Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Amani Abeid Karume akipokea zawadi kutoka kwa Waziri Mkuu wa Kenya, Mhe. Raila Amolo Odinga jana tarehe 25 Septemba, 2008. Mhe. Odinga alimtembelea Mhe. Rais Karume Ikulu ya zamani mjini Zanzibar.
Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha akimkaribisha Waziri Mkuu wa Kenya, Mhe Raila Amolo Odinga muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar jana kwa ziara ya siku moja. Picha na Assah Mwambene wa Mambo ya Nje

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. a.alaikum michuzi na ndugu wana blogi, nimeona bro michuzi umeandika uwanja wa kimataifa wa zanzibar lakini kiukweli haswa huo uwanja haujafikia kiwango cha kupewa jina hilo,naomba viongozi msikie kilio chetu wazanzibari tunanyanyasika sana iweje leo ndugu zetu wa bara wana uwanja wa kimataifa dont get me wrong sisemi kama wasiwe nao ila tunasikitishwa kuona ikiwa sisi ni kama ndugu ilikuwa na sisi tufikiriwe kujengewa kiwanja cha kisasa kitakachoweza kutuwa ndege kubwa kubwa,natumai bro michuzi utazifikisha hizi salamu kwa waheshimiwa viongozi wa ngazi za juu asante.

    ReplyDelete
  2. nyie gombanane kwa siaisa tu , msijenge uwnaja wa ndege wala wa njiwa ...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...