meneja wa kilaji cha redds akionesha ratiba ya fainali za rafda 2008 kwa mama wa mitindo asia idarous (shoto) na mratibu wa fainali hizo irene kiwia wa beautiful tanzanie modelling agency pili (kulia) na mdau wa redds leo hoteli ya kempinski.


*Kupambwa na onyesho la mitindo ya wabunifu wa Kitanzania wanaochipukia
*Mshindi kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano la Afrika nchini Botswana
*Mbunifu wa shati la Mandela kuwa miongoni mwa majaji

Dar es Salaam Oktoba 20 2008:

Tuzo za ubunifu wa mitindo barani Afrika za Redd’s (RAFDA), shindano la aina yake la ubunifu lililofanyika nchini na kudhaminiwa na Redd’s, kinywaji maarufu kinachohusika na masuala ya mitindo kinachotengenezwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), hatimaye limefikia kilele chake.

Shindano hilo ambalo lilijumuisha washiriki toka mikoa mbalimbali nchini katika changamoto mahsusi ya ubunifu kwa nia ya kupata mshindi mmoja litamalizika Ijumaa Oktoba 24 2008 kwenye hoteli ya Kempinski Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo, Meneja wa Kinywaji cha Redd’s George Kavishe alisema, "Redd’s ilipopata wazo la kuanzisha RAFDA, tulikuwa na picha vichwani mwetu ya mbunifu wa mitindo wa Kitanzania aliye kijana, mwenye muamko na msukumo ambaye ataliwakilisha taifa kwenye jukwaa la kimataifa.
Ninasubiri kwa hamu fainali hizi kwa sababu najua kuna watu wengi waliofuatilia mchakato huu kwa karibu wenye nia ya kutaka kujua nani ataibuka mshindi. Ushiriki wa Redd’s katika shindano hili unaendelea kusimika sifa za kinywaji hiki ambazo kwa wengi zinafahamika vizuri."

Fainali hizo pia zitatoa burudani kwa watakaozishuhudia kupitia kwa mwanamuziki Banana Zorro na B Band, nyota ambaye amekuwa akikoga nyoyo za wapenzi wengi wa muziki kwa vibao kama "Nzela", ambacho kimekuwa kikipigwa nchi nzima kwa miezi kadhaa sasa na bado kinaendelea kupendwa na wengi.

Pia kutakuwepo na onyesho la mitindo litakalojumuisha wabunifu kadhaa akiwemo Farouk Abdela atakayeonyesha mavazi aliyoyapa jina la "Under the Veil". Wabunifu wengine ni Masoud Kipanya, Monica toka Morogoro na Criss Designs wa Mwanza.

Kavishe alithibitisha zaidi kuwa miongoni mwa walimbwende watakaoonyesha mitindo ya ubunifu ni mlimbwende wa Kimasai Neshino aliyeshiriki shindano la Face of Africa ambaye kwa sasa anasoma na kufanya kazi wilayani Karatu.
Miongoni mwa majaji atakuwepo mbunifu Sonwabile Ndamase toka Afrika Kusini aliyejipatia umaarufu kwa kubuni shati maarufu la maua analopendelea kuva Nelson Mandela.

Fainali hizo zitatoa mshindi atakayeiwakilisha Tanzania kwenye shindano la RAFDA la Afrika litakalofanyika nchini Botswana. Tiketi kwa ajili ya fainali hizo zinauzwa Sh.20,000/- na zinapatikana kwenye ofisi za Beautiful Tanzanie Agency – Hugo House, Renzo Salon – Mikocheni, Aqua Video Library na duka la vitabu la Novel Idea – Shoppers Plaza, Mlimani City, The Slip Way, Sea Cliff Village na Steers – Samora Avenue.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. YAANI KUNA WATU WANA GUNDU
    HATA PICHA ZAO ZIWEKWE VIPI HUKU NO COMMENTS KHA!
    WADAU HEBU ANGALIENI HII PICHA NA MTOE COMMENTS ZENU

    ReplyDelete
  2. MVUTOOOOOOOOOOOO, MVUTO MDAU
    ngoma hazina mvuto, no comment.
    kuwa na hela, au kazi nzuri sio kwamba ndio uta catch watu, just mvuto mannnnnnn.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...