Rais Thabo Mbeki wa Afrika ya kusini amekubaliana na ushauri wa Chama chake cha African National Congress (ANC) kujiuzulu kwa manufaa ya kile kilichokaririwa kuwa "manufaa ya wa Afrika kusini" na kuepusha kura ya kutokuwa na imani naye. Mbeki ambaye amekuwa akishutumiwa kushinikiza kesi ya rushwa dhidi ya Makamu wa Rais a zamani wa nchi hiyo na M/kiti wa ANC Jacob Zuma ambayo ilitupiliwa mbali na Jaji wiki iliyopita na kusafisha njia kwa Zuma kugombea urais katika uchaguzi ujao.
Katibu mkuu wa ANC Gwede Mantashe amesema kuwa Kamati kuu ya chama ilikubaliana kumwambia Mbeki ajiuzulu kabla ya kipindi chake madarakani naye hakuonesha kushtushwa na alikubali kushiriki katika mkakati huo.
Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, Makamu wa Rais ndiye anayetegemea kuchukua nafasi yake, lakini Makamu wa Mbeki Bi. Phumzile Mlambo-Ngcuka naye ameonesha nia ya kujiuzulu jambo ambalo linaelekea kufanywa na mawziri wengine.
Waziri wa Fedha Trevor Manuel ambaye anaheshimika sana kwa ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo, ndiye anayeangaliwa na wengi kuchukua nafasi ya mpito kama Bwn Phumzile ataamua kujiuzulu.
Rais Mbeki ataendelea kukaimu madaraka mpaka mtu wa kushika nafasi yake atakapoteuliwa.
Kwa habari zaidi nenda
on_re_af/af_south_africa_mbeki.
Hata hivyo uamuzi wa kumfanya Rais ajiuzulu umeleta hisia tofauti nchini Afrika Kusini
endelea hapa.
the_parties/0,2172,177154,00.html)
vile vile chungulia hapa


Lucky Dube aliwaambia viongozi wa siasa ulimwenguni kuwa "be good to the people on your way up the ladder cause you'll need them on your way down. THAT'S THE WAY IT IS" Kama ni kweli kuwa aliweka mkono kwenye kesi ya Zuma ambaye alionekana kuelekea kumalizwa nayo kisisasa, sasa mambo yamegeuka. Wakati huu ambapo Zuma kashinda na jamaa angemhitaji, ndio ambapo anakosa wa kumshika. Itakuwa mbaya kwa hali ya Afrika Kusini, Demokrasia yake na uchumi wake ambvyo kwa ujumla vinafanya vema lakini ni vichanga. Lakini kafanya la maana kuliko kusubiri kung'olewa na Bunge.
ReplyDeleteKila la kheri katika maisha mapya Mzee.
Ya Mbeki na ANC yanainyemelea ChiChiM.
ReplyDeleteHaya yote yanatokea kwa sababu ya watu kuwa na uroho wa madaraka, wakijidai kuwa wanataka kuwafanyia kazi nzuri wananchi, ukweli si hivyo watu wanataka madaraka kwa ajili yao binafsi, nasi washabiki tunapelekwa kama upepo hata kama hatupati faidi ya ama moja kwa moja au ya kipitia pembeni kutokana na watu tunaowataka kuwa madarakani, wakati umefika kuwachagua watu halisi wanaotaka maendeleo kwa wote, si platform talking good then after getting what they wanted they forget the people once and for all, kwa mtazamo wangu JACOB ZUMA si kiongozi mzuri, mtu amelala na mtu ambaye anajuwa ana ukimwi na mtoto wa rafiki yake mkubwa wa umri wa binti yake, sisemi kwamba mtu mwenye ukimwi si mtu hasraili mapenzi la hasha, bali yeye kama public figure alipashwa kuonyesha responsibilty, and how to treat women respectively with diginity, swala la rushwa pia ni law technicality ndio imemtowa dismiss lakini alihusika iweje mshirika wake afungwe na yeye asihusike? ZUMA HAFAI ILI ILE MENTALITY YA KUWA ALIKUWA KAMANDA MKUU WA JESHI LA UKOMBOZI LA UMKOTO-WE-SIZWE ndiyo inayompa support ya watu wengi.
