Mkubwa Habari za kazi,Mdau hapa kwanza kabisa napenda kukupongeza kwa kazi isiyopimika kwa ubora na umakini Bro Michuzi na team yako kwa ujumla.
Pili napenda kukujulisha kuwa kuna kampuni moja inayoitwa Rihanna Arts Promotions ya hapa jijini, imeandaa mashindano ya kumsaka Deejay bora (Bongo Deejays Championship) Tanzania.
Kwa kuanzia wanaanza na mikoa saba ambayo ni Dar Es Salaam, Zanzibar, Mwanza, Morogoro, Mbeya, Tanga pamoja na Arusha.
Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mwezi wa kumi na yatashirikisha wadau mbalimbali wa fani hiyo.
Hiki ni kipindi ambacho yeyote yule anayejijua kuwa anaouwezo mkubwa kwenye fani hii ya U-DJ basi anakaribishwa kwenda kujiandikisha kwenye vituo vifuatavyo kabla ya tarehe 30/09/2008.
Dar Es Salaam: Kisuma Time – Kimara Baruti, Royal Prince Dry Cleaner and Salon – Sinza Madukani
Arusha: Bugaloo Masai Camp na BizKit Fashion
Mwanza: Inuka House karibu na Majukano Hotel
Tanga: G10 Barbers Salon barabara ya kumi na tatu, Nyinda Fashion pamoja na Five Brothers Fashion
Morogoro: Shabani Musa Used spares na Ndaki Auto Spares
Mbeya: Emirates Internet Café, Mbeya Carnival Night Club na Blue House Club
Zanzibar: Starehe Club, Malindi Take Away pamoja na Darajani Kwa Miyanji.
Naomba uwafikishie wadau wa globu yetu ya jamii taarifa hii kwani nina imani wapo wenye uwezo mkubwa kwenye fani hii na wangependa kushiriki.
Mdau Robert wa zain,
kama kutakuwa na maoni au lolote linalohitaji maelezo basi anuani hii waweza kuwapa wadau.
au
0716583599


Kama hilo ni shindano nilitegemea waandaaji watuwekee zawadi zilizoandaliwa kwa ajili ya washindi, vinginevyo tunapata wasiwasi labda mnataka kujinufaisha na vipaji vya watu. Tumeona matukio mengi tu ambapo washiriki wanarushwa zawadi zao na waandaaji, hivyo basi tunaomba uhakiki wa vitu vifuatavyo:- ratiba kamili, majaji ni kina nani (ili tujue uzoefu wao), kanuni za ushiriki, zawadi kwa washindi/mshindi n.k vinginevyo tuachieni ubabaishaji.
ReplyDeletesuala ma judge kujulikana ni wakina nani ni muhimu/maana hata hao ma dj wa bongo wenye kiwango na standard ni wachache mno,wengi wamepenya na kukuzwa na nguvu za radio.....lkn ni weupe!mixing hazitulii mpk loop,tempo 0,scratch ndio ubahatishaji!upeo wa mziki ni mdogo bac taabu tu...
ReplyDeletehivi jamani zanzibar ni mkoa? mimi geography f
ReplyDelete