Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akizindua jiwe la ufunguzi wa Msikiti wa Masjid Maftah, uliojengwa kwa juhudi za Inspekta Jenerali Mstaafu wa Polisi ,Omari Idi Mahita, chini ya ufadhili wa wahisani wa ndani na nje ya nchi katika halfa iliyofanyika Agosti 15, mwaka huu Mjini Morogoro.
Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, katikati, akifurahia jambo wakati wa mazungumzo na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini , Omari Mahita, kulia pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu , kushoto wakati wakimbaribisha katika halfa ya kufungua msikiti wa Masjid Maftah, uliojengwa kwa juhudi za Mahita, Agosti 15, mwaka huu Mjini hapa.
Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, watatu kutoka kulia akiomba dua kabla ya ufunguzi wa msikiti wa Masjid Maftah, katika halfa iliyofanyika Agosti 15, mjini Morogoro. Wa pili kulia ni Inspekta Jenerali wa Polisi Mstaafu, Omar Mahita. picha zote na habari na mdau John Nditi

mbona picha hatuoni
ReplyDelete