Habari toka Singida zinasema polisi mkoani humo wanawashikilia wanafunzi wanne wa shule ya sekondari ya Chemchem katika wilaya ya Iramba kwa tuhuma za kumuua mwalimu wao wa nidhamu, Rajabu Dude (49).
Kamanda wa polisi mkoani humo afande Celina Kaluba amewataja watuhumiwa hao mbele ya waandishi wa habari kuwa ni Shani Mtua (18), Mohamed Salum (18) and Emmanuel Daud (18) wote wanafunzi wa kidato cha tatu pamoja na Michael Msengi (18) wa kidato cha nne.
Kamanda Kaluba amesema kwamba tukio hilo lilitokea alhamisi usiku majira ya saa mbili unusu wakati marehemu akiwa anatoka kwenye matembezi katika kilabu moja cha pombe kijijini hapo.
Amesema wakati mwalimu akiwa anarejea kwake akiimba kwa furaha, alivamiwa na kukatwakatwa na kichwani na kuchomwa kisu kifuani, kabla washambuliani hawajatokomea gizani
Kamanda huyo amesema mwili wa marehemu uligunduliwa na wanakijiji wenzie ambao waliuarifu uongozi na taarifa kupelekwa kituo cha polisi ambako upelelezi ulianza mara moja. Ndipo watuhumiwa hao wanne, ambao amesema wamekiri kuhusika na shambulio hilo, walipotiwa mbaroni
Kamanda huyo pia alisema baada ya kukamatwa wanafunzi hap waliisaidia polisi kukipata kisu kinachosadikiwa kutumika katika shambulio kikiwa kimetupwa kichakani karibu na eneo la tukio.
Haikuweza kufahamika sababu ya shambulio hilo, lakini Kamanda huyo wa polisi amesema huenda lilisababishwa na kulipizwa kisasi kufuatia adhabu aliyopewa mmoja wa watuhumuwa siku chache zilizopita.
Amesema watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika. Hakutaja itakuwa lini zaidi ya kusema upelelezi unaendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hayo yote yanatokana na tabia za kishenzi za walimu wa kibongo.ubabe tu umewajaa! hata hawako friendly kama walimu wa huku ughaibuni. Mwalimu wa kibongo na dent ni chui na paka!

    ReplyDelete
  2. Ehe Mungu utuepushie haya. yasije yakaanza kuwa kama huku ukimpeleka mtoto shuleni hujui kama utarudi kumchukua jioni mzima pamoja na maulinzi yote yaliopo hapa.

    Na wewe hapo juu hata kama waalimu wetu bongo wanaact kiarabu lakini sio halali kujustify that. Hapo sio huyo aliyefariki tu ndio amendoka. Kwanza familia ya mwalimu huyo na familia ya watoto hao sasa hivi inago through so much.

    Kwani siye hatukuchapwa bila sababu na walimu but we turned out good nahmna aliyeua miaka yetu....

    ReplyDelete
  3. mwanafunzi na mwalimu ndiyo ni chui na paka,hata doktari na mgojwa pia ni chui na paka as well na hata polisi na raia ni paka na panya. je unajuwa ni kwanini???

    kwa mshahara gani unaotaka wewe mwalimu awe friendly?????

    Hao watu sio washenzi kama unavyodai, ila ni stress ya maisha zinawasumbuwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...