dj mkongwe choggy sly (kati, RIP) akiwa na mshiriki na baadaye mshindi wa mashindano ya kwanza ya kucheza breakdance, abdul shalamar (kuia), kwenye ukumbi wa silversands. haya tena wadau wenye kumbukumbu zilizotukuka, tupeni utamu wa mambo yalivyokuwa enzi hizo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Unless I toss a coin I won't be able to tell Abdul Shalamar ni yupi kati ya hao wawili. Waandishi mnaweza kuwasaidia zaidi wasomaji wenu kwa kutanguliza mambo ya msingi...

    ReplyDelete
  2. Hii!kaka Míchuzi umenikumbusha mbali! kwanza huyu mkongwe Hamisi Chogeza aka Dj Choggy Sly(mzee wa kizaramo) bado yupo hai?!
    Katika Madj wakongwe na waliolipagia libeneke la Dico liendelee ! Choggy Sly ni msingi wa madj na ni DJ anayeweza kuilezea historia na mhundo wa mwenendo wa Madisco nchini!
    DJ huyu kama angelikuwa USA,Ughaibuni basi angemiliki chuo cha kuwafundisha maDj au Studio zinazo zalisha mdundo wa Disco Beat! Lakini sitoshangaa nikisikia kuwa ananyanyaswa na jamii ya kizazi kipya cha wasio mjua!
    Hivi kishawahi kupewa hata TUNZO kutokana na juhudi zake?
    Sidhani kama baraza la sanaa linaweza kufanya hivyo!
    Pamoja na kuwa baadhi ya vigogo wa sasa ndio waliokuwa wateja wake au wacheza Disco wakati huo!!!lakini
    bado hawautambui mchango wa DJ Choggy Sly! ndivyo Bongo yetu hilivyo! kama alivyoimba Dk.Remmy
    Kilio Cha Samakani baharini!Machoza
    huenda na maji!

    ReplyDelete
  3. we Al unapendaga kudandia treni kwa mbele. We unaona kabisa imandikwa Sly yuko kati, na Abdul Kulia

    ReplyDelete
  4. nnachokumbuka hilo disco lilikuwa linaitwa k.t.u king transimision unit au kunywa tumia usiogope, sidhani kama enzi hizo titarudi tena, mungu amlaze chggy sly mahala pema peponi

    ReplyDelete
  5. Anon wa 16:18, sidandii kokote. Kati na Kulia vimewekwa baada ya kuombwa - havikuwepo. Sina wazimu.

    ReplyDelete
  6. annon 1.32am
    umemuua wewe au??una uhakika gani mana cjaona mahali huu ujumbe wasema ni marehemu

    ReplyDelete
  7. Aisee umenikumbusha mbali sana. Silversand kilikuwa kijiwe kikubwa cha watoto wa chuo, na disco lingine lilikuwa karibu yake liliitwa Rungwe Oceanic halafu tulikiwa tunatembea ufukweni tukiboreka na moja wapo. Bahari beach, na Africana ya watoto wa geti kali...

    Soda ilikuwa sh 20/=, nadhani kiingili ni sh 30/= (sikimbuki vizuri, mambo ya ofa tena) wakati huo nilikuwa mtu wa soda tu.

    Palikuwa na dala dala likiitwa Scaba Scuba la watoto wa mjini lilikuwa la mwisho kuondoka lakini la kwanza kufika mjini, waliniangusha mara nyingi sana magoti yana alama mpaka leo wakati wakinidrop maana kituo cha kwanza kilikuwa Kariakoo na mimi nilikuwa nashukia Victoria. Nilikuwa na siti yangu pale nyuma!!!

    Tukumbushie basi mambo ya Toto disco (Msasani na kukimbilia basi la mwisho pale kawe)..., Mbowe Club, YMCA, Chezimba, Mawingu club, picnic za ngazi moja... Jamani wakati ndo ulikuwa huo!!!!

    ELEN

    ReplyDelete
  8. Rest in Peace Choggy Sly. Nakumbuka discko zake zilikuwa zenyewe! Those were the days!

    ReplyDelete
  9. Annon 4:48 pm

    Jitahidi urudi darasani. Kama hujui hata maana ya RIP..... mambo ya hatari kweli kweli. Halafu unajifanya kumkosoa mwenzio kwa ujinga wako. Uliza uelimishwe kabla ya kuweka utumbo wako hapa..... Nyambafu.

    ReplyDelete
  10. sly rest in peace ulisha nichekesha saaaaaana hamna komedian kama wewe TZ (ulikuwa) kila napo muona steve harvey uwa nakukumbuka.mwenyezi aweke roho yako peponi.

    amina

    ReplyDelete
  11. R.I.P Salum mrisho(DJ CHOGGY SLY)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...