Tanzania ni nchi iliyobahatika kuwa na rasilimali ya wanayama wa pori ,ambao wanaishi kwenye mazingira yao wenyewe,kwa kimombo natural habitat.Sasa kinachosikitisha ni kwamba hao wananyama wanashambuliwa na maadui wengi nao ni :--
Wanyama wenyewe kwa wenyewe[predation]
- Ujenzi wa hoteli nyingi na kubwa kwenye mji wa wanyama pori[ National parks]
-Uwindaji wa kisasa [professional hunting] au kuua wanyama kwa mchezo[kill for fun]
-Badiliko la Hali ya hewa na ongezeko la joto duniaani[Climate Change and Global wa Warming].
Kweli Tanzania tunaelekea wapi?.Tunajua tuna wanayama wanagapi wa pori?.unajua kama wanayama uonekana wengi sehemu fulani na msimu fulani ni kutokana na kufuata chakula na maji?.
Tanzania ilikuwapo moja ya nchi yenye faru wengi hapa duniani.Sasa kwa nini hawapo tena mpaka tunaletewa mbegu kutoka south africa.
Naomba wachumi wenye uchungu wa nchi wasaidie kuelekeza na kufafanua kuhusu lipo bora kati ya kuwinda,kuuza ,kuua kwa mchezo na watalii waje na kuona wanayama na kuacha pesa zao hapa na kurudi kwao.
Kutokana na Balaa hili la ongezeko la joto na badiliko la hali ya hewa,uchumi wa nchi unategemewa kuadhirika kwa kiasi kikubwa sana kwani wanyama wengi hawataweza kubadilika au kuzoea hali ya hewa mpya[global warming].
Kuna dalili kuwa kuna wanyama wataweza kuhimili au wengine watakufa , au kukimbilia NORTH POLE AU SOUTH POLE.[Hali ya baridi kidogo].
Mbuga zetu zinategemewa kubadilika na kuwa miji mikubwa ,hii ni kutokana na ujenzi wa mahoteli ya kitalii husiokuwa wa busara ndani ya mbuga zetu.Sio muda mrefu tutakuwa na mji mkubwa unaoitwa serengeti na hatujui wanayama watakuwa wamekwenda wapi?.au kufa au kuikimbilia nchi jirani.
Tuiache na kuiboresha rasimali hii kama tulivyoiridhi kutoka kwa wazee wetu wenye busara waliopita.
ASANTENI MUNGU
IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
The Institute Of Research And Environmental Quality[Ireq]
P.BOX 80259
DAR ES SALAAM
TANZANIA
[EAST AFRICA]
Tell 011 255 755 901002
Jamaa aliyeandika ana supposed kuwa mtaalamù ????Wanyama watakimbilia North Pole na South Pole kwa sababu kuna baridi kidogo!!!!!!!!I rest my case.Huyu mtaalamu anaijua North Pole kweli????
ReplyDeletehabari mzee,mm niliyekutumia email pls naomba tuwasiliane na ile namba yangu au email.thanks.ally
ReplyDeletewawekezaji wa na watalii hawana mapenzi na mtanzania bali wanamapenzi na rasilimali zetu tu. Watanzania wanatakiwa kufikilia kitu kimoja. Kitu tulichokuwa nacho cha kujivunia duniani ni (limited) rasilimali. Kwasasa, rasilimali nyingi tumeuza kwa watu wanje ambayo ni hatari kubwa. Rasilimali zikiisha hawa watu wanapanda ngede kwenda kwao wanapoweka mapesa wanayo tengeneza katika rasilimali zetu (capital flight), sisi tutaachwa hatuna rasilimali yeyote na masikini milele. Nchi yetu penda usipende ni katika nchi masikini sana duniani. tulitaakiwa kutumia hizi rasilimali kwa manufaa ya kujitoa katikaa umasikini wetu. kila mikataba au Foreign direct investment ilitakiwa iwe katika advantage ya mtanzania lakini kwa ssa inawanufaaisha wawekezaji, kukuza uchumi wa nchi zao na of course mafisadi wanao negotiate contracts. watanzania bado tukonyuma sana. Uongozi tuliokuwa nao ni mbaya sana. Mababu zetu, waliingia mikataba na wakolini wasioelewa na kutawaliwa, sasa Raisi wetu ndio wakwanza kwenda nje kuomba wageni waje kututawala kiuchumi. Ni bola kuwa na mtawala mmjoa kuliko kuwa na watawala 30 kwa sababu vizazi vijavyo vikitakata kujitawala kichumi ni vigumu kushindana na watawala wengi.
ReplyDeleteNchi imeshauzwa, bado mnatawaliwa na wafadhili, demokrasia haijaleta maendeleo bali ufisadi, ubinafsishaji wa makampuni ya serikali unanufaaisha nchi za nje, poleni sana watanzania mnaoota kupata maendeleo, mko kwenye mtego, mimi tu ndio naweza kuitoa Tanzania kwenye mtego huo.
