Aise kaka michuzi,
Pole sana kwa kwikwi ya globu yetu ya jamii. nafurahi kusikia umesharekebisha mambo na libeneke kama kawa. ah, ndio mambo ya mtandao hayo. wala usikonde.
mie leo nimependa hii naomba wawekee na wadau wenzangu wasome.
SIRI YA MPENZI ASIYE MWAMINIFU

HANA RATIBA MAALUM
Ikiwa mlianza vizuri na mpenzi wako, huku akiwa hana mambo mengi sana, sasa ataanza kuwa na ubize usiojulikana. Hana ratiba maalum ya kuzima simu yake. Unaweza ukampigia simu asipokee kwa wakati, aidha ukimwandikia sms hajibu!

Hii inaweza kuwa sababu ya awali kabisa kukufanya uanze kufikiria kwamba mpenzi wako anakusaliti. Katika hili huhitaji kufikiria sana, unaweza kulinganisha na mwanzo wa uhusiano wenu, ni kweli alikuwa na ubize kiasi hiki? Kwanini anazima simu kila wakati?

Wakati mwingine inawezekana amebadilisha namba ya simu kwa ajili ya kukukwepa, hii ni alama ya kwanza kabisa ambayo kama mpenzi wako akiwa nayo, anza kufanya uchunguzi wa kina juu ya mienendo yake.

HAYUPO HURU KUZUNGUMZA NA WEWE
Hii haitofautiani sana na hilo hapo juu, lakini hapa akipokea simu yako, huwa na kigugumizi! Inawezekana kabisa ukawa umempigia kwa muda mrefu na hajapokea lakini atakapopokea hawi huru sana. Ni kama yupo na mtu anayemuogopa!
Hebu soma mfano wa mazungumzo kati ya mpenzi mwaminifu na yule asiye mwaminifu.

“Hallow sweetie, vipi mbona ulikuwa hupokei simu?”
“...Hakuna, unajua...ah...”
“Lakini mpenzi wangu umebadilika sana siku hizi.”

“Mh! Wasiwasi wako tu, mi nipo sawa...hallow...hallow, sikusikii vizuri, una katikakatika...” mara anakukatia simu.
Kwa mtindo huu ni wazi kabisa kwamba mpenzi wako atakuwa na mtu na anahofia kuharibu, hivyo atakata simu.

ANAZIDISHA UMAKINI NA SIMU YAKE
Hili pia ni tatizo lingine, jaribu kuchunguza umakini wake kwa simu yake. Mara nyingi anapenda kuishika simu yake mkononi, siyo ajabu hata akienda msalani akaenda nayo!
Tabia hii hakuwa nayo awali, lakini amekubadilikia ghafla. Hataki ushike simu yake, wakati mwingine anaweza kuweka password (namba za siri) kwenye phone book na messages! Ukiona alama hii ujue unaibiwa!

ANAKUTAFUTIA VISINGIZIO
Hapa ataanza kutafuta kila njia ili mgombane, ukimkosea kidogo tu, anakasirika na inaweza kuwa sababu ya kukataa kupokea simu yako.
Anafanya yote hayo kwakuwa tayari ameshapata mwingine. Hata kama ni kweli mna tofauti na ukaamua kumuandikia sms ili muweke mambo sawa, hatakujibu na badala yake ataifanya hiyo kuwa tiketi ya kuendelea kugombana na wewe. Hapo atakuwa na nafasi ya kufanya atakavyo na patina wake mpya.

...HUENDA AMEPATA MWINGINE
Kwa vipengele hivyo hapo juu, hapana shaka atakuwa anakufanyia hayo yote kwasababu tayari ameshapata mwingine, lengo ni kupata nafasi na uhuru wa kuwa na huyo mwingine.
Jambo hili siyo la kukurupuka katika maamuzi, fanya uchunguzi taratibu na mwisho wa siku utagundua ukweli.

...NG’AMUA...AMUA...!
Baada ya kufanya uchunguzi wako na kubaini kwamba ni kweli mpenzi wako hana uaminifu, huna sababu ya kuendelea kuwa na mtu ambaye anahatarisha maisha yako.

Tumia akili yako ipasavyo, achana na kuongozwa na hisia, hata kama unampenda kwa kiasi gani, mwenzi wako akikosa uaminifu ni sumu kali katika uhusiano. Hapo sasa ndipo unapohitajika kufanya maamuzi sahihi.
Sema na moyo wako kisha amua cha kufanya.
Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. HAYO MAELEZO YANAONESHA MPENZI MWANAMKE NDO ANASALITI...USHAURI KWA WADAU, UKIONA DALILI HIZO NA UKIJARIBU KUREKEBISHA INAKUWA ISSUE...MPIGE CHINI, ATAKUPOTEZEA MUDA....MADEM NI URITHI WETU NA YOTE YANAWEZEKANA PEKUPEKU NA HATA KWA VIATU...UKIMEGEWA DEMU WAKO NAWE MTAFUTE MNYONGE UMMEGEE HAIPUNGUZI MAUMIVU ILA INAZIDISHA HADHI YA KIUME...KUMEGEWA NI JAMBO KUKIMBIWA UMEISHAFIKIRIA??????

