SHIKAMOO UNCLE MICHUZI,
MIMI NAITWA SOPHIE NAOMBA MSAADA WA USHAURI KUTOKA HUMU KWENYE BLOG HII YA JAMII.
MIMI NA UMRI WA MIAKA 19 NATARAJIA KUANZA MASOMO YA CHUO KIKUU MWEZI UJAO NIMECHAGULIWA CHUO KIKUU DODOMA KWENDA KUSOMEA SOCIOLOGY,WAKATI HUOHUO NIMECHAGULIWA PIA KWENDA KUSOMEA SHERIA MZUMBE LAKINI KITENGO CHA SHERIA KIKO MBEYA, SASA SIJUI NIFANYEJE NIMESHINDWA KUAMUA NICHAGUE KOZI GANI.
YAANI KATI YA HIZI MBILI IPI ITAKUJA KUNISAIDIA ZAIDI HUKO BAADAE?OMBI LANGU HUMU KIJIJINI KWAKO WAMO WASOMI WENGI WANAWEZA KUNISAIDIA KWA MAWAZO YAO, KWAKUWA WANAO UPEO MKUBWA NA WANAJUA NINI DUNIA YA SASA INAHITAJI.OMBI LANGU NI HILO TU.
UNCLE NAOMBA EMAIL ADDRESS YANGU USIIBANDIKE HAPA.
ASANTE SANA
SOPHIE.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Sophie acha kupoteza muda na kutafuta ushauri katika hili,ukweli nikwamba KASOME SHERIA,hiyo Sociology soko lake la ajira si zuri saana,na hata kama utapata ajira sidhani kama utaipenda kiivyo,kama sheria.
    please nenda Mzumbe kasome mama na kila lakheri.

    ReplyDelete
  2. Mie nahisi nenda kasomee sheria.
    Kwanza Chuo cha MZumbe kinatajikana sana kwa upeo wa usomeshaji na uzoefu hasa katika sheria.
    Pili nahisi kuwa muelekeo wa Tanzania ya kesho sheria itakuwa ina soko zaidi kuliko mambo ya sociology.
    Kwahiyo nafasi ya kwenda kusomea sheria kwa msichana kama wewe ni nzuri zaidi.

    ReplyDelete
  3. Sociology hailipi dada yangu.Achana na hiyo kitu kabisaa nawajua waliosomea sociology wanaishia kufanya kazi zisizo za walichosomea.KWa maoni yangu kasomee SHERIA.

    ReplyDelete
  4. Tanzania inawanasheria wachache sana wa kike,so husipoteze muda nenda mzumbe kasome sheria Mdada!

    ReplyDelete
  5. dada sophie bora usomee sheria, kuna kazi mingi sana za kuhukumu mafisadi, social service kwa nchi yetu bado hatuna hicho kitengo, soma sheria, wahalifu ndo tunao wa kumwaga, angalia watu wanasota sello kisa hakuna hakim wa kusikiliza kesi zao, ina maana hiyo taalum yako ni deal!!
    Soma sheria mdogo wangu, mie sina elim ila nikapata muda wa kuwa mwanafunzi, nasoma law tuu!!, wana pesa hao balaa, hakuna firm ya law iliyo masikini, angalia akina chenge, masha, mkono, byabusha n.k, shauri yako ukisoma hiyo social!

    ReplyDelete
  6. sociology ni somo mama katika masomo yote. hili somo ni la haki pasipo na lawamama sheria inakula upande moja safi mwingine malalamiko. Sociology linahitajika pande zote hata wahandisi hawawezi kuanzisha au kuendeleza mradi au kuendesha mradi bila masociologist kwenye sector ya afya ndiyo muhimu zaidi. Usidharau umesoma wapi. Hata kama dodoma wewe zingatia masomo, ongeza wigo wako katika kujifunza kimataifa Utakuwa na future mzuri

    ReplyDelete
  7. mbona jawabu ni rahisi sana.sheria huwezi kuifananisha na socology hata siku moja. nenda kasome shaeria. mimi ni mwanasheria na nilisomea hapo hapo mzumbe. sheria inalipa sana dada ila pale mzumbe kuna wakorofi wawili itabidi upige msuli sana maana hao jamaa ni roho za korosho sana. wa kwanza ni binamungu na wa pili ni benjamin. sasa itabidi shule iwe kali sana maana hawa jamaa wanapenda kufelisha wanafunzi. lakini ukijitahidi utafanikiwa. ni mimi emma a.k.a OSAMA

    ReplyDelete
  8. Dada 'Sofi'kapige laws acha kubabaika, soko lake siyo baya kama ulivyoambiwa hapo juu.Kama utaweza specialise kwenye Industrial laws!!

