* Twanga Pepeta yawaangushia moja moja
Na Mwandishi Wetu
TAKRIBAN Wabunge 100 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wikiendi iliyopita walipata utambulisho wa jina jipya la Zain Tanzania. Kampuni hiyo ya simu za mkononi inayoongoza katika mtandao wa mawasiliano nchini, iliandaa hafla ya chakula cha usiku iliyoambatana na dansi katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, kwa lengo la kutambulisha jina lake jipya.
Mawaziri, Wabunge, Waandishi wa Habari na wakazi wengine wa Mkoa wa Dodoma, walipata burudani iliyoporomoshwa na bendi ya African Stars (Twanga Pepeta International) na muziki wa kundi la taarab la Dar es Salaam Modern Taarab huku wimbo wa Pembe la Ng’ombe ulioimbwa na Hamer Q ukiwachengua, katika hafla iliyoandaliwa na Zain Tanzania kutambulisha jina lake jipya kwa Wabunge.
DJ maarufu, 2 Shots na bendi ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta International, ambayo hivi karibuni ilishinda tuzo ya Albamu Bora ya Mwaka kupitia Mtaa wa Kwanza, walikuwa miongoni mwa burudani zilizosindikiza utambulisho wa Zain Tanzania kwa Wabunge, hafla iliyoambatana na chakula cha usiku.
Bendi ya Twanga Pepeta ilikuwa na wanamuziki wake mahiri wakiwamo, Charles Gabriel 'Chalz Baba', Salehe Kupaza, Luiza Mbutu, Hamisi Kayumbu 'Amigolas', Msafiri Said 'Diouf', Dogo Rama, Abuu Semhando, Said Jumanne 'Jojoo Jumanne', Ismail Mzunga 'Kizunga', Miraji Shakashia na wanenguaji, Lilian Tungaraza 'Internet', Maria Soloma, Mandela, Super K, Abillahi, Bokilo na wengineo.
Katika kunogesha burudani hiyo, kulikuwa na mashindano ya kucheza muziki yaliyowashirikisha wabunge huku kukiambatana na zawadi anuwai ikiwemo mikoba yenye nembo ya Zain, fulana na muda wa maongezi.
Iddi Azan (CCM), Mbunge wa Kinondoni na Kapteni John Komba (CCM), Mbinga Magharibi walionyesha umahiri mkubwa wa kusakata dansi na walifanikiwa kushika nafasi ya kwanza na ya pili katika mashindano hayo ambayo wao ndio walikuwa majaji wakuu.
Hilo lilikuwa tukio kubwa la tano kuandaliwa na Zain Tanzania ikiwa ni sehemu ya shughuli zake za kutambulisha zaidi jina lake jipya baada ya mengine manne yaliyoandaliwa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo, waandishi wa habari, watu mashuhuri na wakazi wa Dar es Salaam.
"Jina Zain ni zuri. Zain imetuonyesha utandawazi, tunawashukuru kwa maendeleo waliyotupatia. Uwezo wa soko ni wateja milioni 40 million… kati ya hao, milioni 20 wanaweza kuwa wateja wa Zain," alisema Philip Marmo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), aliyekuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo ya kuitambulisha Zain.
Awali, Meneja wa Zain Kanda ya Kaskazini, Samson Majwala alisema katika nasaha zake, kwamba Celtel imebadilisha jina la kutambulika kama Zain, na sasa ina kauli mbiu mpya ya A Wonderful World (Ulimwengu Maridhawa), ambayo inadhihirisha nguvu, ubunifu na muunganiko wa makundi mengi ya wateja, waajiriwa na wadau wengine.
"Celtel imebadilisha jina na kutambulika kama Zain, na kwa kubadilisha jina kuwa Zain, tunachukua mafanikio ya Afrika na kuyasambaza duniani kote, kama mtandao mmoja tutakuwa katika nafasi nzuri ya kuwapa wateja wetu huduma na bidhaa bora zaidi zenye ubunifu mkubwa, pamoja na mtandao ulio bora,” alisema.
"Ikitambulika kama Zain, tumeanzisha mtandao wa kwanza duniani unaounganisha mabara baada ya kupanua na kuunganisha huduma yetu ya One Network (Mtandao Mmoja) kati ya Afrika na Mashariki ya Kati. Huduma hii sasa itapatikana kwa watu milioni 500 kutoka Pwani ya Magharibi mwa Afrika, kuelekea Mashariki ya Kati, ikiwa ni eneo kubwa kuliko Marekani. One Netwok itawawezesha wateja wa Zain kuendelea kuwasiliana na marafiki na familia, kwa gharama nafuu wakivuka mipaka," alisema.
Alisema hafla hiyo kwa Wabunge ni sehemu ya majukumu ya Zain ya mwanzo wa enzi mpya kwa wateja wake Tanzania na kuleta mapinduzi katika mawasiliano na maisha ya Watanzania na huu ni mwanzo wa mafanikio.
"Tunapanua mtandao ambao tayari unaongoza nchini kwa kuwa na mizizi maeneo mengi zaidi nchini ili kutoa mchango endelevu katika kukua kwa uchumi na kusaidia jamii ya Tanzania,” alisema Majwala.
"Tunaamini jina la Zain linaweka msingi madhubuti ambao tunaweza kuutumia kujenga kundi la kampuni 100 zinazoongoza duniani na lengo letu ni kuwahudumia vizuri zaidi wateja wetu.

Hatua hii pia inaendeleza mafanikio ya biashara yetu barani Afrika na itapeleka mbele na kufanikisha kutekeleza azma ya kuifanya Zain kuwa moja ya kampuni kumi za simu za mkononi zinazoongoza ifikapo mwaka 2011,” alisema Majwala.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...