Heshima yanko Mh. Nanihii wa Tegeta.,
Kwanza pole na kazi. Nimekutana na habari hii toka gazeti la The EastAfrican
/2558/456998/-/s32iumz/-/index.html

Habari yenyewe inahusu wafanyabiashara katika sekta binafsi Uganda kuiomba serikali yao iwalinde kutoka kwa upinzani kutoka kwa wafanyabiashara toka nchi nyingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mfano mmojawapo waliotoa ni kuwa sekta ya ujenzi Uganda bado ni changa na wanahofia wakandarasi waliobobea toka Kenya kuja Uganda na kuchukua biashara yao yote. Hata hivyo, serikali ya Uganda ilikataa ombi hilo toka kwa sekta binafsi.

Sasa naomba uwasilishe swali/hoka kwa wadau, hususan Bw. Kakuru toka Uganda. Kumbe na Waganda nao wanaogopa Jumuiya, hususana Wakenya, ingawa wanajidai kutushutumu Wabongo kuwa ndio tunaogopa?
-- ----------------------------------------------------------------------------------
Peter S. Nalitolela,
AMINSS Graduate Program,
Trent University,
Peterborough,
Ontario,
Canada K9J7B8

PHONE: +1-705-748 1011 EXT 6453
CELL: +1-705-313 0014
FAX: +1-705-748 1652 ATTN: Peter
web:
http://www.people.trentu.ca/peternalitolela/

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Wakenya wenyewe 8Kenya manufactures) wamekataa East Africa label eti kwa madai ya kwamba ni gharama kupata leseni wakati TZ na UG wamekata hiyo leseni kisa wanaona makampuni yao yata-loose in regional market kwa vile ni machache yamejiandikisha huku kote ni ku-protect market kwa vile policy inasema ni bidhaa zenye hiyo label tuu ndo zitauzika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...