Baadhi ya wanachama wapya wa NSSF wa Uingereza Mlolele Mavanza (chini, kulia) na Joyce Msafiri Makanta wakikabidhiwa kadi zao za uanachama za NSSF na Afisa Mwandamizi wa mmfuko huo Boniface Kanemba, huko Reading Uingereza hivi karibuni.
Watanzania kibao waishio Uingereza wamejitokeza kujiunga na Mfuko wa Hifazi ya Jamii (NSSF) baada ya kugundua kuwa shirika linajenga nyumba kwa ajili ya kuuzia wanachama wake kwa mikopo.
Baadhi ya Watanzania hao wameileza globu hii ya jamii kuwa wamekuwa wakipata hasara sana kwa kutuma fedha za ujenzi wa nyumba kwa ndugu zao, ambao huwa wanakula pesa au wanajenga nyumba chini ya kiwango kinachotakiwa.
Watanzania hao pia wameendelea kusisitiza kuwa huduma hiyo itawafanya nao waweze kuwa na pensheni yao kwani wapo nje ya nchi kwa kutafuta maisha ila hatimaye watarudi Tanzania baada ya kustaafu.
Pia, watanzania walio wengi wamefurahishwa na huduma ya Matibabu kwa wanafamilia pamoja na huduma za uzazi zinazotolewa na Shirika hilo.
Kwa maezezo zaidi kuhusu huduma hii wasiliana na:
Baadhi ya Watanzania hao wameileza globu hii ya jamii kuwa wamekuwa wakipata hasara sana kwa kutuma fedha za ujenzi wa nyumba kwa ndugu zao, ambao huwa wanakula pesa au wanajenga nyumba chini ya kiwango kinachotakiwa.
Watanzania hao pia wameendelea kusisitiza kuwa huduma hiyo itawafanya nao waweze kuwa na pensheni yao kwani wapo nje ya nchi kwa kutafuta maisha ila hatimaye watarudi Tanzania baada ya kustaafu.
Pia, watanzania walio wengi wamefurahishwa na huduma ya Matibabu kwa wanafamilia pamoja na huduma za uzazi zinazotolewa na Shirika hilo.
Kwa maezezo zaidi kuhusu huduma hii wasiliana na:
Director General,
National Social Security Fund,
Benjamin Mkapa Pensheni Towers 7Th Floor,
Azikiwe Street,
P.O.BOX 1322,
Dar es salaam,
Tanzania
TELEPHONE: +255 22 2163400 - 19.
HOTLINE: +255 756 140140 .
FAX: +255 22 2200037.
E-MAIL: dg@nssf.or.tz
P.O.BOX 1322,
Dar es salaam,
Tanzania
TELEPHONE: +255 22 2163400 - 19.
HOTLINE: +255 756 140140 .
FAX: +255 22 2200037.
E-MAIL: dg@nssf.or.tz


hizo hati zinatolewa nyumbani kwa mtu?
ReplyDeleteBig Up NSSF. Huu ndio ubunifu unaotakiwa.
ReplyDeleteKaka michuzi unaweza kutuulizia kama watakuja USA pia au ni U.K tu?
ReplyDeleteanon wa 1
ReplyDeletena mimi nashangaa maana hayo mazingira yamekaa kinyumbani nyumbani.
Ndiyo mazingira ya biashara za bima na kununua dhamana(bonds, shares)n.k yanavyofanyika huku ulaya na marekani.
ReplyDeleteUkivutiwa na bima,shares au bonds huonani uso kwa uso na mtu, una jaza fomu ulizoletewa kwa njia ya barua kupitia posta unajaza na makato yanaanza shapu shapu. Na statement ya makato na michango yako utapatiwa kwa posta, huoni sura ya mtu wala nini.
Hivyo huyo afisa wa NSSF amekwenda mbele zaidi kumjali mteja kwa kuonana nae macho kwa macho, maana makampuni na wafanyakazi wa Bongo hawaaminiki, lazima umwone staff wa bima au benki(CRDB Tembo/VIZA card) ili mambo yakienda mrama unajua utamshika nani shati.
hayo makochi mie mh! na hivyo vitambaa vitoeeee....kama tuko njombe
ReplyDeleteOh no! Ni wale walikuja huku wakasema watatujengea nyumba na cost zake ziwe dola laki moja na mtu unatakiwa ulipe kwa miaka mitatu au hao ni wengine? wale walidhania sijui tunachuma hela huku au kuchota mtoni tu. Hata kama ndugu zangu wanaiba hiyo hela lakini 3 br house kwa laki moja bongo karibu na bagamoyo!!!!!! Heri ni tajirishe ukoo wangu sijui hizo nyumba zinakuja na satellite
ReplyDeleteDr Dau umefanya la maana njoo na USA basi, hayo ndio mambo ya kisasa.
ReplyDeleteBig Up Dr Dau
Hongera Dr. Dau na kikosi chako kizima cha NSSF kwa kujali watanzania.Ila wenzangu na mie waliozoea kula hela za ndugu zao na kuwadanganya kwa kuwapelekea picha za nyumba za watu kuonyesha progress wameliwa, watafute kazi za kufanya sasa maana bwawa limeingia ruba!
ReplyDeletehawa ni wasanii tu kama benard chisumo huyo anyejiita agent wa crdb bank tena kama bahat naona anauza gar ok achana na hiyo walikuwa wanapita kila nyumba hapa reading wakisema unaweza kufungua account ya crdb na ukkiingiza pesa hapa loyds zinaingia moja kwa moja yote sawa lakin yule dada akachukua kila kichwa 10pounds kibongobongo karib 20elf tena nammind sana yule dada lakin mpaka leo cha ajab watu wameletewa acc no lakin card hazionekan mwaka wa 2 sasa kwa hiyo tumechoka na utapeli
ReplyDeletewaongo tu hao mambo yanafanyika nyumban kama kina benard chisumo na yule dada msanii wa crdb bank aliyetoka bongo wasituzingue hao
ReplyDelete