Mdau Thompson Mmari na mai waifu wake Jamila wakimeremeta agosti 9, 2008 katika kanisa la Christ Embassy Birmingham huko Ukerewe. baada ya hapo waliendelea kumeremeta kwenye bonge la resepsheni katika ukumbi wa hoteli ya Dudley Quality Hotel ya hapo Birmingham.
kwa niaba ya wadau wote globu hii ya jamii inawapa hongera wameremetaji hawa na kuwatakia maisha mema na ya furaha isiyo karaha.
PS: Globu yenu ya jamii pia inaendelea kukaribisha picha za matukio ya jamii kama haya ili tusherehekee kwa pamoja.
libeneke oye!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mshikaji hongera sana kwa kupata mke. Mmependeza sana!
    Kwa sisi tulio ughaibuni kupata wasichana wa kibongo wenye quality za kuwa wake na wao kukubali kuwa wake ni shughuli pevu, walio ughaibuni suala hili wanalielewa vizuri.

    Mdau,
    mctz2000@yahoo.com
    Ughaibuni.

    ReplyDelete
  2. Mwanamme ni Thompson Mmari na mwanamke ni Jamila. Baba yake ni nani?

    ReplyDelete
  3. kaka yangu unayesema ughaibuni hakuna wanawake wenye quality za kuwa wake sio kweli . wapo wenye hizo quality ila kuwaona ndio issue yaan hawajiexpose sana ila wapo wengi tu issue ni kuwajua tu .

    ReplyDelete
  4. dada zetu mnapotea siku hizi naona jamila muislamu umeingia kanisani. haya bwana

    ReplyDelete
  5. Ughaibuni: Wanawake wengi na ila keep in mind kuwa WIFE MATERIAL hawaonekani onekani hovyo hovyo. Hata kwenye hayo ma-party yenu makubwa makubwa hamuwaoni kabisa. Hawana muda huo. Wao wanafikiri wafanyeje kupata pesa na sio kuzitumia hovyo hovyo na hayo ndio maendeleo katika familia. Labda uhame huko uliko uhamie sehemu nyingine labda utawaona. Na ukikaa kuuliza uliza mno wanaume wenzako huwezi kumpata mwanamke wako kwani wengine husema vitu ambavyo hawavijui kuhusu mtu wala hawana uhakika navyo. Msiwe na papara katika kutafuta wake zenu. Angalia unataka nini katika maisha yako ndio umfuate msichana. Tafuta msichana wakati umeshatulia. Ukijituliza ewe kijana na wewe utapata mwanamke aliyetulia. Kama bado unacheza cheza basi utaishia kwa hao hao ma-clubing freeks. Sio mnaenda tu kama mmekatwa kichwa mkikataliwa na wasichana wa maana mnaanza kusema wasichana wa watu vibaya. Hapo ndipo unapoishia kuoa mwanamke ambaye huna raha basi tu bora umeoa na wewe uko kwenye list. Do your homework and do it yourself.

    ReplyDelete
  6. we acha mawazo ya kizamani mwanamke kwenda kwenye party sio kwamba hafai kuwa mke.ulaya stress nyingi lazima sometimes ujimix na watu wengine,nyie ndo mnaojinyonga kwa stress kwa kukaa wenyewe ndani shauri yako sio nzuri kiafya especially kiakili.nenda kaoe kijijini kwenu kama hivyo

    ReplyDelete
  7. Tatizo kubwa ninaloliona kwenye some comments ni kwamba mtu wala hajua maisha ya ughaibuni lakini anatoa comments nadhani ni bora ukapata picha halisi kwanza kabla ya kuanza kuongea mbovu maana sie tulioko huku tunajua maisha kwa ujumla yakoje. UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...