Dear Bwana Michuzi,
Naomba msaada tutani. Mimi ni mdau mzuri sana wa globu yako na hua haipiti siku mbili hata kama niko bize namna gani, bila kui-peruzi globu hii.
Sasa, nina ombi kidogo ambalo nilikua nataka uniwakilishie kwa wadau wenzangu hapa hapa nchini, nione kama itawezekana kupata msaada. Kwa kifupi nikwamba sio watu wote wana upeo sawa, na kuna wengine wanachukua mikopo kwajili ya kununua gari, iwe ya kikazi manaaake biashara, ama ya binafsi tu.
Hawa watu wanakua wengi kaajiriwa serekalini ama kwenye makampuni ya binafsi ya nguvu (corporates), ama sekta ya benki. Kwao kupatiwa mikopo ni rahisi kwani muajiri anakua guarantor. Ila kuna baadhi ya vikundi vya watu ambavyo hawana such guarantors ila wao ni credit-worthy pia.
Kwa mfano mie nataka kuuza ama ku-trade in gari yangu nnayotumia ili niweze kupata nyingine ya kisasa, bali sio kusema kwamba ninayotembelea imechoka sanaaaaa. Japo kuji up-grade tu.
Sasa, ina maana hapa nchini hamna wauza magari ama commission agents/dealers ambao wanaweza kukubali trade-in, tuseme kwa mfano, thamani hiyo iwe milioni 3, kisha niongezee milioni kama 2 na kukopeshwa gari ya thamani kama milioni 8 hivi??
Mradi wabaki na log-book hadi mtu amalizie malipo, na mradi kuwe na maelewano na written contract ambayo wanasheria wamehusishwa. Naomba uniwakilishie hili. Kama kuna mdau anayehitaji kuwasilana nami anitumie barua pepe kupitia
AMA
Asante.


Mdau, swali lako zuri sana na nafikiri sio wewe tu unawaza hivyo. Watu wengi tu wana mawazo kama yako.
ReplyDeleteBinafsi nahisi kwa soko la Tanzania, bado mpango(scheme) kwa sababu hakuna mfumo wa kumbukumbu za kueleweka kwa watu.
Nchi za wenzetu inawezekana kwa sababu wanaweza kuku-trace pale mtu unapotokomea na gari/deni.
Sasa wewe unaweza kuwa mwaminifu na kuhakikisha unarudisha deni, lakini asilimia kubwa ya watu wataingia mitini.
Kuna sababu nyingine zinazohusisha bima, au mali pindi mkopaji akishindwa kulipa (kwa sababu yoyote ile) na vigezo vingine vingi.
Nafikiri hizo ni sababu chache ambapo watu wanaona isiwe taabu wanaamua ku-deal na cash basis.