latoya leo hoteli ya southern sun
latoya akijibu maswali ya waandishi juu ya ushiriki wake kwenye big brother III. shoto ni ronald baraka shelukindo meneja wa operesheni wa multichoice tanzania na kulia ni furaha samalu meneja mauzo na masoko wa kampuni hiyo
ronald baraka shelukindo akiteta na latoya wakati wa mkutano na waandishi leo
mkuu wa wilaya ya nanihii na balozi wa zain na latoya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Mkuu wa nanihii sikuwezi! Huo mkono begani wako au wa Latoya mtoto wa kike?? Sijauelewa

    Mdau L

    ReplyDelete
  2. Latoya ni half caste au pure african breed? anafanya wapi kazi arusha?anaishi wapi?alisoma wapi?kalelewa na nani?

    ReplyDelete
  3. Ha! kumbe huyu mtoto ni mrembo hivyo. Balozi jitazame mfungo huu!!!

    ReplyDelete
  4. BALOZI MITHUPU! SIJAUNGA MKONO STAILI YAKO HATA KIDOGO. UMEPIGA KONOZ NDANI YA MFUNGO VILEVILE HICHO KIDOLE SIJUI UMEKUSUDIA NINI?
    I HOPE MAMOU HUWA ANATEMBELEA BLOG HII.

    ReplyDelete
  5. Picha nzuri sana michuzi,watu wamemponda sana huyu 'mdada'.Ila mimi napingana nao kidogo.Huyu binti yuko very strong kwenye kujieleza.Presenter maarufu wa Mnet KB juzi(wakati Latoya anatolewa nje ya jengo)alikuwa anamwuliza maswali magumu,na ya mitego sana.Latoya alikuwa makini kwenye kuyajibu kwa ufasaha na alikuwa anayagundua mapema maswali yale kabla ya kuyajibu.Huku akiwa amejifunika bendera yetu ya Taifa,ugenini Latoya alijibu maswali kwa confidence kama vile alikuwa mshindi!!(Sijui leo alipoongea na waandishi).Mambo ya sex affairs ni masuala binafsi,Latoya ni binadamu.Ana uchangamfu wa kuzaliwa nao.

    ReplyDelete
  6. Mheshimiwa balozi naomba kuuliza hiyo sign yako ya kuonyesha kidole kidole kidogo cha mkononi una maanisha nini? kuna maana nyengine ambayo ni kuwa unamsema mwenzio kuwa una nanhii ya kiume ndogo!

    ReplyDelete
  7. Kaka Michuzi hicho kidole vipi? Mwezi mtukufu huuu hahahah unakuwa kama unataka kuna nihii....

    ReplyDelete
  8. kwa kweli huyu dada ametudhalilisha sana huko South,jamani siku ya kwanza tuu kanza kuparamia wanaume na kushikwa shikwa! mi sijapata kuona kwani huko big brother ukitaka kushinda ndo aliambiwa afanye aliyoyafanya? hilo ni fundisho kwa wengine wajao asisingizie kuwa ni mchezo kuna kushindwa na kushinda, alizidi kujilainisha. hakufundwa huyo

    ReplyDelete
  9. Kaka Michuzi, hicho kidole cha mwisho kidogo, kina maana gani???? lazima utakuwa unajua maana yake kwenye picha ya mwisho,au ndio mbinuo huooo !!!

    Huyo dada tumwache kasha likoroga basi basi akalinywee Arusha... MATONGEE au SOWETO GARDEN.

    Mdau,
    SWEDEN

    ReplyDelete
  10. Hayaa jamani kimwana chetu ndio hicho kimerudi na mkuwaa wa wilaya ya nanihaa na balozi wa zain kapiga nae picha.

    ReplyDelete
  11. Kaka swaumu na hilo kumbatio kulikoni?! Au bi mdogo huyo?

    ReplyDelete
  12. Bro Michuzi hicho kidole unacho kielekeza kwa huyo latoya una maanisha nini? je una maanisha %$#@!&^%%^$#%^(@#! BBA3 huyu hapaaa au?

    ReplyDelete
  13. Mheshimiwa balozi....Huu ni mwezi mtukufu usisahau....

    I am very proud as a Tanzanian kwa jinsi binti yetu alivyojiwakilisha na kutuwakilisha kwenye jumba la BB3. Kwa kweli alivyoipeperusha bendera ya Tanzania kila siku inatia moyo sana. I was also very happy with the way she presented her task in the dump. It was very educative na imeonyesha kwamba anaweza kwenda mbali in issues of presentation.

    Kama alivyosema, ni bora kwamba ametoka ili awe na wigo mpana zaidi wa kuvua "samaki". Kwa kipindi alichokaa kwenye BB3 house kinatosha kabisa kumfanya afanikiwe katika malengo yake.

    Namtakia kila la kheri dada yangu!

    ReplyDelete
  14. Balozi wa Zain wats wrong with your finger mwezi Mtukufiu huu.
    Ila mmependeza usijali najua My wife wako (Mamito) hatomind

    ReplyDelete
  15. Ebwanaeeeh! chuma kipo single?

