuwa maudhui unayokaribia kuyaona inawezekana hayafai, sasa una uhuru wa kuendelea kuyaona au kuacha. Kama umechagua kuendelea kuyaona basi usipige kelele.

    Ni ujuha uliokithiri kwa wewe kuomba msaada wa kumkamata utamu, unahangaika sana kwani unacheza ngoma usiyoijua. Kama polisi wanashida naye it won't take more than 6 minutes to arrest him.

    Jaribu kuwa muwazi, wewe mwenyewe jina lako na physical contact zako hujazianiaka sasa tukusaidiaje?

    Unapo andika kitu kwa jumuiya andika kama msomi na chambua mada.

    Ningekuelewa kama ungesema, mfano " utamu ametoa picha au maelezo ya watu 200, kati ya hao una hakika 23 wameonewa kwa sababu, 1,2,3,4,5,..... na ukweli ni huuuuuuu, ushahidi wake ni huuu."

    Hebu weka wazi, ni ndoa ngapi zimevunjka? na ndoa ya nani umefikiria imevunjwa bila hatia?

    Simtetei utamu wala simjui, lakini anachofanya inahitaji apongezwe, kwani anamulika jamii, utamu hana tofauti na kipindi cha radio tanzania miaka ile ya 80 kiitwacho "MIKINGAMO NI SIKIO LA UMMA"

    Kazi ya utamu ni kudeliver message anazoletewa ili kama kuna mapungufu kwenye jamii yarekebishwe na si vinginevyo.

    Upumbavu wa kuja mnasema sijui kufanyeje fanyeje ni utoto, wanawake kibao marekani na uingereza ni malaya tu na wako so cheap, ni aibuuuuuuuuuu, lakini pia wako madume wazinzi sana, sasa kama hawa wanaume mnawafumbia macho ni shauri yenu, lakini ukweli lazima uanikwe.

    Naweza nikakubaliana nawe kwa point moja, tathmini ifanywe kwabla mtu/watu hawajalipuliwa, lakini sidhani kama unasema utamu amekosea simply because, on display there is a photo of your sister, mother or aunt. Kama kweli ni vyangu, what's wrong?

    Utamu:
    These are the challenges, without them you'll not be there.
    What needs to be done is, may be to verify any contents or photos prior to them being published.

    So far, you are doing a veru good job, we will appreciate if you will furnish us with more photos ili tujing'ate ulimi.

    Keep it up. BRAVO BROTHER

    NTOMBIWASUNGU BUKUNENEZA,
    VANCOUVER, CANADA

    ReplyDelete
  15. SASA WEWE NDIO UMETUMWA NA HAO POLISI?

    TAFUTA KAZI NYINGINE YA KUFANYA, ULISHAAMBIWA UKIFUNGUA DIRISHA UTAINGIZA NDANI ZAIDI YA HEWA SAFI, INZI NA VUMBI PIA VITAINGIA HIVYO NI BORA UZOEE TU HUU UHURU MPYA WA WATANZANIA.

    ReplyDelete
  16. You are right hana haki kuweka picha bila idhini yao na hana maadili ya kiandishi huyo mtu. what you can do is report the blog kwa their provider. am sure somewhere on the blog you can have that or if not find their provider and report them listing your reasons and the blog would automatically be suspended until investigated

    ReplyDelete
  17. huyo utamu kwanza picha anzoweka hata hao watu hawavutii...mabaka wengien sijui ya wapi yani hata huo utamu anauona kuziona kidogo akili itakua imemruka. kama anaweka picha za uchi basi aweke watu wanaovutia jamani sio utumbo wakuwapa watu nightmares