ReplyDeletenikumbusheni ndugu zangu huyu Jacob Zuma si ndie yule alieripotiwa kuwa alifanya mapenzi na mwanamke mwenye aids/hiv positive ilhali akijua hilo na alipoulizwa alisema kuwa "ndio lakini nilikogo baada ya tendo" au ni mimi ndie nimechanganya majina?
ReplyDeleteKusini kwishne kabeje nehinehi...pale Zim Changarai kibaraka chini linakuja hilo jamaa la kuoga maji Zuma duu wafwileee
ReplyDeleteNi ajabu na kweli. Mbeki alikuwa anamchukia sana Jacob Zuma, lakini akampa uwaziri wa mambo ya nje mtalaka wa Jacob Zuma.
ReplyDeleteNakubali kuwa viongozi wetu wengi wanakuwa na ubinafsi na kuwa corrupt,
ReplyDeletehata hivyo anasitahili sifa jinsi alivyo jiuzulu kwa hiyari kutofautisha na watu kama Banda na Mugabe ambao wanashikilia utawala hata ikawa uongozi wao hauna faida ye yote kwa wananchi. Mfano mzuri aliuanzisha Mzee Mandela, sijui kama tutaishi maisha marefu kuona viongozi wa nchi nzote za Afrika wataondoka kwa amani wakati utawala wao unapoisha. One day.
MBongo wa ATL- USA
mbinu za kudumisha wakoloni mamboleo ndio yeye mbinu za kisiasa hizo
ReplyDeleteHiyo ndio democrasia ya kweli amboyo bongo inabidi tuige.
ReplyDeleteNadhani Mwalimu angekuwa hai kama vile mze Mandela angewanyoosha haw aviongezi wa bongo.
We praise people in chosen words, Mbeki is a responsible man with responsibility conciousness, he helped Zimbabwe to be where it is today which is a point to celebrate, he is not like westerners who believed in ending violence by instigating another violence....he is a true African with a true and enviable wisdom...standing Zuma who is popular in S.A was not easy...he did all what he did not because somebody was forcing him but because if you see how Zuma behaves i'm sure you'll agree with me that he lacks substance.
ReplyDeleteLook what happened in Rwanda in 1994, the envasion of RPF from outside the country which caused what they call genocide, which is Kagame own making but who is being praised by westerners as not the genocide initiators (RPF) but baptised him as the who came to end it, but guys if African leaders like Mbeki who has seen alot in his life had to be given chance like what happened in Zimbabwe and Kenya...we could not be looking for scapegoat in Rwanda today where westerners are dictating us today by telling us who is good and who is bad in that Kagame own making war(invasion) and who is supported by them today.
Mbeki as human being who knows that, rule of law is pillar of all development is leaving today because of what he believe in which shows how responsible he is. He will be remembered as a Zimbabwe peace brocker among other things and a true African who never believed that violence is a solution.
Mbeki kafukuzwa na Mandela. Huo ndio ukweli kwani alikwisha enda kinyume na malengo ya ANC ya kumkomboa mweusi kiuchumi. Mbeki alikwisha ota mbawa akawa ahambiliki wala asikii la mtu. Ni kweli sikio la kufa alisikii dawa. Hili fundisho kama mafundisho mengine yaliyotokea Kenya na Zimbabwe. Pia ni kweli kabisa kama Julius angelikuwepo Nkapa asingefanya biashara Ikulu na JK asingekuwa na kigugumizi kuhusu EPA na Richmond.
ReplyDeleteIjapaokuwa mimi sijui vizuri historia ya maadili ya Zuma, tuna kila sababu ya kuwapongeza ANC kwa kuonyesha mfano mzuri wa utawala bora. Kama rais Mbeki ameboronga hakuna sababu ya kulindana. Anaondoka na mtu mwingine awe Zuma au ye yote anachukua nafasi yake. Na huyo Mbeki hakuwa mbishi. Huu ndio utawala bora. Kama Tanzania tungekuwa na utamaduni huu mimi ningependekeza kwa wana CCM kuwa wamwombe Rais JK kujiengua na kumhakikishia anarejeshewa mkoba wake wa zamani wa uwaziri wa mambo ya nchi za nje ambao anaonekana kuumudu zaidi ya urais. Urais si urahisi!!!!!
ReplyDeletehttp://www.anc.org.za/people/zumaj.html
ReplyDelete