Waziri wa Ncha Ofisi ya Makamu wa Rais (Mzingira) Dk Batilda Burian akiangalia Kobe akiyekamatwa na Ofisa Habari Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Chipu. anaewapa Maelezo ni Katibu Msaidizi Bw Pondo Ali wakati wa Ziara ya kutembelea Vikundi vya kuhifadhi Mazingira vya Zanzibar Jana. picha na mdau Ali Meja wa Ofisi ya Makamu wa Rais


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Bro. Michuzi,rekebisha jina la Mheshimiwa. Ni Dr.Batilda Burhani.

    ReplyDelete
  2. Sio kobe ni kasa

    ReplyDelete
  3. Anony Sept 28 11:00pm
    Michu yuko sawa ni Buriani

    ReplyDelete
  4. Jamani huyu Batilda Burhani anafanana na mama Salma Kikwete, am I right? hebu muangalieni vizuri. Kidogo inanipa mawazo hii kitu... ama?

    ReplyDelete
  5. WADAU MUNAOELEWA,
    NAOMBA KUULIZA IKIWA HUYU MAMA BURIANI AMEOLEWA AMA YUKO SINGLE?
    NAULIZA KWA NIA SAFI JAMANI, MUSINITUPIE MADONGO.

    ReplyDelete
  6. kobe au kasa???ndo nini??tortoise je?
    ila kweli kafanana na mama kikwete labda ni ndugu hawa mana hii serikali imejaa undugu na ushosti nk...me pia uwa najiuliza sana ivi awa mawaziri wanawake mboni sijawai sikia waume zao ngaa wanatangazwa??au basi waandikwe "Mrs"...ila wanaume kwa kutojiamin asa mwanamke akiwa matawi km ivi???sijui matatizo gani apa??ila awa viumbe wanawake huwa hawana shida apa utakuta anae jamaa wa kawaiiida basi

    ReplyDelete
  7. huyo mama kaolewa na mzanzibari na akabadilishwa na dini ndiyo maana katikati kuna jina salha na ushungi kavalishwa, mzanzibari hataki mchezo kamuweka ndani toto la kimasai.

    ReplyDelete
  8. Huyo mama ameolewa ni mke wa mtu na wala hafanani na mama Salma Kikwete, yeye ni muarusha wa kaskazini mwa Tanzania mama Salma ni wa kusini mwa Tanzania. Na jina lake jamani ni Dk. Batilda Buriani (ni Phd holder sio Dakitari wa maradhi).

    ReplyDelete
  9. Nakubaliana na jamaa hapo juu, huyu hasa ni kasa sio kobe. Kasa aishi zaidi baharini , kobe ni wa nchi kavu na sijui kama aliwa especially yule asiyefunga ramadhan
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  10. Ni ubinafsi au udini kukaa watu kadhaa wakichambua intimate details za watu kama vile dini. Juweni kuna uhuru.

    ReplyDelete
  11. Haya weye anon wa 29, 1.29 pm tutajie au tufafanulie huo undugu wa Dr. Batilda Buriani Muarusha wa Arusha na Mama Salma Kikwete wa Lindi, ukoje huo undugu wao maana na sie tupate kuelewa! Watu wengine huwa wana wivu wa ajabu kabisa huyo mama na PhD yake unamuona hafai kuongoza mpaka abebwe kwa mbeleko? Au kwa sababu hapo kavaa ushungi basi hawezi kazi kwa kuwa ni mwanamke wa kiislam? Watu wengine wa ajabu kabisa, acheni wivu usiokuwa na kichwa wala miguu, kama mwanamke shule yake imepanda haijalishi ni dini gani na amepata nafasi ya uongozi chuki ya nini? Subiri na wewe uwe Raisi uweke shangazi zako, shoga zako, dada zako, wajomba, kaka, na wengineo kama ni rahisi kama unavyofikiria. AU ilitakiwa serikali iwe na viongozi wa kikiristo peke yake ndio ionekane kuwa hao viongozi hawakupendelewa! Sasa inabid mwiko tuuite mwiko wala sio kijiko cha mti, acheni roho zenu za kwanini na tabia zenu za udini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...