MNENGUAJI maarufu wa Bendi ya FM Academia, Rukia Bruno (pichani) amefariki leo mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam .

Balozi Credo aliyejitambulisha kama kaka wa Mwanamuziki Nyoshi el Saadat ambaye mkewe amefariki, amsema shemeji yake alikuwa Muhimbili ambako alilazwa kabla ya kujifungua mtoto aliyefariki wiki moja iliyopita na kuzikwa hospitalini hapo.

"Habari za msiba za Bruno ni kweli na upo Sinza nyumbani kwa Nyoshi ambako familia ya marehemu ipo katika kikao cha kupanga siku ya maziko ya marehemu yatakayofanyika siku yoyote kuanzia sasa," alisema Credo.

Aidha, Bruno alisema hafahamu chanzo umauti wa Rukia ambaye ameacha mume na mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Stallone.

Kabla ya kuwa bendi ya FM Academia mnenguaji huyo alikuwa katika bendi ya Twanga Pepeta, Bendi ya Tamutamu ambazo alijipatia umaarufu mkubwa kutokana na uwezo wake wa kuwapa burudani mashabiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. pole sana nyoshi Mungu ndiye muweza wa yote Mungu akutangulie katika kipindi hiki kingumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...