    ReplyDelete
  18. kusema kweli watu wote wabaya kuanzia utamu mwenye blog mpaka waliotoa maoni na kutoa siri za ndani za watu.
    NA SWALI MOJA TU WATU WAHUSIKA WAJIULIZE,JE NI NANI HUYU AMETOA SIRI ZANGU ZA CHUMBANI?NINA HUAKIKA MAMBO YA CHUMBANI HUFANYWA NA WATU WAWILI TU.SASA HAPA KATIKA KUANGALIA NI KWAMBA KUNA UWEZEKANO MKUBWA MARAFIKI KWA MARAFIKI WATOLEANA SIRI ZAO KWA VILE HAWA WEZI KUJULIKANA."RAFIKI YAKO ANAWEZA KUA HADUI WAKO".
    kama kuna uchafu wote watu wanafanya waliokuwa majuu basi hio ndio aftermath yake.
    kufanya hadithi hiwe fupi ni kwamba utamu blog ilikuwa na advantage na disadvantages zake.
    advantages:
    1.itawezesha watu kurekebisha tabia.
    2.watu watakuwa wahaminifu kwenye ndoa zao na italeta mapendo zaidi na ndoa kudumu.
    3.itasaidia kupunguza magonjwa ya zinaa kwani watu watajaribu kutulia na mpenzi mmoja.
    4.itarudisha mapenzi kwa watanzania kwani watu watajirekibisha tabia zao.
    5.watu watakua wanajieshimu popote walipo.
    6.itasaidia watu kufocus na maisha yao zaidi ya maendeleo na kuachana na upuuzi wote waliokuwa wanafanya kama ni kweli yalioandikwa.
    disadvantages
    1.kuvunjika kwa ndoa kama kweli wahusika waliotajwa wamefanya mambo hayo.
    2.watu kusingiziwa kwamba wao ndio walioa siri zao wakati labda sio wao.
    3.kujenga chuki katika jamii ya watanzania.
    cha maana sasa hivi viongozi wote wa jamii za watanzania huko u.s.a na u.k wahitishe mkutano hili waweze kupatanisha watu na kurudisha upendo katika jamii zao.
    na huyu utamu swala lishughulikiwe hili glob yake ifungwe kwani haiendani na maadili ya mtanzania.
    wasalaaam na watakia watanzania wote maisha mema ya amani na upendo popote na tujiandae kuukaribisha mwezi mtukufu wa ramadhani.

    ReplyDelete
  19. Wewe naona unapiga debe bure, unapoteza muda wako, hii ni dunia ya Information, technology and communication au post-modernity. kila mtu ana uwezo wa kuweka duku duku zake, fikra zake, mawazo yake, habari yoyote aliyonayo kwenye the world wide web!!!! hakuna mtu yeyote mwenye IMMUNITY kwenye internet!! Obama, Blaire, Bush, Britney Spear, Naomi, Angelina Jolie, Fatuma, Rukia, Athumani, kamugisha, etc etc woote wkitetereka siri zao za ukweli na zisizokuwa za ukweli zinamwagwa hapa kwenye HTTP://WWW.
    Unless wahamie China. Na China nako kutabadilika tu

    K

    ReplyDelete
  20. Unachekesha sana, kwani ni lazima awe mtanzania? mimi nimekutana na website kibao za kiswahili ambazo si za watanzani, za wa-USA, wa-UK tena owners wazungu na zinamatusi tupu wengi wao ni njia ya kujifunzia kiswahili, achana na hilo pia kuangali web yoyote i hiari ulazimishwi, kama watu wanaachana simply because ya website basi wangeachana wengi huku Ulaya, pia wen host wanaiona hiyo web kama ingekua si sahihi wangeifunga siku nyingi sana, kuna web za matusi kibao na mbaya zaidi ya hiyo ya utamu hata kama utaifunga haitasaidia kitu chochote, pia kama unataka ifungwe au kulalamika it is such simple job to do contact host and file your complaints na ninahisi ni google.com wasiliana nao hao and frm there you can see how to go about, lakini unachofanya hapa sasa ni kwamba unaitangaza na watu wengi wataitembelea sasa kuliko awali ni hiyo ndiyo huluka ya binadamu hupenda kutenda au kuangali vitu ambavyo wewe unasema si vizuri, let the world be as it should be not the way you want it be. INAONEKANA JINSI GANI UMGENI KATIKA UTANDAWAZI, TATIZO LAKO NI RAHISI SANA KULI-SOLVE HATA BILA YA TANGAZO LAKO.

    ReplyDelete
  21. JAMANI NAOMBENI HIYO LINK YA THE UTAMU NA MIMI NIJIE THE UTAMU WA MACHO YANGU MBONA WACHOYO HIVYO HALAFU KAKA MICHUZI WANGU NIMECHELEWA KUKUTUMIA BIRTHDAY WISHES NAJUA UTANISAMEHEE.NAKUTAKIA MAISHA MEMA BABA YANGU NA MUNGU AKUJALIE MAISHA MEMA DAIMA NA UPENDO KAMA ULIYONAO UJUMBE MUHIMU WATANZANIA TUACHE CHUKI IMEKUWA MBAYA SANA KWA SASA YAANI VIUGOMVI VILIANZA TARATIBU SASA HIVI IMEKUWA SIJUI NDIO MNASEMA BEAF AU BEFF MIMI KIINGEREZA MAYOLO DOI TAYEEE

