WAKATI MIPANGO YA KUMPELEKA NJE YA NCHI MPIGANAJI ATHUMANI HAMISI (PICHANI) ALIYEJERUHIWA VIBAYA KWENYE AJALI YA GARI ILIYOTOKEA MWISHO WA WIKI ILIYOPITA HUKO KIBITI, MARAFIKI WA KARIBU WA MGONJWA WAMEAMUA KUFUNGUA MFUKO MAALUMU WA KUMCHANGIA ILI KUMSAIDIA YEYE NA FAMILIA YAKE KATIKA WAKATI HUU MGUMU. MFUKO HUO UNAITWA
'SAIDIA ATHUMANI HAMISI APONE'


MWENYEKITI WA MFUKO HUO NI DADA ASHA BARAKA WA TWANGA PEPETA AKISAIDIANA NA KAKA ERIC SHIGONGO BOSI WA GLOBAL PUBLISHERS PAMOJA NA BALOZI WA ZAIN AMBAO TAYARI KILA MMOJA WAO AMETOA SHILINGI LAKI 3 KWA AJILI HIYO.
HALI YA MGONJWA BADO TETE NA JUHUDI KUBWA ZINAFANYWA NA MADAKTARI WA MUHIMBILI KITENGO CHA MOI KUMTIBU. KINACHOSUBIRIWA NI BARAKA ZA MADAKTARI HAO ILI ATHUMAN HAMISI ASAFIRISHWE HARAKA KWA MATIBABU NJE YA NCHI.
TAYARI KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA VODACOM IMEELEZA NIA YAKE YA KUSAIDIA KWA HALI NA MALI KUFANIKISHA MATIBABU YA ATHUMANI HAMISI POPOTE DUNIANI


MICHANGO YA KUTUNISHA MFUKO HUO WA SAIDIA ATHUMANI APONE UNASIMAMIWA NA DA' ASHA BARAKA NA ANAYEPENDA KUCHANGA ATUME KUPITIA AKAUNTI


ASHA R. BARAKA
A/C NO. 01J 2018672700
CRDB BANK
HOLLAND HOUSE BRANCH
DAR ES SALAAM
KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU NAMBA
+255 713 606 564

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Naomba niulize swali, je hapo MOI hapati matibabu? Je madaktari wamesema hawawezi kumtibu? Ingekuwa vyema haya maswali yajibiwe kabla kuomba watu fedha za kumpeleka nje maana isjekuwa imekuwa fashion kupeleka wagonjwa nje ya nchi kutibiwa ilhali kuna wengi wanaotoka nje ya nchi kuja kutibiwa hapohapo MOI.

    ReplyDelete
  2. Inaelekea unayeuliza hilo suali haujawahi kutembelea hospitali za Bongo, wala kusikiliza kilio cha wananchi kuhusu matibabu yanayotolewa huku nchini. Ujue basi kwamba huku Bongo kuna hali ya uhaba wa vitendea-kazi na upungufu wa utaalam tukifananishwa na nchi kama India au Afrika ya Kusini. Hata kupata CT-Scan nchini imekuwa ni shida. Ndio maana siku zote unasikia watu wanatafuta kupata tiba nje ya nchi pamoja na madaktari wa Bongo kukimbilia ugenini ili kupata ajira wenye mshahara endelevu.

    ReplyDelete
  3. CT Scan nayo shida au mzee unataka kuuza habari? MNH mbona pako poa, madakatari hawajashindwa kumtibia ila tiba ni ghali mno ukilinganisha kila mwananchi kaelekeza kilio chake kwa serikali. Ushauri kwa wachangiaji wa harambe hiii...fungu flani tuwape wauguzi hapo Muhimbili uone kama Athmani hajaja juu fasta. MNH ina kila aina ya daktari bingwa ila mshiko ndo ivyo...ccm yenyewe imeongeza mishahara kwa wapiga porojo wake wanaacha kuwajari watu ambao ni uti wa mgongo wa taifa hili....Athman Mwenyezi atakuponya haraka na familia yako ipewe faraja kwa kipindi kigumu kama hiki.

    ReplyDelete
  4. Anonym. wa 5:32 kauliza maswali muhimu sana. Nakupa big up ndugu yangu kwa kuliona hili. Labda niongezee, mnasema kuna kampuni ya simu (VODACOM) imekubali kugharamia matibabu, sasa na hii michango ya nini tena?

    ReplyDelete
  5. Fungueni account maalumu kwa ajili yake kama jina mulilopendekeza hapo juu' hili hufanyika katika mabenki yote, hata huku nje kitu kikijitokeza ufunguliwa account ya muda na kikiisha account hufungwa, musiweke pesa kwenye account ya mtu binafsi sasa atatenganishaje accountability ya pesa ya mgonjwa na yake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...