bosi wa masoko wa zain kelvin twissa akimkabidhi bi mwajabu fungo za Rav4 lake leo. Chini bi mwajabu akitesti gari lake jipya kabisa alilojishndia leo hapa dar
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain Tanzania imemkabidhi gari jipya aina ya Toyota RAV 4, mshindi wa sita wa promosheni kubwa ya magari ya Endesha Ndoto Yako 2, Mwajabu Hassan Salum, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo (Alhamisi, Septemba 18, 2008).

Mwajabu mwenye umri wa miaka 48 ambaye ni mkazi wa eneo la Keko Toroli wilayani Temeke, Dar es Salaam, alikabidhiwa gari hilo na Meneja Masoko wa Zain Tanzania, Kelvin Twissa.

Mwajabu, ambaye kazi yake ni kuuza mbao, ndiye aliibuka mshindi katika droo ya sita Agosti 18, mwaka huu. Promosheni hiyo inahusisha magari 11 yanayotolewa na Zain Tanzania kwa kipindi cha mwaka mzima.
Akiwa na uso uliojaa tabasamu na bashasha, Mwajabu alikabidhiwa gari hilo lenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 40, mbele ya umati wa watu waliojitokeza kwenye eneo lake la biashara, kushuhudia makabidhiano hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Mallya.

"Kama mnavyofahamu Zain Tanzania bado inaendeleza jitihada zake za kubadilisha maisha ya wateja wake kwa kuwazawadia magari mapya kutoka Toyota Tanzania yakiwa yamesajiliwa kwa jina la mshindi na kulipiwa ushuru na bima zote husika.
Zain, kampuni namba moja ya simu za mkononi inayotoa huduma katika nchi 22, inaendesha promosheni ya Endesha Ndoto 2, tutakabidhi jumla ya magari 11 mapya kwa Watanzania wenye bahati likiwemo jipya la kifahari aina ya Toyota Land Cruizer, " alisema Twissa.

"Mwajabu tumemkabidhi akiwa mshindi wa sita wa RAV 4 na Jumatatu (Septemba 22, 2008) saa 5 :00 asubuhi tutamchagua mshindi wa saba wa RAV 4 ofisi za makao makuu ya Zain na tunawaomba wateja wetu wasizime simu zao ili wasipoteze bahati yao ya kunyakua gari," alisema Twissa.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ufunguo na kadi ya gari hilo lililovuta umati mkubwa wa watu kulishuhudia, Mwajabu, alisema anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kutimiza ndoto yake ya kumiliki gari lake binafsi kutokana na kushinda bahati nasibu hiyo ya Zain.

"Kwa kweli nina furaha isiyo kifani, pia sina budi kuishukuru Zain kwa kunitimizia ndoto yangu... hivi sasa nitatulia kwanza, nikae chini na familia yangu kabla ya kuamua nifanyie nini hilo gari," alisema Mwajabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mwenyenacho huongezewa.
    Ng'ombe wa Maskini hazai.
    Maskini akiokota huambiwa kaiba.

    ReplyDelete
  2. Hongera mama, kweli kabla haujafa usikate tamaa,,wengine watu wazima hatujaendesha hata Toyota Corola bado..HONGERA KWELI KWELI, mana kuna wengine tunawaona, wanaishia kuendesha ya kuazimwa na wanaume wao,,hongera mwaya, umetoa jasho kwenye hiyo bahati nasibu....kweli mwanamke MEWATA..

    ReplyDelete
  3. mie yangu mawili.

    1. Kevin twisa kama shati unaamua kuchomoloa chomolea lote, kama unachomekea chomekea lote. siyo nusu umechomolea nusu umechomekea, aah mambo gani haya.

    2. bibie i hope anajua pedal iko wapi

    ReplyDelete
  4. hivi vigezo vya kucheza huo mchezo hamna....?????? Mtu anapewa gari tu je leseni anayo kweli?

    ndio mwanzo wa kupata ajali kila siku.

    ReplyDelete
  5. Duh TANZANIA inazeesha acheni mchezo. Huyo mama namiaka 48 tu?????????? mweeeeeee wenye miaka 48 huku!!!!!! utashangaa na macho yako wakikuambia wana miaka 28 unaamini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...