    ReplyDelete
  9. Hivi vitu dada yangu inategemea na interest ya mtu sana.Na si sahihi mtu kufikiria kuwa siciology haina ajira,la hasha kw namna tunavyokwenda inahitajika sana hasa kwa wakati huu ambapo serikali inapunguza mzigo wake kwa sekta binafsi.

    Unaweza kupata ajira ktk sekta binafsi, serikalini na sehemu nyingine.Ila ni ukweli usiofichika kuwa Sheria inaonekana kuwa superior ukilinganisha na sociology ingawa wako wanasheria wamemaliza na bado wanasaka ajira pia.

    Angalia na uwezo wako pia, na talent zako.Je wewe ulikuwa unataka kuwa nani baadaye au unataka kuwasaidia Watanzania ktk nyanja gani?

    Nikupe mfano mmoja, kuna jamaa mmoja akasema ni vigumu sana kwa mtu wa sociologia kufungua firm yake wakati mtu wa sheria anaweza.Mimi nikawa na mpa mfano wa Marehemu Munga Tehnani.Ni mtu ambaye alijiajiri na akawa anafanya kazi inayomuingizia kipato.

    Hivyo basi mwenyewe ndiye utakaye weza pata jibu.Wengi wanapenda sheria na sahii na wanavigezo kama wengine wameeleza kuwa hapo baadaye Dunia inahitaji wanasheria lakini kwangu mimi si sahihi naamini hapo baadaye tunahitaji kuwa na Watu wa maendeleo ya jamii zaidi.

    Sociologia utakupa mafanikio ata kama unataka kuajiliwa na international organization lakini ni mara chache sana mtu wa sheria ikawa hivyo.Katika haya masuala ya mambo mtambuka hauwezi kukosa watu wa sociologia na sasa hivi wameongezewa upana wa ajira hasa ktk mazingira haya ya kuongezeka kwa magonjwa kama UKIMWI na mengineyo.

    Kazi kwako dada yangu mimi nimekupa upande mwine wa shillingi ambao wachangiaji hapo juu hawakuueleza.

    ReplyDelete
  10. SHERI, dada SHERIA, hata usipokuwa Lawyer wa kwenda Mahakamani kama unaogopa Mambo mengine(...), Usijali, kuna kazi nyingi unaweza kufanya zinazohusiana na Law, ndani na nje ya nchi. LAW, itakuaidia zaidi.Kuuliza si ujinga na Hongera.

    ReplyDelete
  11. we mtoto acha ushamba sheria haina dili bongo labda kama utaenda nje ya bongo. nenda kasome sociology dili za kumwaga bongo now and then.

    ReplyDelete
  12. Law all the way

    ReplyDelete
  13. Kutoka Sheria unaweza kufanya kazi ktk maeneo mengi, tofauti na ilivyo sociology ambayo imebanwa. Sheria ni ngumu ila matunda yake ni matamu. So mdogo wangu kupoteza wakati acha ambaa zako mbeya kwa Sheria ya Mzumbe. Nakutakia Masomo mema.
    Rny - Ist.

    ReplyDelete
  14. Mijitu yote iliyochangia hii mada naona bado ina ukungu kwenye bongo zao. Yaani wote wamegusia kuajiriwa baada ya masomo. Hivi hamuwezi kufikiria kuhusu kujiajiri wenyewe mpaka muajiriwe? Mkidai hamna pesa za mtaji kwa sasa yapo mashirika kibao yanayotoa mikopo kwa masharti nafuu. Jamani watanzania tujijengee utamaduni wa kujitengenezea mazingira kuliko kusubiri kutengenezewa na kwenda kujiegesha tu.

    Hivi wewe Sophia unaonaje ukaenda kusomea Sociology and then ukaja na idea yako ya kuanzisha NGO itakayokuwa inadili na maswala ya kijamii?

    Nina hakika kuwa hili suala halishindikani na pia utajijengea uzoefu pamoja na heshima kubwa zaidi kwa jamii kuliko hiyo sheria ambayo baadaye utakuja jijengea maadui kibao au hata kuuwawa pale utakapokuwa kinyume na matakwa ya watu.

    All the Best in Your Choice.

    ReplyDelete
  15. Hello Sophie,
    Swali lako ni la msingi sana katika hii jamii yetu na blog ya jamii pia. sio pekee ndie umepatwa na tatizo kama hilo but ni wengi sana. Kimsingi nadhani naweza kusema kwamba watanzania wengi huwa tunasoma kufaulu na sio malengo. Kwanini mtu mpaka unachagua hizo kozi usiwe na priorities? wengi ukiwauliza hata hapo wanasoma PHD hawakuambii why wamespecialise kwenye hicho kitu. Nakumbuka niligombana na wengi pale nilipokataa goverment sponsorship ya kusoma BSC science general Mlimani na kuenda IFM kusoma field ingine as a Private student. Pia nilipokataa kwenda MSC Kule belgium kwa full sponsorship nakuja huku UK on my own initiatives.

