Timu kamambe ya Bongo United itaelekea mjini Atlanta,ijumaa oct 24 tayari kwa mpambano wa mechi ya kirafiki na wahasimu wao Atlanta Tanzanite Fc,itakayochezwa jumamosi oct 25,mara ya mwisho timu hizo zilipopambana Bongo United waliibamiza Tanzanite 3-2.
katika mechi mbili ilizocheza za kujipima nguvu,ilizocheza oct 12 na Senegal,Bongo United iliibuka na ushindi wa 3-1.
magoli yaliofungwa na Seif,Shaban na Denis,wakati lile Senegal lilifungwa na mchezaji wao hatari wa timu hiyo Keita.na katika mechi nyingine waliocheza oct 19 Bongo United waliweza kuichakaza timu ya Malawi 4-0 timu ambayo ipo kwenye ligi,mabao ya Bongo United yalifungwa na Inno,Seif(2) na Owen.
Kikosi cha mauaji kitakachosafiri hiyo ijumaa chini ya kocha wao Rashid Lato,aliyewahi kuichezea ushirika Moshi,Small Simba na timu ya Taifa,makipa ni Dedy,Alawi,Lucas,mabbeki lemy,Evans,Beach boy,Adam ny,ray,Simon,Tobi,Marco,Mawenya,Vasco na Aris.Viungo ni Owen,Libe,Vicent,Hussein,Inno,Kheri,Dogo,Choteka na Yasin.mafoadi ni Dickson,Seif,Kendo,Denis,Shabani,Adam dc na Chichiba,wachzaji wote wako fiti tayari kufanya mauaji


Majungu mbona hatumsikii hapa, au yeye majungu yake kwa fc bongo ya helsinki tu?
ReplyDeleteKweli nimekubali Marekani mwisho, huwezi kufananisha na mansese ufini, wapika majungu wote wamesaluti.. tehe tehee ee
ReplyDeleteKAZI IPO BONGO NI SMBA UA YANGA JUMAMOSI HII, Mdosi wa yanga ndio kasha sema yanga ikifungwa tu anakatisha mkataba na ufadhili basi...tehe tehee watu tumbo joto.