Mshiriki wa shindano la Big Brother Afrika III kutoka Tanzania Latoya Lyakurwa akizungumza na aliyekuwa mshiriki wa Big Brother Afrika II toka angola, Tatyiana (huyu naye kaja bongo sijui kufanya nini), baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo akitokea sauzi katika jumba la mashindano hayo.

Binti huyo ambaye anakuwa mtu wa kwanza kutolewa katika mashindano hayo alisema kilichokuwa kinatokea katika jumba hilo ni mchezo tu hakuna vingine.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Michuzi umenifurahisha sana hapo nimecheka sana eti (huyu wa ANGOLA sijui kaja bongo kufanya nini!!inawezekana anakula malavidavi(jina jiipya kabisa nilikuwa silijui) na jamaa yake yule walikuwa kule kwenye BBA2 Sasa huku ni kama home ya pili!!1ila nimecheka sana hapo ulivyooongezea
    Jo

    ReplyDelete
  2. sio mbaya! katusave kichizi na sex skendo. obviously mwaka huu ingekua tuff kubeba $$$,$$$. richiana=laricco
    bond

    ReplyDelete
  3. AFAZALI AMEREJEA TUPATE KUMNYWESHA VIDONGE VYA ADABU. YAANI ALIBOA KINOMA HUKO SAUZI, MWANAMKE KISEBENGO KAMA HAJAWAI KUONA WANAUME KHA!

    ReplyDelete
  4. Tanzania people are really pretty

    ReplyDelete
  5. Mdogo wangu latoya uninoboa sana sana ndani ya jumba,tatizo uliona kuwa sex ndo itakufanya ubaki ndani ya jumba na bahati nzuri ndo imekutoa tena asubuhi kweupe. kazi kwako sasa na boyfriend wako.
    Yote tisa watoto wa kichaga wazuri jamani. karibuni uchagani.
    Waosha vinywa kazi kwenu, tehe tehe!

    Mangi wa K'koo

    ReplyDelete
  6. ALicho nifurahisha Latoya ni kutomba radhi wadanganyika kwa uwakilishi wake mbovu.
    Kwa taarifa niliyonayo kwa wadau, Latoya hana BF, ndo maana mjengoni palikuwa hapatoshi kwa vidume kupiga madenda, haya tena amerudi nyumbani mafisadi anzeni kwenda mbio.
    Jamani ehe...mnakumbuka ujio wa Abby Bongo?? ilikuwa kama ivi Tatyana anavyokuja, sasa ivi wadau wamechukua jumla na kazi wamempa na huyu Tatyana nahisi kuna fisadi kesha tangaza vivutio vya uwekezaji...yetu macho, lets wait n c.

    BBA12
    Gwanzhou

    ReplyDelete
  7. Yaani Latoya ukiacha mambo ya kijinga uliyokuwa ukifanya ya kung'ang'ania wanaume, ulikuwa na uwezo wa kufika mbali sana. Umetuuzi Watanzania kwa mengi sana, umetutia aibu sana haswa sisi wanawake zaidi pale ulipovua nguo mbele ya wenzako. Sitaisahau siku ile!!

    ReplyDelete
  8. Yote tisa mimi umeniboa uliposema ulikua unataka umaarufu watu wakujue, WHAT THE HELL CAN YOU OFFER IN THIS WORLD TO MAKE PEOPLE REALISE YOU EXISTANCE??? Toya you could keep that for yourself sio maneno ya kuongea mbele za watu unatufanya wa TZ tuonekane majuha watu wanashindania $100,000 wewe unagombea umaarufu, hapo umechemsha.

    ReplyDelete
  9. Yote tisa mimi umeniboa uliposema ulikua unataka umaarufu watu wakujue, WHAT THE HELL CAN YOU OFFER IN THIS WORLD TO MAKE PEOPLE REALISE YOU EXISTANCE??? Toya you could keep that for yourself sio maneno ya kuongea mbele za watu unatufanya wa TZ tuonekane majuha watu wanashindania $100,000 wewe unagombea umaarufu, hapo umechemsha.

    ReplyDelete
  10. Ha ha ha ha, mwanamke komo(forehead)...!

    ReplyDelete
  11. hahahhahaah michuzi mbavu zangu huyo wa ANGOLA anakuja kutafuta nini hahaha simple si mlimuita wifi ndio anautimiza kwa kujileta heheheeh na mbado hehehehehe bado nacheka

    ReplyDelete
  12. Nyie watu acheni kumuandama mtoto wa watu, Alichofanya nini cha ajabu ambacho Richard hakukifanya? Au washiriki wengine hawakukifanya? Au kwa sababu mwanamke? Acheni kumuandama na maneno. Bahati haikuwa yake na nchi nyingi zilishasema kuwa tanzania wamezidi kushinda na mara hii walipania kuwatoa watanzania nje. Mie sioni cha ajabu alichofanya ambacho washiriki wengine hakifanyi sasa hivi. Acheni kuchonga wabongo. mwacheni mtoto wa watu.

    ReplyDelete
  13. Wewe 12:14 acha kutetea upuuzi. huyo demu kachemsha. Watazamaji wanaangalia character, siyo kuparamia wanaume/wanawake. Richard alikuwa mtulivu sana mwanzoni. He fell in love with our wifi from angola. Wale walikuwa wanapendana kikweli. Huyo Latoya na komwe lake, akajifanya kukopi ya richard na kumfuata muangola. Unadhani watazanaji hawagundui copy cat. Richiana was the real thing. Ananikumbusha MA MISS... I quote "nikishinda nitasaidia watoto yatima na wajane...." Thinking capacity ndogo sana. Inasikitisha....That's it I'm signing out!

    ReplyDelete
  14. wote mnaofuatilia BBA ni wachovu tu! Wewe unaangalia kusudi uone nini? eti watu wakae ndani ya nyumba siku sijui 90. Mlikuwa mnaangalia kusudi awa-entertain...sasa kawa-entertain mnamponda...kha. Mmechoka sana! Ni sawa na kuangalia mechi ya ndondi alafu uanze kulalamika jamaa kaumizwa...ulitegemea nini?...kudadadeki!

    ReplyDelete
  15. Bro Michu. leo umefurahisha sana wadau nikiwa mmoja wao kwa hiyo statement yako kwenye mabano. Jibu ni rahisi sana, yawezekana kuna jamaa wameanza ubia, kuna uwezekezaji wa aina nyingi mkuu huu unaosikia viongozi wanawavutia watu wa nje waje. Utasikia tu ameshapewa na kazi wakati wabongo wanalia kila siku kuwa hakuna kazi.

    ReplyDelete
  16. wewe anony.. wa Tarehe September 24, 2008 9:10 AM, angalia matumizi ya lugha....

    """"ALicho nifurahisha Latoya ni kutomba radhi wadanganyika kwa uwakilishi wake mbovu.""""""


    ...kuomba radhi na siyo kutomba radhi....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...