Na Mwandishi Maalum, Washington D.C., Marekani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa siyo kila kiongozi wala kila mtumishi wa umma ni mwizi wala mla rushwa, hata kama ni kweli kuwa, kwa kiasi fulani, bado lipo tatizo la rushwa katika nchi za Afrika.
Amesema kuwa tatizo la wale ambao wanachagua kutangaza kuwa Afrika inanuka rushwa, ni kwamba wanafanya jaribio la kupuuza mambo yote mazuri yanayotokea katika Afrika na kuishia katika kushikia bango rushwa tu.
“Tusijiweke katika hali ya kutengeneza mazingira ya kwamba kila jambo linaloendelea katika Afrika ni rushwa tu,” Rais Kikwete amewaambia wajumbe wa taasisi ya Foreign Policy Brain Trust ya Wabunge Wenye Asili ya Afrika mjini Washington, D.C.
Rais Kikwete alikuwa anajibu maswali ya wajumbe wa mkutano huo baada ya kuwa amemaliza kutoa hotuba-mada (keynote address) muhimu kwenye mkutano huo jana (Ijumaa, Septemba 26, 2008) katika Kituo cha Walter E Washington Centre. Alikuwa anatoa hotuba-mada iliyozungumza nini Afrika inatarajia kutoka kwa Rais mpya wa Marekani atakayeingia madarakani Januari 20, mwakani.
Rais Kikwete aliyewasili mjini Washington akitokea mjini New York juzi (Alhamisi, Septemba 25, 2008) usiku amewaambia wajumbe wa mkutano huo:
“Hatukatai kuwa ipo rushwa katika Afrika. Tunachosema ni kwamba jambo hilo linatiwa chumvi nyingi kupita kiasi. Ni kama vile iko rushwa katika inchi ya Bara letu na katika kila senti inayoingizwa Barani Afrika… kuna wezi kila mahali, siyo Afrika pekee.”
Amesema kuwa kama kuna rushwa katika fedha za misaada inayotolewa kwa Afrika, misaada inayodhibitiwa kwenye kila hatua na wafadhili wenyewe wanayoitoa, bado liko tatizo kubwa zaidi kuliko Waafrika kuwa wala rushwa.
“Hii ni fedha yenu, na mnataka kujenga barabara katika nchi yoyote ya Afrika, na mnatoa fedha yenu na kuisimamia nyie wenyewe, sasa kama inatokea rushwa katika fedha hiyo ya ujenzi wa barabara, basi lazima mjiulize ni mfuko upi hasa fedha hiyo imeingia,” amesisitiza Rais Kikwete.
Kuhusu Tanzania, Rais Kikwete amesema kuwa Serikali yake inapambana kweli kweli na changamoto hiyo ya rushwa kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Tanzania.
“Moja ya dalili za Serikali inayokula rushwa ni kushuka kwa mapato ya Serikali, ama Serikali kushindwa kukusanya mapato. Mapato yetu yamekuwa yanaongezeka kila mwaka tokea tulipoingia madarakani,” amesema Rais Kikwete na kuongeza huku akiwa anashangiliwa:
“Mapato ya Serikali yameongezeka kutoka sh trilioni tatu hadi kufikika trilioni saba kwa mwaka, kiasi cha kwamba katika mwaka huu wa fedha tunagharimia sisi wenyewe bila msaada wa yoyote bajeti yetu ya matumizi ya Serikali. Haijapata kutokea. Sisemi hakuna rushwa, lakini hili ni suala la nani anataka kusema na kutangaza jambo gani kuhusu wewe.”
“Kama mtu anasema mabaya tu kuhusu wewe, basi ni mabaya tu yatakayojulikana. Katika hali hiyo, mazuri yote yatawekwa pembeni ama kupuuzwa, na hivyo kujenga picha kama vile kinachoendelea katika Afrika ni rushwa tupu.”
Rais pia ametumia muda mwingi kuwaelezea wajumbe wa mkutano huo kuhusu jinsi Afrika ilivyopiga hatua, iwe katika demokrasia, ama katika utoaji wa huduma za kijamii, ama watu kujiongezea pato.
Amesifia uhusiano mzuri kati ya Tanzania na Marekani na kusema kuwa anatarajia kuwa rais ajaye wa Marekani ataongeza na kuimarisha zaidi uhusiano huo.
JK amesahau kumalizia kuwa kuongezeka kwa mapato ya nchi si hoja kama mapato hayo hayawafikii wanannchi na kuboresha huduma za jamii!Mfano mapato hayo yana maana gani kama hospitali hazina dawa, maji safi hakuna, walimu haba, madawati issue, umeme issue, ajira issue...!!!
ReplyDeleteHapo Kikwete unaanza kuchemsha ukisema hivyo ina maana gani? au ndo mambo ya kuwakumbatia mafisadi? issue hapa ni hatua gani unachukua juu yao na sio kujifananisha na rushwa za nchi nyingine zilizoendelea, jifunze hilo mzee tunataka hatua zichukuliwe kuwatia hatiani mafisadi si kujiuzulu tuu
ReplyDeleteBlaa Blaa Blaaa
ReplyDeleteYou are right Mr president but the problems is what have you done to make sure Tanzania becomes a free corruption zone.
ReplyDeleteMay be you're clean but how about all those scandalous EPA,Richmond not to mention all.Its a straight forward issue but you failed the country for not take any measure such as court action against all your friend and that why the western label all leaders a corrupts.
What happen if someone stole something and you dont report to the authority? for me all of you a thiefs that is the reason they said all African leader a corrupts.
You get the point Mr President? if your not then you're not Honest and that is the big problems of Most of African leaders to fail to differentiate between Fiction and non-fiction.
Cheers Mr President
Mjusi (as known Kenge)
London,East
Mjusi ninakuunga mkono. Lkakini ushauri kidogo, nje ya mada, hizi lugha za watu ukiwa huna uhakika nazo tumia hii ya kwetu. hata ukikosea wanasema ndicho kiswahili cha wasomi!!!!!
ReplyDelete