mtangazaji wa kipindi cha michezo cha EATV patrick nyembela akitoa zawadi ya mpira kwa nahodha wa Albino Magic Team wakati wa mazoezi yao ocean road. mpira huo umetolewa na msamaria mwema ambaye hakutaka jina lake litajwe. patrick ametoa wito kwa wasamaria wema wengine kujitokeza kuisaidia timu hii ya aina yake kwa hali na mali kwani kama wanavyoonekana hawana vifaa vya michezo na pia hujinyima hata kula ili kusevu nauli ya kuhudhuria mazoezi kila siku.
patrick nyembela na nahodha wa Albino Magic Team wakitoa tano kwa msamaria aliyewapa zawadi ya mpira
tizi likiendelea kwa sana
hapo wakipata vifaa vya uhakika lazima maximo apate salamu siku moja
kikosi cha Albino Magic Team kikila pozi na mwalimu wao (kulia). azma kuu ya kuanzishwa kwa timu hii ambayo ni ya kwanza hapa nchini pengine na kwingineko duniani ni kupata fursa ya kujiweka fiti na pia kuhamasisha wananchi kuondokana na fikra potofu dhidi ya wadau albino, badala ya kukaa tu na kungoja misaada. kikosi hiki kesho kinatarajiwa kuungana na jumuiya ya albino katika maandamano ya kupinga unyanyasaji wa maalbino na pia kuishinikiza serikali ichukue hatua madhubuti na za kudumu dhidi ya unyanyapaa pamoja na mauaji ya kikatili ya albino.
maandamano hayo, yanayotarajiwa kupokewa na JK viwanja vya karimjee kesho asubuhi, yataanzia mnazi mmoja.


kaka michuzi, nimefurahishwa sana na team hivo ya Albino. Sasa kwa upande wangu mimi nipo ugalibuni nawezaje kutuma msaada wa kuwapa shavu, kama vile viatu maana naona hata wengine hapo hawana, hata chochote. Ninasubiri jibu lako
ReplyDeletepatrick nyembela asante sana wakilisha team hiyo mambo yanakuja mengine your sister[DC]
ReplyDeleteRafiki zangu,
ReplyDeletemnakumbuka zama zile tukienda Ocean Road Hospitali kuangalia sinema za James Bond (Live and Let Die) kwa ndugu zetu hawa?
Mnamkumbuka kiongozi wa hawa ndugu zetu Mzee Lameck?
Mnakumbuka tukijifunza kuvuta sigara pale kwenye kioski cha kibaiskeli nje ya vyumba vya kujifungulia kina mama? Mnakumbuka wale wazazi waliokuwa wanasaidiwa kujifungua na mama zetu barabarani Mtaa wa Luthuli?
Mnakumbuka vilio na kelele na za kina mama zetu wakati wa kujifungua?
Mnawakumbuka dada zetu mapacha tuliosoma nao Forodhani Sekondari na kusali nao kanisa la Mtakatifu Josefu?
Quo Vidas Tanzania? = Tanzania unaenda wapi?
Haven´t we learn from Mauaji ya Shinyanga? Mauaji na mateso ya kina Twiga Nindwa na Mazenghenhuka? Mauaji na mateso yaliowapeleka mahakamani na wauaji? Yaliowapeleka mahakamani na kuwafunga na kuwalazimisha kujiuzuru viongozi, mawaziri, mapolisi na maofisa upelelezi?
Kama historia haitukumbushi na kutufunza, nini kitatukumbusha na na kutufunza? Turejee ya Shinyanga ili yatupe njia mkabala ya kukabiliana na haya ya sasa. Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema na Upendo tuongoze katika njia zako. Amen.