TUKIO JINGINE LA KIPEKEE LA MICHEZO TOKA CASTLE LAGER
*Castle Lager yaipa Klabu ya Gymkhana Sh. milioni 10
*Fedha ni kwa ajili ya kufanyia mashindano ya kimataifa
*Castle Lager yaendeleza michezo Tanzania
Dar es Salaam, September 24 2008: Castle Lager, bia bora barani Afrika, kwa mara nyingine tena inafanikisha mashindano ya kimataifa ya michezo hapa nchini.
Kama sehemu ya nia yake ya kuendeleza michezo katika ngazi za taifa na kimataifa, Castle Lager imetoa Sh. milioni 10 kwa Klabu ya Gymkhana ili kuiwezesha kukarabati na kuboresha viwanja vyake tayari kwa mashindano ya kimataifa ya kriketi. Mashindano hayo ambayo ni pamoja na Ligi ya Dunia Daraja la 4 ya Baraza la Kimataifa la Kriketi (ICC), Klabu Bingwa ya Kriketi Afrika Mashariki na Kombe la Afrika la kriketi yatafanyika kati ya Oktoba 2008 na Februari 2009.
Akiongea jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Castle Lager Mpeli Nsekela alisema, “Kwa mara nyingine tena Castle Lager inajivunia kuwa sehemu ya michezo nchini Tanzania. Udhamini huu kwa Klabu ya Gymkhana ni namna mojawapo ya bia yetu kutilia mkazo azma yetu ya kuona michezo inakuwa ya hali ya juu hapa nchini.
Kwa miaka mingi Klabu ya Gymkhana imekuwa ikiheshimiwa na kuenziwa na wapenzi wa michezo mbalimbali pamoja na wale wanaopenda kriketi.
Kutokana na kwamba kuna mashindano ya kimataifa yanayoanza hivi karibuni, Castle Lager imeona ni vyema kuwa sehemu ya historia ya Klabu hii kwa kuipatia Sh. milioni 10 kwa ajili ya ukarabati wa viwanja vyake.”
Udhamini wa Castle Lager wa Sh. milioni 10 kwa Klabu ya Gymkhana utaviwezesha viwanja vya klabu hiyo kuwa tayari kwa Ligi ya Dunia Daraja la 4 ya Baraza la Kimataifa la Kriketi (ICC) itakayoanza Oktoba 4 na kuzikutanisha Hong Kong, Visiwa vya Fiji, Italia, Afghanistani, Visiwa vya Jersey na wenyeji Tanzania.
Pamoja na Klabu ya Gymkhana, viwanja vingine vitakavyotumika ni Annadil Burhani – Upanga, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Ubungo na Leaders Club – Kinondoni.
Nsekela aliongeza kuwa timu zitaanza kuwasili nchini kuanzia Oktoba 2, 2008 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius K. Nyerere na kwamba zitakaa kwenye hoteli ya Golden Tulip. Mashindano hayo ni sehemu ya mchujo wa kupata washiriki wa Kombe la Dunia la ICC litakalofanyika barani Asia mwaka 2011.
Kufanyika kwa michuano ya kimataifa ya kriketi jijini Dar es Salaam ni ushahidi thabiti wa hatua kubwa Tanzania inazopiga kwenda mbele katika mchezo huo na kuhusika kwa Castle Lager katika mashindano haya inaifanya hii kuwa mara ya tatu kwa bia hiyo kufanikisha michuano ya kimataifa katika miezi ya hivi karibuni.
Mwezi Julai Castle Lager ilitumia kiasi cha Sh. milioni 80 kudhamini Kombe la Kagame, fedha ambazo zilitumika katika shughuli zote za maandalizi na uendeshaji wa mashindano hayo ambayo yalikutanisha pamoja timu toka Afrika Mashariki na Kati.
Fedha hizo pia zilitumika kwa ajili ya vifaa vya timu pamoja na kuzisaidia timu za nyumbani katika maandalizi ya kombe hilo.
Udhamini huu kwa mchezo wa kriketi unafuata udhamini mwingine wa Castle Lager kwa mashindano ya mashua ya Tanzacat yanayoendelea kwenye Klabu ya Mashua ya Dar es Salaam ambayo yalianza Septemba 11 na kumalizika Septemba 26 2008.
Castle Lager imetoa jumla ya Sh. milioni 7 kwa mashindano hayo na hivyo kufanya gharama ya udhamini wake kwa michezo mwaka huu kufikia Sh. milioni 100.
Castle Lager inatengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania.
Castle Lager inatengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania.
hivi jamani hii misaada mingine ni ya masharti au! hao jamaa wa kriketi wana fedha kibao halafu bado tunawapa mamilioni hivi watanzania tutaendelea lini? kwanini fedha hizo zisipewe wahitaji haswa kama vituo vya yatima kwa kusaidia elimu zao hadi vyuo vikuu? mi nahisi siyo bure kuna masharti fulani, tubadilike jamani. mdau UG
ReplyDeletenadhani huu ni udhamini wa kibiashara na si msaada
ReplyDelete