Wewe anony wa 13,2008,11:54 wa kwanza,Umekwenda shule?.Husianzishe mjadala alafu ukakimbia.Hii ni oja muhimu kwa ajili ya nchi.kwanza unatakiwa uingie kwenye website hiyo hapo chini,alafu uje ujibu au utoe maoni.Husiingie kwenye ujumbe huu,hapa hapakufai[kichwa chako cha panzi].Nenda kwa mwalimu wako aliyekufundisha geograph,au ukamuulize mdogo wako au mtoto wako wa darasa la tano kuhusu south pole and north pole.Alafu uje kwenye mada hii.
ReplyDeleteAsante Sana mtoa Mada hii.Kwa Kweli Hii tunaweza kusema ni "WILDLIFE GENOCIDE".Kwa kweli jamaa kaelezea vizuri sana.Nchi yetu ni Tajiri kwa kweli.Tunaona matangazo kwenye Tv huku Nje ,yakielezea Serengeti,Ngorongoro na mbuga zingine.Hivi kweli uchumi wa nchi yetu inategemea depletion of resources[wildlife] in order to boost up our economy?.Hii inaingia akilini kweli.Mfano kama mtoa mada alivyosema tulikuwa na Faru wengi,kila mtu anajua.Sasa Tumesaidiwa faru watatu.Je watu wa Tanapa wanatuambia nini?na Bunge letu linalotunga sheria nalo alitazami swala hili?.Kwa mtindo huo Tanzania itaingia kwenye matatizo mengi ,1.USALAMA WA NCHI UTAKUWA MDOGO SANA.KWANI WALE WATU WALIOKUWA WANATEGEMEA KUPATA RIZIKI ZAO KUTOKA KWENYE UTALII WATAKUWA HAWANA KAZI.WIZI,UJAMBAZI UTAONGEZEKA.NA IDADI YA HAO NI KUBWA KULIKO HAWA WENYE MAKAMPUNI YA UWINDAJI.2.ENVIRONMENTAL REFUGEES,TANZANIA HAPO MBELE ITAKUWA KAMA ETHIOPIA NA SOMALIA ,AMBAZO HAKUNA RESOURCES NA HATIMAYE KUSABABISHA WAKIMBIZI WA KIMAZINGIRA.WAKIHAHA KUTAFUTA RIZIKI NCHI ZA JIRANI ,AMA KWENYE KWA HAO WAZUNGU.
ReplyDeleteMAANA YA KWENDA SHULE KWA HAKI NIKUELIMISHA WALIOIKOSA HII BAHATI KWA MOYO WOTE.KAMA WEWE NI FORM FOUR MUELIMISHE DARASA LA SABA HATA KWA MHUTASARI ILI YEYE AJIVUNIE ELIMU YAKO KWAMBA IMEMSAIDIA. IKIWA ELIMU ULIYOIPATA UNAITUMIA KUMNYANYASA KWAMBA YEYE HAJASOMA NA HAWEZI KUCHANGUIA CHOCHOTE ZAMBI YAKO NI KUBWA SAWA NA DHAMBI YA ASILI. KWANZA UNAFURAHIA KUTOKUSOMA KWAKE PILI WEWE NI HASARA KWAKE NA KWA TAIFA KWA UJUMLA. KWA KWELI WATOA MAONI WAMEONYESHA UCHUNGU NA NCHI YAO, WASOMA MADA WAMETIWA UCHUNGU NA NCHI YAO. HUU NI WAKATI WA KUAMKA KILA MTU ANAJUKUMULA KUJENGA NCHI KATIKA KAYA YAKE. USINGOJEE UWE RAIS AU MBUNGE. TENDA WEMA NENDA ZAKO MUUMBA ATAKUPIGA MUHURI USIHOFU. BAAHATI IKIJA BILA WEMA BASI HUJUE INAKUHADAA ITAPOTEA MARA MOJA. BAHATI INAKUJA KWA KUWEKEZA WEMA (EMOTIONAL BANK ACCOUNT)
ReplyDeleteAliyeanzisha hii mada ana uchungu na maendeleo ya nchi yake japo hajabahatika kuwa na vyanzo vizuri vya kuweza kumjibu maswali yanayomsumbua. Hili ameliweka bayana alipoomba wachumi wenye machungu na nchi wamwelekeze lipi bora, kupata hela kwa kuua wanyama kwa kujifurahisha au kupata fedha kwa njia ya kuwaona wanyama hao katika mazingira yao ya asili wakiwa hawabughudhiwi.
ReplyDeleteKwa mwenendo wa nchi yetu, ana sababu kuwa na wasiwasi wa kuanza kujengwa maghorofa Serengeti. Kuna sera bubu ya ufisadi inaendelea na wadau wameanza kuwa na wasiwasi.
Suala la mabadiliko ya hali ya hewa na ongezeko la joto duniani bado ni sayansi yenye midahalo ya kitaalamu ikiendelea. Jambo la busara ni kujiandaa kwa madhara yatokanayo na mabadiliko haya. Jambo la kukatisha tamaa ni kuwa mataifa yaliyosababisha janga hili bado yanaendelea na bidii ya kuliendeleza kwa njia mbalimbali kama vile kutengeneza magari yenye injini kubwa zinazotumia mafuta kupita kiasi na kututupia magari yao madogo yasiyo na ufanisi. Tunaweza kutoa mchango kupambana na tatizo hili kwa kuvumbua teknolojia zinazofanana na matatizo yanayotukabili badala ya kuagiza nje, tusiishie kulalamika tu.