    Please know what you want to achieve and be honest to yourself. unaweza kujiajiri kama lawyer pia kama social weorker kama utakuwa well equiped na creative. Hakuna formula najuwa watu kadhaa wamekushauri sheria but please mimi naamini sheria sio tu kupass exams ni pamoja na kuwa logical thinker. so kama unaweza go sheria but with reason.. wengine wanasema sheria ngumu saaana but usijali kila somo ni gumu.

    kwakuwa sikujui uwezo wako sana naweza kukusukumia kwenye Sheria kwani ni rahisi kudefine future na kama walivyosema wengi, nchi yetu wanasheria wakike wachache na future inahold kuwa na wanasheria.. but uamue mapema unataka kuspecialize kwenye sheria ipi? Criminal law, Businness law, Familly law, nk. sio baadae uje uulize tena je ipi inalipa!!

    All the best,
    G7
    UK

    ReplyDelete
  16. fanya kitu unachopenda maana ukumbuke ndo itakuwa ajira yako mpaka kifo. Sheria iko more prestigious...na sababu ni kutokana na wachache walio mashuhuri. Lakini sociology is wider...na utaweza kufanya kazi katika field nyingi. Fanya research kwanza...ongea na watu katika hizo field mbili uone ni ipi hasa utapenda kuichangia. Uone wanafanya kazi gani hasa na kama wewe ungependa kufanya kazi hizo. Ningekushauri ufanye research hasa...maana ndo life lako hilo!...kuuliza kwenye blog haisaidii sana...

    ReplyDelete
  17. Do what is best for you. Mimi sikubaliani na wanaotoa vigezo vya kwamba kitu fulani kinalipa zaidi ya kingine. Wanaosema kwamba sheria is the best wanafikiri kwamba everybody can be a good lawyer or advocate. Sheria kwa mtazamo wangu wanaokuwa successfull ni wale wenye vipaji sio waliosoma ili mradi wamalize shule. Pia kwa upande sociology naweza sema kwamba ipo saturated sana kuna intake kubwa sana. sasa wakimwagika mtaani sijui kazi wanapata wapi. Mi ushauri wangu nisingependa kuegemea upande wowote. By now lazima uanze kujua malengo yako kimaisha sio kubahatisha. Do what ur insticts tells u to do. Nao mnaompa ushauri ingekuwa vizuri ukatoa data ni nafasi gani za kazi zipo na unaweza kuorodhesha kwamba nikisoma sheria nitakuwa nani? N vipi mishahara inakuwaje? Nafasi ya kjiajiri ipoje?

    ReplyDelete
  18. wewe tafuta bwana uolewe ndicho kilichobaki,shule hazina mpango wowote ule. wewe kama umemaliza masomo ya awali basi inakutosha kwani umesha kuwa na uwezo wa kujui lipi baya na jema huko kutaka kuendelea na masomo ya chuo kikuu ni kuharibu akili yako tu kwani hakuna lolote la maana unaweza kujifunza huko, mambo ya kufundishwa vitu ambavyo vingine hutakaa uvione maishani mwako, kufundishwa mambo ambayo hata hayapo kwenye ukweli wa maisha,kama mafomula ya mahesabu,makanuni mbalimbali na pia kukariri kwiiingi nk.najua utaona kama nakuyeyusha lakini ni ukweli kinachotakiwa wewe ni kujiamini tu kwani hiki ndicho kitu ambacho watu wengi ambao hawakuendelea na masomo ya kuaribu akili wanakikosa,kujua kiingereza sio lazima uwe umeenda shule kwani kuna watu hiyo ni lugha yao na hawajui hata jinsi ya kuishika kalamu.

    Mbega mweupe

    ReplyDelete
  19. SOCIALOGY NI POA SANA HASA KWA NINYI KINA DADA UNAJUA SISI WANAUME WA KIBONGO HATUPENDI WATU WALIO SOMEA SHERIA WANAKUWA WAKALI SANA SASA UKIMALIZA SOCIALOGY UTAKUWA VERY SOCIAL KIAINA VILE.HATA TIGO ITAKUWA HAISUMBUI SASA DADA YANGU ACHANA NA MZUMBE WEWE NENDA KALE SOCIAL TU HIYO NDIYO MARKET SANA KWA KINA DADA, NEXT TIME WEKA EMAIL ADDRESS KAMA UNATAKA KUPEWA USHAURI SASA WATU WATAKULAJE TIGO KAMA EMAIL UMEBANA? SIUNAJUA UZURI WA NYUMBA CHOO? ASANTE KAKA MICHUZI MZEE WA TIGO KWA KUNIRUHUSU NIWEKE MAWAZO YANGO HUU...!

