Wakati nikiwa naendelea kusaka ze fulanzzzzz ya jamii iliyotoweka masaa 48 yaliyopita katika hali ya kutatanisha, nachukua nafasi hii kutoa ahsante sana kwa kampuni ya FREEMEDIA , wachapishaji wa magazeti ya TANZANIA DAIMA na SAYARI kwa shavu la nguvu walilonipa mie na balozi mwenza wa Zain, Lady JD kwa makala yake ya Ijumaa septemba 19, 2008 (bofya hapa uione).
samahani kwa kuchelewa kutoa shukrani hizi kwani ndio kwanza nimepata nafasi ya kuisoma yote na kujikuta nitakuwa mtovu wa shukkrani endapo kama nitasita kushukuru. asante sana Freemedia.
Aidha, napenda kurudia tena kwamba heshima niliyopewa si yangu mimi ila ni ya wadau wote ambao ni wasomaji na pia waendeshaji wa blog hasa hizi za kiswahili popote walipo. Nasema hivyo kwa sababu heshima hiyo ya ubalozi sambamba na makala kama hiyo ya Freemedia imenisisimua sana na kunifurahisha sio tu kwa sababu nimepata mimi, la hasha.
Ni kwa sababu hatimaye fani ya blog imeanza kupata umashuhuri na kutambulika kwa namna ya kupendeza na si kinyume. Ambavyo ndiyo kusema safari ya kuelekea kutambulika kwa blog kama chombo cha habari kamili kama vingine imeanza taratibu na iko siku tutafika kama ambavyo wenzetu wa nchi zilizoendelea walivyoweza kufika.
Ninachotaka kusema ni kwamba hivi sasa fani ya blog imeshika hatamu katika kila nyanja huko kwa wenzetu kiasi ya kwamba imeshaanza kushindana na fani zingine, ambapo hivi sasa karibu kila chombo cha habari ama taasisi ina blog yenye kuelezea shughuli zake na mambo mengine. Kwa lugha ingine ni kwamba tovuti pekee haitoshi, na blog ni chachandu ya nguvu katika kupasha na kupokea habari ama taarifa.
Vyombo vikubwa duniani kama vile BBC, VOA, REUTERS, DW, CNN na kadhalika, pamoja na kuwa na tovuti, pia vina blog. Na sio blog tu, wenzetu wana mpaka vitengo vya blog pamoja na wahariri mahususi wa hizo blog, kuonesha jinsi walivyo serious na fani hii. Na mambo yao ni mswano kabisa.
Natumai hata sie tutafika huko siku si nyingi zijazo. Hata sijui kwa nini sisi, na wengine wengi katika dunia ya tatu, bado tunasuasua kuipokea fani hii ya blog kwa sababu zisizoeleweka. Pengine ni kwa sababu kuna blog ambazo hazifurahishi hivyo samaki wote wanaonekana wameoza, wakati sio kweli.
Nadiriki kusema hayo yote kwa sababu fani ya habari imo katika mapinduzi makubwa baada ya kubainika kwamba zile zama za habari kuwa ya upande mmoja inayoyoma kwa kasi, na kwamba hivi sasa wasomaji wamekuwa wanashirikishwa kwa kutoa maoni na mawazo yao kwa urahisi na uhuru, kila baada ya kuona ama kusoma habari moja ama ingine.
Kwa lugha ya wenzetu hii inaitwa 'interactivity' (bofya hapa usome zaidi), ambayo imekuwa silaha kubwa ya kuvutia wasomaji wengi zaidi na zaidi. Yaani zama za waandishi peke yao kuwa na kauli ya mwisho inaanza kupitwa na wakati.
Ni kweli kwamba blog zimepanua wigo wa uhuru wa kupokea na kutoa habari, lakini vile vile si uwongo kwamba uhuru huo ukitumiwa isivyo unaleta mushkeri na kutuchelewesha sie wa dunia ya tatu kufika haraka huko tuendako.
Hivyo nashauri na kutoa changamoto kwa wale wote wenye kuendesha blog zinazochafua hali ya hewa katika jamii waache kufanya hivyo kwani ni njia moja inayochelewesha maendeleo ya kweli ya teknolojia hii ya kisasa ya habari.
Ni kweli tuna uhaba wa vitendea kazi (kompyuta na internet) ambavyo hata hivyo haimaanishi kwamba tukae tukisubiri hadi vienee. Je, ni wangapi walijua kwamba siku moja simu za mkononi zitafika hadi vijijini na kutumiwa na mamilioni ya watu bila kujali kipato chao? Jibu la swali hili linajibu swali la je, hii teknolojia ni kwa manufaa ya watu wangapi ama wa aina gani?
Naomba nimalizie kwa kuwashukuru tena FREEMEDIA kwa kutambua umuhimu wa blog, na pia natoa saluti kwa ZAIN kwa kuufungua huo mlango wa kutambua blog kuwa chombo kamili kwa kunitunuku heshima ya ubalozi.
Nafurahi kusema kwamba hivi sasa napata mialiko mingi toka kila sehemu sio kama mwandishi na mpiga picha tu, bali pia mwendesha blog. Natumai wadau wanablog wenzangu nao wataanza kunufaika baada ya kufikiwa hatua hii.
Kwa wale ambao wanataka kujiunga na fani hii ya blog nasema karibuni sana, milango kwangu iko wazi kwa ushauri na kubdilishana mawazo. Niandikie tu kupitia issamichuzi@gmail.com tutasaidiana tu. Wala usisite wala usihofu.
'Play your part, it can be done' Mwalimu Nyerere alisema.
-Michuzi
hongera sana mwana.Nje ya mada-Naomba kujua mkongwe mwenzio MADANGA S.MADANGA yupo wapi kwa sasa au yoyote mwenye habari zake atuhabarishe humu bloguni.
ReplyDeletekazinjema
Nje ya mada, Kumbe kaka Una DIMPLE mashavuni??? khaa !!!! napenda sana once mtu achekapo mashavu kubonyea....... ntakuja kuomba mbegu.
ReplyDeleteToo long to comprehend. Get to the point.
ReplyDelete"Thanks for recognition bestowed on me and I will be of unappriciative if I dont putforth all who blog on this blog. Thats it."
Kuliko kuleta misiasa ya CCM.
Get to the point nigga
mchumia juani hulia kivulini kula kuku bro michuzi kubwa juu.
ReplyDeleteAfu anonimasi wa 5:44 ana kiingeredha kigumu!!!!
ReplyDelete