    ReplyDelete
  16. Najua wengi mtapinga hichi ninachoandika sasa hivi:

    Huyu binti alitaka kuleta zile za kibongo bongo za kutoka kwa kuigiza alichofanya mwenzako bila kujua muanzilishi alijipanga vipi kukabiliana na changamoto. Huyu mtoto alidhani kwa kuwa Rich alifanya sex mle ndani akashinda basi na yeye anaweza kuwa hivo. AU alidhani kwa kuwa Gaetano alifanya same thing na kupata umaarufu basi na yeye aige..

    Hii iwe fundisho kwa girls wote wa kiafrica, this is men's world! Like it or Not..angekuwa mwanaume ndo kafanya aliyofanya Latoya angeonekana dume la mbegu na watu wange vote ili abaki waone picha za bure. Lakini alivyofanya Latoya kaonekana kicheche, nilikuwa Rose garden ile wiki ya kupiga kura na siku hiyo tulikuwa kama na debate dizain kuhusuiana na Latoya na watu kibao waliomba tu atoke coz waliona kama anatuaibisha na mimi ni mmoja kati ya waliovote yule mwingine abaki.

    Ni wakati wa Multi choice kuwaiga Wenzetu ambao wawakilishi wao wa BBA kabla ya kuondoka kwenda kuwakilisha nchi wanawapa nafasi watu kuwashauri, kama walivyofanya Botswana.

    All in All karibu nyumbani mama, jiandae sasa kuanza kutongozwa na mijibaba yenye uchu na totoz kali kama wewe. Usipokuwa mjanja huchelewi kupata skendo kwenye magazeti ya udaku au watu hawachelewi kukupa kigari chekundu.

    ReplyDelete
  17. huyu dada bomba ila huo mkono wake unatisha inaelekea anapiga sana push up maana kono limekomaa kwa style :-)
    mdau sweden

    ReplyDelete
  18. Namtakia kila la kheri Latoya. Sijali tabia wanayomsema aliiionyesha hiyo anajua yeye na Mungu wake. Mwanzo sikufurahishwa na tabia ya kugive up task mapema sana kila task alionyesha kukata tamaa haraka lakini nilifurahi alivyogunduwa na kujirekebisha mwishoni na kumaliza a very challenging task. LATOYA IF YOU HAVE LEARNED ANYTHING FROM BB IS DO NOT GIVE UP ALWAYS GO ALL THE WAY LIFE WILL COME WITH CHALLENGES BUT DON'T GIVE UP...i KNOW YOU WILL MAKE IN LIFE YOU SEEM TO BE A BEAUTIFUL PERSON IN AND OUT...SO DO NOT LET THIS FAILURE DISSAPOINT YOU

    ReplyDelete
  19. teh teh namie swali kama la anon wa kwanza, huo mkono begani kwa kaka Michu, ni mkono wa Michu au wa nani, PLEASE do not tell me ni wa huyu binti, mmh mkono mbona wa kiume, jamani hamfanyagi hand treatments...
    pia napenda kujua huyu mtoto ni mtz pure au mzungu wa kuchovya, uzuri anao ila mmh kama ni wa kuchanganya, basi bongo tumezidi kupapatikia watoto wa kuchanganya.

    ReplyDelete
  20. BARAKA SHELUKINDO MAMBO YAKO MSWANO!

    ReplyDelete
  21. Mheshimiwa balozi na mkuu wa wilaya, hebu jilie mikonoz kiulaini, baada ya kazi ngumu. Mmependeza sana hapo, na mnatukonga nyoyo wadau. Wadau mnaonaje haka kashati ka mheshimiwa balozi na mkuu wa wilaya tukikapandisha cheo kawe kanatumika badala ya fulanazz?

    ReplyDelete
  22. Mtaani unasemwa KISONOKO!,
    redioni wametangaza HABARI zako,
    magazetini imeandikwa KASHFA yako,
    bloguni yametandazwa mapicha yako,
    televisheni zimeonyesha SAKATA lako!!
    SAKATA LAKO, SAKATA LAKO!

    ReplyDelete
  23. Mkuu wa wilaya mfungo vipi hapo? au tutalimaliza mambo yote kwenye zile saba za extension? hahahaaaa mambo ya Balozi wa Zain

    ReplyDelete
  24. Kumbe Mkuu Na Balozi Wa Naniliu Bitozi Nyangema????? Angalia Pozi Lako Na Hiko Kidole Kimekosa Pete La Diamond Gram Kama 50 Hivi

    ReplyDelete
  25. nanyie kutwa mmedhalilishwa mmedhalilishwa wakati nyie wenyewe mabingwa wakunanihiii ebu muacheni dada wa watu nyie wenyewe waswafiiiiii ebu angalia maisha mengine dada yaliyopita yamepita

    ReplyDelete
  26. Mimi ninavyoona huyu msambaa Shelukindo angemuoa Latoya.
    Sijui kwanini lakini naona wana match sana

    Mdau
    UK

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...