Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi,Maalbino ,wakati alipopokea maandamano ya kulaanani ukatili na mauaji ya maalbini,yaliyofanyika katika viwanja vya ukumbe wa Karimjee jumapili asubuhi.
albino na wanaharakati wa kupinga ukatili dhidi ya albino wakiandamana

Mbunge wa kuteuliwa anayewakilisha maalbino, Al Shaimaa John Kwegyir akiteta jambo na JK wakati wa hafla ya kuzindua na kuichangia taasisi ya Goodhope Star Foundation ambayo itatetea na kutoa huduma kwa maalbino nchini,iliyofanyika katika hoteli ya Movenpick. Katika harambee hiyo iliyoendeshwa na JK zaidi ya shilingi 16.3/m zilikusanywa.Rais Kikwete alitoa jumla ya shilingi milioni mbili na nusu 2.5/m kama mchango wake kwa taasisi hiyo.
ujumbe kwenye mabango unaeleza hisia za wanaharakati hawa na albino wakiwa maandamanoni


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. MUNGU IBARIKI TANZANIA IONDOKANE NA BALAA HILI!!

    ReplyDelete
  2. Mmh, Kaka Michuzi,
    Nimevumilia nimeshindwa naona hata wadau wengine hawaulizi sijui unabania maoni? Kwani Kaka KICHAA UTAMU KAPATWA NA NINI? Mbona hapatikaniki?

    ReplyDelete
  3. Hii ni aibu kubwa kwa Tanzania,mambo ya ajabu ajabu mara utasikia watu wanawauwa wazee kwa imani za kishirikina.Habari hizi zimetapakaa kwenye vyombo vyote duniani,utafikiri tunaisha enzi za ujima.

    ReplyDelete
  4. Haya maandamano yangefanyika kanda ya ziwa yangekuwa na maana zaidi kwani kule ndiko haswaa tatizo lilipo kubwa kwa sababu watu wengi wanaofanya vitendo hivi wengi ni wachimbaji wadogo wadogo(Wachoji) na wavuvi wa samaki ziwa Vicotria(Ninavyosikia).Lakini bado hatujachelewa,serikali/jumuiya ziandae maandamano menginr mikoani.Hili janga tutalipiga stop kwa mwamko na elimu kwa raia tu.Mungu tuondolee jinamizi hili.

    ReplyDelete
  5. RAISI ANGEWAOMBA MSAMAHA MAALBINO KWA SERIKALI KULIFUMBIA MACHO HILI TATIZO KWA MUDA MREFU. LAKINI TUJIULIZE, MAALBINO WASINGEANDAA MAANDAMANO, RAISI ANGEYASEMA ALIYOYASEMA JUZI? KWANINI MIEZI YOTE HII ALISHINDWA KUKEMEA HILI TATIZO? INAELEKEA SERIKALI ILIONA KUWA HAIHUSIKI NA TATIZO HILO NI JUU YA MAALBINO WENYEWE KULISHUGHULIKIA, HII NI AIBU KWA TAIFA LINALOJIFANYWA HALINA UNYANYAPAA KWA WALEMAVU.

    ReplyDelete
  6. Mdau wa October 21, 2008 8:12 AM

    Ni kweli ingekuwa bora kama serikali ingeliona na kulishughulikia hili tatizo mapema.

    Lakini kama unavyojua serikali ina matatizo meengi sana ya kushughulikia kwa hiyo kama hupigi kelele unaweza kusahaulika

    ReplyDelete
  7. MDAU OCT.21. 2008 11.01 AM KELELE KUHUSU MAUAJI ZILIANZA MAPEMA SANA MAUAJI YALIPOANZA TU, MBONA VIBAKA HAWAPIGI KELELE KUHUSU MAUAJI YAO LAKINI SERIKALI INAWAPIGIA KELELE? UKWELI UTABAKI PALEPALE HAWAJATENDEWA HAKI NA SERIKALI ILIYOWEZA KUPELEKA MAMIA YA ASKARI TARIME KUIHAMI CCM KWA KISINGIZIO CHA KUDHIBITI WIZI WA MIFUGO NA MAPIGANO YA KIKABILA LAKINI MARA BAADA YA UCHAGUZI ASKARI HAO WAKAYEYUKA WAKIZITUPA HOVYO HATI WALIZOPEWA KUPIGIA KURA WATOTO WAKAZIGEUZA KARATA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...