Mchungaji Mtikila alishambuliwa mjini Tarime alipokuwa akiwanadi wa gombea wa chama chake wa Udiwani na Ubunge.
Habari zilizopatikana kutoka huko jana jioni zilisema kua, Mchungaji Mtikila alipatwa na mkasa huo wakati akizungumzia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime (CHADEMA), marehemu Chacha Wangwe kwamba kilisababishwa na watu fulani.
Kwa mujibu wa habari hizo, Mchungaji Mtikila alipata maeraha kadhaa kichwani ambapo alipelekwa katika zahanati ya Tarime na kushonwa nyuzi tatu na Dk. Philemon Hugilo.
Aidha, ilielezwa kwamba, Mchungaji Mtikila alilazimika kuvalishwa shuka nyeupe kutokana na nguo zake alizokuwa amevaa, kutapakaa damu. Habari zaidi zilisema watu wanne wametiwa mbaroni kuhusiana na tukio hilo. Chanzo: Nipashe/Mzee Wa Mshitu
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...