    Mtanzania mpigania amani

    ReplyDelete
  22. Kama kawa hayawani hajifichi,wewe kama ulikuwa hutaki kuonja utamu ilikuwaje ukaitembelea hiyo blog?.kila mtu anajua kuwa kabla hujafungua hiyo blog kuna tahadhari kuwa uendako kuna utamu,tena inauliza kama uko teyari kuonja utamu bonyeza hapa na kama unaona haoko teyari bonyeza hiyo sehemu nyingine ambayo nadhani hata baba mtakatifu benedict 16 hawezi kuibonyeza.sijui kana unaelewa maana ya hiyo tahadhari? kwa manufaa yako kama ulikuwa hujui ni kwa ajili ya wehu kama wewe ambao huwa wanachanganyikiwa kwa utamu na kuanza kufikiria mambo kama yako.hakuna mahakama hapa duniani itakayo sikiliza kesi yako na usipo angalia unaweza kufungwa wewe au ukalipa faini kwa kuisumbua mahakama hii yote ni kwa sababu ya ile tahadhari iliyowekwa pale.inavyo onekana uko bongo na ninavyo jua mimi ni kwamba hela inanguvu kuliko mahakama hapo bongo, na hao polisi ambao umeongea nao wanakuyeyusha kwani wanaongoza kwa kuitembelea hiyo blog,si unakumbuka walikuwa wanaambiwa wawakamate changudoa waliokuwa wakiuza miili yao,unakumbuka mahakama yao(changudoa) ilikuwa wapi? kama hukumbuki nitakukumbusha ilikuwa kwenye magari yao hao polisi, unajua jaji alikuwa nani? jaji alikuwa mtu maharufu sana anaitwa URODA.Toa boriti kwenye jicho lako ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwenzako, kwa maana nyingine zichome kwanza moto hizo dvd na magazeti ya ngono uliyo yajaza nyumbani kwako na uache kulipa pesa kwenda cafe kuangalia utamu.
    Mwana mtoka pabaya wewe

    Mbega

    ReplyDelete
  23. YAANI SIWEZI KUAMINI KUNA WATU WANAMTETEA HUYU JAMAA !!!!!HIVI MNGEKUWA NI NYINYI SURA ZENU ZIMEWEKWA KWENYE PICHA ZA NGONO AU MZAZI WAKO AMETUKANWA MATUSI YA NGUONI NA KUSINGIZIWA AMELALA NA FULANI, HIVI KWELI MNGEMTETEA HUJU JAMAA?

    ReplyDelete
  24. WALE WOTE MNAOTETEA UPUMBAVU WA UTAMU NGOJA MAMA ZENU AMA BABA ZENU AMA DADA ZENU WAWEKWE HUMO NDIO MTATIA KILI, NA WENGI WANAOMTETEA HUYO UTAMU NI WAGONJWA WA AKILI NA NI MA PERVET ,KAZI YAO NI MAMBO YA NGONO TO HUO NI UGONJWA, WASHENZI KWELI NYIE

    ReplyDelete
  25. Anonymous wa august 28,2008 saa 2:44 wa Vancouver Canada.Wewe sio una mtetea huyo the utamu mwanzo alikuwa anaweka picha za kurekebisha tabia lakini sasa kazidisha,anatoa picha za wa2 hi5,facebook na website nyingine alafu unasema anarekebisha tabia gani?ww anonymous wa 28,2008 2:44pm subiri aweke picha ya dada yako au kaka yako wanavyo rukiwa au mama yako yupo uchi ndio utajua anarekebisha tabia.

    ReplyDelete
  26. Wow!!!!! mimi naona wala usingeweka habari hizi huku kwa vile ni kama unaitangaza hiyo blog. Mimi nilikua wala sijaiona hii blog wala kuisikia ila leo macho yamenitoka.

    Ila nilichogundua ni kuwa
    1. Picha unzosema zinatoka kwenye hizo blog hapo juu nimeziona/kama zipo chache ni za kawaida yaani public view ila watu wanaotoa comments ndio haoa hao sijui waliozituma aua la.

    2. Nyingine zinaonyesha zimetumwa na watu kama kurevange au kutoa hasira. Ila muhusika wa hiyo blog naona yeye nazipokea tu.

    3. Kuna moja tu kati ya zote nimeona imekua edited. Ingawaje huyo editor mwenyewe hata kazi haijui. Utaona kabisa tofauti.

