Brother Michuzi,
samahani kwa kukusumbuwa kidogo, nilikutumia email kitambo lakini sikuiona katika blog yetu ya jamii, kwa hivyo natuma tena. Naomba uniwekee suali langu hili kwenye blog yako ili ndugu zangu waweze kunisaidia na kunipa mawazo.
Suala langu ni kuwa nataka kununua gari ya aina ya landrover, natafuta kampuni, wakala au mtu binafsi nyumbani anae jishuhuisha na uigizaji na uuzaji wa magari haya.
naona contact zao iwe email, website, number ya simu au mahali walipo ili niweze kuwasiliana nao.
Tafadhali brother michuzi, usitupe ujumbe huu ndani ya gunia.
Shukrani kwa wote
Tafadhali brother michuzi, usitupe ujumbe huu ndani ya gunia.
Shukrani kwa wote
Mdau Zenj
Muagizaji na Msambazaji wa Land Rover ni Cooper Motors Tanzania Limited au CMC wako karibu na Maktaba Kuu ya Taifa oposite na ilipokuwa ofisi za Michuzi zamani (Daily News na Print Park) Mtaa wa Maktaba kama sikosei.
ReplyDeleteNenda kwa Leodgar Tenga.Ni mtu mwenye nafasi pale Landrover Tanzania Limited.Atakusaidia.
ReplyDeletewewe mchawi ombi lako liliwekwa kwenye hii blog siku za nyuma na ukapewa ushauri uache kununua magari ya kizamani,kwani tunakumbuka ulikuwa unatafuta landrover ya kizamani.kwani kama ulikuwa unatafuta mpya sijui umetafuta wapi kwani hata mtoto anajua ziko wapi. wewe kwanza uko zenji sasa sijui landrover ya nini wakati kandambili zinakutosha.tuondolee wanga hapa
ReplyDeleteWewe mzenji ina maana hata yellow pages uijui? ni vyema uendelee kutumia usafiri wa punda kama mnavyotumia huko mchamba wima na kaburi kikombe.
ReplyDelete