mdau mchokozi will edward wa zk public relations akiwa katika neshno la imarati

robert pires
Naungana na Pires kwamba: Arsenal itatamba Ulaya

Kamanda,
nimesoma kwenye gazeti la The Sun, mchezaji wa zamani wa Arsenal, Robert Pires amesema kwamba Arsenal msimu huu huenda ukatwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mkongwe huyo ambaye hivi sasa anachezea Villarreal ya Hispania, alisema vijana hao wanaonolewa na kocha wetu, Arsene Wenger, msimu huu ni wazuri zaidi kuliko msimu uliopita, licha ya kuwapoteza nyota kama Mathieu Flamini, Alex Hleb, Gilberto na Jens Lehmann.
Pires amesisitiza kwamba Gunners wanaweza kutwaa taji lao la kwanza msimu huu tangu walipotwaa kwa mara ya mwisho Kombe la FA mwaka 2005.
Alisema: "Nimekuwa nikitazama mechi za Arsenal wakati wote – Sijawahi kukosa kutazama mechi yao.
“Nafikiri wamepiga hatua kwa kiasi kikubwa. Wachezaji wamekuwa imara zaidi, ni kikosi cha chipukizi ambao wana uzoefu wa kutosha.
“Ninafikiria mambo mazuri kuhusu Arsenal mwaka huu.
"Sijui kama litakuwa ni taji la Ligi Kuu England au Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini msimu huu angalau wanaweza kutwaa taji moja.”
Hiyo ni kauli ya Robert Pires ambayo mie mdau wa Gunners, WILLY EDWARD wa ZK Public Relations, pia naungana naye.
Mambo ndio kwanza mmeanza kuyaona, ni dozi kwa kwenda mbele, Blackburn Rovers alipigwa 4-0 wiki iliyopita, jana Bolton Wanderers naye kabugizwa 3-1 kwao.
Man United, Liverpool (subutuuuu! - michuzi) , Chelsea mtakoma safari hii!
Kikosi chetu kimejaa chipukizi lakini kinatisha:
Makipa: Manuel Almunia, Lukasz Fabianski na Vito Mannone.
Mabeki: Bacary Sagna, Kolo Toure, William Gallas, Alexandre Song, MikaelSilvestre, Johan Djourou, Gael Clichy.
Viungo: Abou Diaby, Cesc Fabregas, Tomas Rosicky, Samir Nasri, Denilson, Aaron Ramsey, Jack Wilshere, Emmanuel Eboue, Amaury Bischoff.
Washambuliaji: Eduardo da Silva, Robin van Persie, Carlos Vela, Theo Walcott, Emmanuel Adebayor na Nicklas Bendtner.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Blah blah blah yote hayo ni kwasababu miaka ya nyuma tulikuwa na wazee na msimu huu tumeamua kununua vijana.hivi huwa hamchoki??kuongea tuu.

    ReplyDelete
  2. Nguvu ya soda ...

    ReplyDelete
  3. Michuzi tuheshimiane naye jamani mwacheni kuhusu mpira michuzi aweke timu yake. Blog hii kila mtu akianza kusema atoe kuhusu timu yake mchezaji wa zamani kasema nini unafikiri kutakalika itajaa mpaka juu, yote sababu Arsenal leo yuko juu aliyekuwa juu sie kina MAn City tunamsubiri chini aje kukaa na sie hasa man united plz mwacheni michuzi na bwawalake, mengine ok ila mpira kuhusu timu za nje plz tutafute blog mpya ya kiswahili kuhusu mpira kwa michuzi mwacheni atoe yake basi akifungwa huwa anachuna kutowa. msiwe kama william wa Uk haonekani mpaka siku ameshinda mie sinipo yeye na G7 wa Uk na William wa Uk soon mtawaona man u ikishinda. sina mengi from JO. sie nafasi yetu ya 5 au 6 hatuna matatizo na mtu man u watamaliza wa 8 safarihii bingwa Arsenal wa 2 Liverpool Then Chelsea 4 Aston Villa au MAn City.

    ReplyDelete
  4. duh
    ivi wanaume uwa wana pozi izi za pics???uzipeleke home swity home ulikua ulaya???teh teh watajuaje??
    kimeo,,,,,,,,,

    ReplyDelete
  5. Arsenal hamchelewi kupiga kelele kama Taifa Stars, ooh Ringobert anatumia vitisho vya mwili na kutupiga viatu ndo maana tunafungwa.

    Juzi bahati yenu kina Diouf na wenzie wamehama Bolton Wanderers amasivyo mgelala.

    Juzi tu Wenger huko Urusi alikuwa analia ooh mtaniulia Wilcott, si mnaona ManUtd walijaribu kwa Chelsea wakaambulia kadi 7 za njano.

    Sasa wababe wote wa Northwest England, kina ManUtd,Liverpool watakuja kuwafunga 7-0 bila kadi kwa kuwakwatua viatu.

    ReplyDelete
  6. unafagia humo nini baba...tehe...tehee te....

    ReplyDelete
  7. Yale yale!! eti unafagia!! kwani kufagia sii kazi????jamani ndo maana bongo huwezi tumia choo cha city unless una uharo. michuzi please naomba uwaelimishe hawa wanajamii ambao bado wana mazereu ya kazi.nimefagia huu mwaka wa 7 sasa na nimeweza kujisomesha na kuwa bread winner wa familia yangu.hudadeki tuko mbali saana kama mawazo ndo hayo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...