Leo ni siku ya kuzaliwa ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anatimiza umri wa miaka 58.
Rais Kikwete alizaliwa Oktoba 7, 1950 katika Kijiji cha Msoga, Kata ya Lugoba Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Ni mmoja wa watoto wa Khalfan Kikwete na Asha Binti Jumbe (wote ni marehemu).
Baba yake mzazi alifariki dunia Agosti 8, 1998, Kinondoni Dar es Salaam; mama yake aliaga dunia Juni mosi, 1999. Mama mzazi wa Rais Kikwete alikuwa ni miongoni mwa wake watano wa Mzee Khalfan aliyekuwa na watoto watatu.
Rais Kikwete ni mwanawe wa pili, akitanguliwa na dada yake mkubwa, Zena (marehemu), na mdogo wake, Mohamed Mrisho Kikwete.
Kabla ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Kikwete alikuwa Waziri kwa miaka 17 ikiwamo miaka 10 ya uwaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aligombea urais katika uchaguzi Mkuu uliopita akashinda, na Desemba 21, 2005 aliapishwa kuwa Rais wa nne wa Tanzania.
Kwa mujibu wa kitabu cha ‘Kikwete, Safari ya Ikulu,’ Rais Kikwete ana watoto saba; wawili kati ya hao, Ridhiwani na Salama alizaa na mke wake wa kwanza, Aziza Sabuni (marehemu); watano amezaa na mkewe wa sasa, Salma ambao ni Miraji, Ally, Khalfan, Mwanaisha na Rashid ‘Chodo’.
Rais Kikwete alizaliwa Oktoba 7, 1950 katika Kijiji cha Msoga, Kata ya Lugoba Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Ni mmoja wa watoto wa Khalfan Kikwete na Asha Binti Jumbe (wote ni marehemu).
Alizaliwa akiitwa Jakaya Khalfan Mrisho Kikwete, na kukua katika familia ya viongozi. Babu yake alikuwa Chifu; baba yake alikuwa kiongozi wa serikali; yeye alianzia katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Baba yake mzazi alifariki dunia Agosti 8, 1998, Kinondoni Dar es Salaam; mama yake aliaga dunia Juni mosi, 1999. Mama mzazi wa Rais Kikwete alikuwa ni miongoni mwa wake watano wa Mzee Khalfan aliyekuwa na watoto watatu.
Rais Kikwete ni mwanawe wa pili, akitanguliwa na dada yake mkubwa, Zena (marehemu), na mdogo wake, Mohamed Mrisho Kikwete.
Kabla ya kuwania urais kwa tiketi ya CCM mwaka 2005, Kikwete alikuwa Waziri kwa miaka 17 ikiwamo miaka 10 ya uwaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aligombea urais katika uchaguzi Mkuu uliopita akashinda, na Desemba 21, 2005 aliapishwa kuwa Rais wa nne wa Tanzania.
Kwa mujibu wa kitabu cha ‘Kikwete, Safari ya Ikulu,’ Rais Kikwete ana watoto saba; wawili kati ya hao, Ridhiwani na Salama alizaa na mke wake wa kwanza, Aziza Sabuni (marehemu); watano amezaa na mkewe wa sasa, Salma ambao ni Miraji, Ally, Khalfan, Mwanaisha na Rashid ‘Chodo’.
Tunamshukuru Mungu kwa kila jambo.
ReplyDeleteMungu azidishie maisha marefu ya amani na atuongoze vizuri
Happy birthday,kiongozi wetu. allah akupe afya njema na nguvu ya kuendeleza taifa letu.dalili njema za uongozi mzuri zimeshazaa matunda.nasi sote tumpe support
ReplyDeleteHappy Birthday Mr. Prezidaaa!!
ReplyDeleteNakutakia maisha marefu japo hutaki kuwashugulikia wahujumu uchumi wetu sie wadanganyika.
"...nikitiza nyuma umri unaniaandamaa lkn bado sijafanya kitu cha maana"
Sir Wambura
St Lousina cath.
mbona haujamtaja yule mtoto waliyemuadopti anaitwa mohamed
ReplyDeleteHappy Birthday Mkuu wa Nchi. Miaka iwe mingi zaidi, yenye neema kwako, familia na Taifa letu
ReplyDeleteIla nimegundua kumbe Bi Salma nae kama Sarah Palin vile
Kwanza namtakia Birth Day njema
ReplyDeletePili kuna maneno tunayasikia sikia huko mtaani lakini tunashindwa kujua ukweli wake
Mfano:
1. Je anauhusika vipi na klabu ya yanga, kwani tuliomchagua ni wananchi wote wakiwemo na mashabiki wa Simba sasa tunaposikia maneno maneno ya kwamba huenda anatumia madaraka yake kwa manufaa ya timu moja kati ya hizi mbili kwa kweli hatuelewi
2. EPA EPA EPA ....tunakubali alieleza eleza pale bungeni lakini mbona kama mmmhhhh ...!!!! naona kama maelezo sijui hayajakuwa bayana au sijui mimi ndio sikuelewa
Kwa sasa nina hayo mawili tu ... (mengine nayahifadhi kwa sasa)
Happy Birthday x2
ReplyDelete2 you mr jk, kumbe bado mdogo jamani!! tunakutakia maisha marefu,uongozi bora na hekima tele.