    4. Watoto wa shule bongo huko mliokuwa sexual active mapema kuweni macho. Hizi simu za camera siku hizi mwisho wake ndio huo. Picha ni forever wadogo zangu. Na wanaume wasio na akili ndio hao wanawaweka huko kwenye hiyo blog

    5. Ukiangalia hapo kwenye hiyo blog. Legal wise it is hard to get him. Ingekuwa ni child porno kweli wangeifunaga lakini hiyo kuifunda sio rahis kwa vile huyo mtu ameweka warning kuwa site yake ni adult only kwa hiyo wakiangalia na kuona hamna watoto mikono yao imefungwa.

    6. Internet international law bado haijakuwa vema. Huyo mtu nchi yeyote aliyopo atakayeweza kumshitaki na kufika popote ni kama wanaishi nchi moja othewise ni shida sana.


    7. Mtu ukienda party na kama hukuaga au hujavaa vizuri kama unavyojulikana jitahidi mtu asichukue picha yako. Picha za walio kwenye party who knows nani kazituma huko. Kikulacho kiko nguoni mwako.

    8. Cha muhimu ni kuacha kuingia kwenye hiyo site huko tu na kumwachia ajiwekee diary yake mwenyewe tu na kujifurahisha mwenyewe.

    ReplyDelete
  27. hii blog haitaondolewa kwa sababu zifuatazo (1)ingekuwa hilo jambo la kuvunjika kwa ndoa limeanzishwa na hiyo blog basi tungeweza kuyafikiria kwa umbali hayo maombi yako. lakini tunavyo jua sisi ndoa zimeanza kuvunjika toka enzi ya adamu na eva,(2)sizani kuwa kila blog inayoweka picha za watu imepata idhini ya hao watu, (3)kuna blog na website nyingi tu ambazo zinajishughulisha na mambo mengine kwa hiyo sidhani kuna aliekulazimisha kutembelea utamu,
    (4)kitendo chako cha kuomba huu msaada umeifanya utamu kuwa maarufu zaidi kwani kuna ambao walikuwa hawaitambui lakini sasa wanataka kuijua,(5)kwakuwa utamu inapatikana mara moja ukiandika utamu kwenye google basi inamaanisha imefaulu viwango vya kimataifa kuwepo,(6)utamu ni kama alkaida ya osama kwani haina phisical location na ina mawakala wengi tu ndiyo maana ina picha za kila mji hapa duniani (7) utamu imekuwa hewani muda sasa naona ulikukwa hujaistukia na ina wapenzi wengi sana na hawajawai kulalamika,kwa lugha nyingine ni chombo cha kupeyana utamu kwani inashauriwa ukisha pata habari mbali mbali kupitia kwa michuzi na mdogo wake basi umalizie kwa kuitembelea utamu ili u make u r day.
    tahadhari naomba ukae kimywa kwani ukija kugundulika utakoma na kama ndiyo hiyo ndoa yako ya ndoano unayoichunga tutaiweka kwenye www.

    ReplyDelete
  28. Mimi nionavyo Wewe ulietoa wazo hilo kwanza kabisa TOA JINA LAKO KAMILI........Unaogopa nini?

    Na wewe nadhani una mapungufu kwa kujificha ficha

    ReplyDelete
  29. BELOW NI CONTENT WARNING UNATAKIWA KUBONYE KABLA YA KUINGIA UTAMU, SASA SIJUI MNALALAMIKA NINI WAKATI MNAKUBALI WENYEWE AU HAMJUI KIZUNGU? KWA TAARIFA YENU UTAMU WANAINGIA WATU KIBAO WENYE AKILI ZAO, PROFESSORS, LAWYERS, ENGINEERS, DOCTORS ETC. NA TENA WANAIFURAHIA KWA SANA.

    Content Warning
    The blog that you are about to view may contain content only suitable for adults. In general, Google does not review nor do we endorse the content of this or any blog. For more information about our content policies, please visit the Blogger Terms of Service

    I understand and I wish to continueI do not wish to continue

    ReplyDelete
  30. [b]Wewe usitake kutuleTea habari zako za kishamba hapa kwanza umeshasema MSAADA KWENYE TUTA sasa kweli wewe unaakili timamu mind your business usipende kudandia mambo kwa vile utaumia jaribu tena nadhani pale kuna kitu kinakuambia kabla ya kuingia so itakuwa vigumu sana kuweza kumkamata utamu pia nadhani utamu sio yeye yupo peke yake bali wapo nchi mbali mbali so utafanya kazi ya bure kaa chini watafutie familia yako hela ya kula usipende kufanya vitu ambavyo havina faidi kwa familia yako nadhani yangu hayo tu...Na wengine acheni ushamba kwanza mliombwa kuingia utamu...[b]

    ReplyDelete
  31. Michuzi umeona hilo?? advert la nguvu duh ! utamu kiboko

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...