CCM TAWI LA LONDON
MKUTANO MKUU WA KUCHAGUA WAJUMBE
15 WA HALMASHAURI KUU YA TAWI (BEC).
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wanachama Wote - C C MWakereketwa Wote - C C MWapenzi Na Wana-Mapinduzi Wote
Tarehe: 16/11/2008
WAPI NA MUDA: (MTAFAHAMISHWA SIKU ZIJAZO)
Wanachama wa CCM watakaopenda kukugombea nafasi hizo fomu zinapatikana kwenye tovuti ya Tawi:
pamoja na Ofisi za Mashina, ada ya fomu ni £ 10.
Wanachama wanatakiwa kutuma fomu iliyojazwa kikamilifu kwa:
Katibu wa Tawi,
02 Appleshaw Court,
02 School Road,
Tilehurst,
Reading,
RG31 5AL.
(Kwa Kumbukumbu: Tafadhali Wasilisha nakala (kopi) ya fomu yako kwa Mwenyekiti wa Shina pale/jirani na unapoishi.)
Malipo ya Fomu: Wagombea wanatakiwa kulipia moja kwa moja kwenye akaunti ya Chama na kuandika Jina lake kwa kumbukumbu. Tafadhali tunza risiti yako kama kumbukumbu.
Akaunti ya Chama ni: Benki: Lloyds TSB (UK)
Tawi: Market Place, Reading
Jina la Akaunti: Chama Cha Mapinduzi
Akaunti Namba: 0587300 na Sort Code: 30-96-96
Kwa ufafanuzi zaidi, tuma Barua Pepe: info@ccmlondonuk.org
Pia unaweza kuwasiliana na viongozi wa Tawi:
Maina Owino – 07900040288 - Mwenyekiti Susan Mzee- 07799435327 - Katibu
Alan Kalinga-07738916447 – Katibu wa Uchumi na Fedha
Moses Katega – 07791584289 – Katibu wa Siasa na Uenezi
Wanachama Wote Mnakaribishwa Kugombea Nafasi Hizo
-- Wenu katika ujenzi wa Taifa
Soames Phares
Mkurugenzi wa Habari na Teknologia
Chama Cha Mapinduzi
Tawi la London
United Kingdom

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Get a life Soames.

    ReplyDelete
  2. NILIKUWA NAULIZA TU IKIWA NA NAFASI HIZI ZA UONGOZI NAZO ZINAINGIA KATIKA ILE MISHAHARA MIPYA YA CCM ILIYOTANGAZWA KARIBUNI YA KUANZIA MILIONI MOJA?

    Mkereketwa

    ReplyDelete
  3. Mimi sikai London na huku nilipo pengine ukiwahesabu watanzania hata wa ujumbe wa nyumba kumi hupati. Je mtaniruhusu nije nigombee huko kwenye matawi yenu halafu nitakuwa nakuja huko kwa train ikibidi????

    ReplyDelete
  4. duh hii kali, tawi ni london lakini katibu wa tawi anaishi reading! ama kweli penye kula ......

    Halafu nataka kuuliza sana tu hiki chama cha mapinduzi ni mapinduzi gani haya? tanzania bara walipata uhuru na zanzibar ndio waliopinduwa, jee hii ina maana hiki chama ni cha zanzibar? but then zanzibar sio nchi? ok ok msirushe marungu nauliza tu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...