    ReplyDelete
  2. Michu, kama hili ni wazo lako, nakuunga mkono, mguu, kichwa na hata vidole... I have been there and I have seen that. Ask me and I will tell you what. I am a woman, lakini nadhani hii tabia inatokea kwa binaadamu wote, kwa maana ya kwamba sisemi kuwa ni wanaume pekee wanaweza kuwa na tabia hii. Lakini jamani hivi inakuwaje hamuoni kuwa dunia imekwenda harijojo (chuckle). Why cheat is she/he not good enough now? Why don't we love people we sleep or even have babies with? Au huwa tunawafuata kwa matamanio tu? oh jamaniiii. Ni kweli haya mambo sio mazuri, kama ulimpenda mwanzo ukamwita baby, sweet potato pie and all those eatable sugar candies... make sure you mean everything from the start. Kama ikitokea kutokuelewana, wote ni binadamu jaribuni kukaa na kurekebishana, ikishindikana..... chukua time ndio ufikirie kuanza na mwingine sio kuchanganya nge wawili jamani... maisha mafupi.

    ReplyDelete
  3. Hee bwana ndiyo,nimekubali mtu wangu...!!! Haya yamenikuta...!!!.Typical situation..!!!
    Mdau,
    USA.

    ReplyDelete
  4. Asante sana Mdau, maana mpenzi wangu yuko hivyo kwa hiyo, ni wazi ana mpenzi mwengine kama ulivyo shauri akili kichwani mwangu.

    ReplyDelete
  5. Kwa Mume na Mke Sawa. inatatanisha ILA Kama Mtu Si Mke Wala Si Mume ni Wapendanao hamjaowana shauri zenu kila mtu chake kila mtu si wamwenyewe, boyfriend na girlfriend bwana anaweza kuwa na yoyote na akichukuliwa na mtu usilalamike sababu hamjaoana cha watu mie najuwa ni mke au mume basi fullstop mengine mtajijuwa ambao si wa halali mungu anapenda wa halali. uwe mkristo au muisilamu topic zenu pelekeni magazeti ya umbeya sio hapa. Ally Mapesa.

    ReplyDelete
  6. we mtu mbona hatari hivo,hujazungumzia hata hao wapenzi wakae wajadili kidogo future yao we unashauri kuachana tu.halaf mnalalamika sikuiz ndoa hazidumu.We minakuita muaribifu wa jamii wala sifati ushauri wako mbovu ng'o!!

    ReplyDelete
  7. kama mtu una hakili zako timamu sidhani unaweza kuandika upuuzi huo { ally mapesa } fikilia AIDS, wanawake wanafahamika , angalia siku moja utalisha meza moja na mume mwezako, halafu uje kutoa comments zako hapa

    ReplyDelete
  8. Ni kweli hii ipo na ni noma michuzi,mimi na mke wangu tulishakubaliana hakuna mmoja wetu kugusa simu ya mkonononi ya mwenzie hata kama inaita teeeh teeeeh teeeh.Mdau uliyetoa maoni nadhani yamekukuta,pole.
    Hii tuache kujiumauma 90% ya wanaume hatupendi wake/wapenzi/wachumba wetu kugusa simu zetu za mikononi.Sababu?...'Nature'

    ReplyDelete
  9. ALLY MAPESA vipi mkuu umeamka hujapika mswaki unakuja kulopoka vipi mkuu tulia inaonekana hayo mambo hayajakupata ndio maana mimi natamani wakuchukulie mke wako au kama una gf alafu kula nae sahani moja huyo mwanaume alafu siku ya pili njoo hapa toa maoni yako umeonaje nadhani kwa wewe utaona raha tu.....Na pia kwa hayo maneno yako na wasiwasi na wewe...Pamoja wadau waliomsapoti mshikaji.....ALLY MAPESSA THINK BEFORE YOU TALK IF YOU DONT HAVE SOMETHING TO SAY JUST CHILL BRO!!!

    ReplyDelete
  10. KWA KWELI JAMBO HILI LINAHITAJI BUSARA YA HALI YA JUU SANA HASWA IKIFIKA WAKATI WA KUFANYA MAAMUZI, JAMBO LA MPENZI KUZIMA SIMU, KUJIFANYA HASIKII UNACHOSEMA,KUWEKA PASSWORD,ANAAMKA ASUBUHI ANAKWENDA CHOONI NA SIMU MKONONI,UKITUMA MSG ANACHUKUA LISAA KUJIBU,KUKUPA MAJIBU YASIYO SAHIHI HAYA YOTE YAMEKUWA NI MAMBO KAWAIDA KWA WAPENZI WENGI HASWA KWA VIJANA WA KISASA WENGI WAO HUDIRIKI HATA KUKWAMBIA NIKO JOB LAKINI KUMBE YUKO ANAPATA DRINK NA BEST YAKE UKIULIZA VIPI MBONA UKO HUKU ANASEMA NILIBADILI MAWAZO NIKAONA NIJE KUNYWA DRINK,KWA KWELI NDUGU ZANGU TUSIPOKUWA MAKINI TUTAKWISHA MANAKE HAKUNA ALIYEKAMILIKA NA WOTE WANALAZOMISHA KUAMINIWA BADALA YA KULAZIMISHA WAO KUJIAMINI

    KIPEPEO.

    ReplyDelete
  11. DU KWELI NIMESHAGUNDUA,HAPO JUU KUNA MTOA COMMENT MMOJA AMENIGUSA MIMI, HUYO NI BOYFRIEND WANGU, MY SWEET POTATO,HUWA ANAJIFANYA ANAJUA KUFUATILIA SANA MATOKEO YAKE YANAKUWA MABAYA, YEYE HUWA ANAKUWA NA MARAFIKI WA KIKE BUT MIMI NIKIWA NA MARAFIKI WA KIUME HATAKI NI UGOMVI TU. SIMWELEWAGI.BUT MIMI NINAMPENDA YEYE TU, NA SINA MWINGINE ZAIDI YAKE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...