    ReplyDelete
  20. mimi nadhani fanya unachoweza. Pamoja na ukweli wa kubabatiza kuhusu nini utakifanya baada ya kukamilkisha digrii yako, fanya kile unachopenda. bado nadhani ukiwa unapenda sociology unaweza kupata kitu bora zaidi. Watu wasikudanganye kwamba sociology ni kwa ustawi wa jamii, la hasha unaweza kubamba hiyo halafu ukatafuta kitu kinachoambatana nacho na kama unadhani wewe ni mkaliw a sheria na una kipaji go for it la maana sana ni kuwa do what you can do na tyena something you can do best huku unajisikia raha.

    ReplyDelete
  21. KUMBE WASOMI WAPO HAPA ALAFU WATU WANAONGEAGA PUMBA TU AMINIA NAONA SASA TUNAVUTA HATUA NZURI SANA NA NI VIZURI JAMANI TUWEZE KUSAIDIANA KWA KILA JAMBO NAONA KUMBE WAOSHA VINYWA HAWAPO KUMBE NDIO WALE AMBAO HAMNA KITU EMPTY.....

    ReplyDelete
  22. SOMA UNACHOWEZA. CHA MUHIMU NI KUPATA DEGREE. KUNA WENGI WAMEENDA KUSOMA WANACHOPENDA KUMBE HAWAKIWEZI WAKADISCO.

    WATU WENGI HUENDA SHERIA KWA SABABU INA SOKO. HATA KUPATA NAFASI UDSM LAZIMA UWE NA DIV 1 NZURI HASA <7PTS. JAPO UNWEZA KUPATA NAFASI KATIKA VYUO VINGINE KILAINI KWANI HAVINA USHINDANI NA UDSM.

    CHA MSINGI ANGALIA UZITO WA CHUO NA UZITO WA KICHWA CHAKO, KWANI UNA DIV NGAPI?

    ReplyDelete
  23. Sophie umeuliza swali la msingi lakini hujatoa maelezo ya kutosha kuwezesha mtu kukushauri vema.
    Ushauri naokupa unafananafanana kidogo na wa G7.
    Kwanza, unaweza kuwa na mafanikio bila kusoma chochote au kwa kusomea chochote. La maana ni kuwa uhakikishe kuwa chochote unachokifanya unakifanya kwa namna ambayo kila mtu atasimulia jinsi ulivyo hodari kwa hilo.
    Pili ni kuwa jibu la usome nini unalo wewe. Kukusaidia kulifikia jibu hilo nikuulize swali: kwa mfano ungekuwa na hela za kukutosha kupata mahitaji yako ya muhimu bila kulazimika kufanya kazi na ukawa na uhakika wa kuendesha maisha yako hata kustaafu leo hii, ungetumia muda wako kufanya kitu gani? Jibu lako litakuelekeza fani unayopaswa kusomea.
    Nakutakia kila la heri na uchaguzi wa mwelekeo. Ufikapo chuo kumbuka kukaza msuli na kuzingatia masomo.

    ReplyDelete
  24. sikiliza dada yangu mimi nakushauri ukasomea sheria kwani hata hiyo sheria unaweza ukaanzisha NGO yako. Wnasheria wangapi wamejiajiri wenyewe na pia wameweza kuanzisha NGo zao.
    Amka dada.

    ReplyDelete
  25. mi niko along the same lines kama G7, kakupa ushauri mzuri sana. Kwanza usisome kufuata mkubmo; too bad watanzania wengi ndio tunavyochagua course, tunaangalia "what is hot now". Pili kuhusu suala la ajira; you will cross that bridge when you get there; and trust me, unaweza kuajiriwa no matter what degree you do, inategemea na upana wa mawazo yako na hangaikaji. Na pia kama baadhi ya wadau walivyogusia hapo juu; kuna suala la kujiajiri pia.

    A degree haikufundishi tu kutoka chuo na kwenda kufanya kazi; it gives you a lot more than that; ability to reason, think critically and be innovative. So the most important thing changua unachokipenda na utakachokimudugu. Kitu ukikipenda utafanikiwa tu. Na kumbuka kama mdau mmoja aliposema juu hapo, this is a career you are building; you will be doing this for the rest of your life. So ukichagua course fulani kwakuwa tu ni 'deal', unaweza kuajiriwa ukatengeneza hela nzuri but get bored to death in just a couple of years.

    All the best!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...