kilichonifanya nikupende ni hiki
1. ulipozichukuwa zile nyumba walizouziana wale viongozi wasio na uchungu na nchi na kuzirudishia serikari hapo nimejuwa kabisa unastahili kuongoza nchi
naleo nimepata nafasi ya kusema asante na hongera wewe nakukubali upo madarakani kwa umma!!
Happy Birth Day !!!!
ReplyDeleteTumekuwa tukishuhudia jirani zetu Burundi, Rwanda, Kenya n.k wakiwa katika migogoro mbalimbali inayopelekea hata kuuwana wao kwa wao kutokana na matatizo ya ukabila
Tunashukuru hapa kwetu matatizo hayo hayajafikia kiwango hicho ...ilaaaaaaa ...!!!!!!
Kuna tatizo moja ambalo linachukuliwa kimzahamzaha na linakua taratibuuuuu .....!!!! chonde chonde lisije likatufikisha kusikotakiwa .... na tatizo hilo niiiiiiii !!!!!!!
"Usimba na Uyanga"
ooooohhhhhhh ..... !!!!!!!!!
Happy Birthday that is what I can say Today, No comment
ReplyDeleteKenge
Happy Birthday Mr President. May GOD be with ypu today and Years ahead. Have your happiest borthday ever1 Enjoy your day to the fullest. Be Blessed our President.
ReplyDeleteOnce again Happy Birthday!
Happy birth day, Your Excellency rais wetu mpendwa.Mheshimiwa Rais pale baraza la mitihani unaonaje ukapatupia jicho.Kuna bahadhi ya wiongozi wa baraza la mitihani(NECTA) wanahujumu taifa kwa kuuza/kuvujisha mitihani na kuliingiza taifa katika hasara ya kutunga mitihani mipya ikiwemo kushusha kiwango cha elimu nchi katika kipindi hiki ambacho dunia inakwenda kwa kasi sana.Nakutakia afya njema.
ReplyDeleteHongera sana Mhe. Rais wetu JK. Nakupongeza sana kwa kufikisha umri huo, at 58 and still looking young. Mwenyezi Mungu akuzidishie kila la kheri na neema.
ReplyDeleteposted by Msoga
happy birthday J.K; Mungu akupe maisha marefu. wakati kama huu ndio tunatakiwa kumsifia mh kwa yote mazuri aliyofanya na kumshauri pale alipoteleza. mimi nakupa full ufagio!
ReplyDeletezambia wanakufagilia sana mno hasa kwa hotuba yako yenye busara uliyoitoa siku ya msiba wa rais wao!
dumisha mazuri mzee; nakutakia maisha mema!
Duh ... Hivi kwanini Perfomance ya Taifa Stars imekuwa sio nzuri kuliko ilivyotegemewa ?
ReplyDeleteDuh ... Hivi ni kiasi gani cha pesa kimetumika kwa safari za nje ?
Duh ... Hivi kwanini bei ya mafuta Tanzania ni kubwa kuliko nchi jirani zinazotuzunguka
Duh ... Hivi kwanini pamoja na kuhutubia bungeni kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo suala la EPA lakini mbona bado vuguvugu la EPA halijakwisha au kutulia ?
Duh ... Hivi kwanini tishio la migomo ya wafanyakazi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku
Duh ... Hivi kwanini " Zanzibar Political crisis imekuwa issue kuliko hapo awali" ?
Duh ... Hivi kwanini mafisadi wamekuwa wengi kipindi hiki cha awamu ya nne ?
Let the game begin
Let us follow what ANC did.
Happy birthday
Naomba niungane na watu wengine katika kukutakia siku njema ya leo ikiwa ndiyo tarehe yako uliyo zaliwa. Mengi umefanya tangu ulipoanza kulitumikia taifa hili na mengi zaidi na mazuri umeyafanya tangu ulipoingia madarakani. Mimi binafsi nakutakia maisha mema na yaliyo marefu ili uendelee kuitumika nchi yetu. Pamoja na hayo ningeomba kutumia siku ya leo kukumbusha ingawa najua hujasahau ile ahadi yako uliyoitoa baada ya kuapishwa kuwa raisi wa tanzania. Nakumbuka ulisema ''Nitakapo maliza muda wangu wa uraisi NATAKA kukumbukwa kwa kuwatoa wananchi katika janga la umasikini walilonao'', kwa maana nyingine ukumbukwe kwa kuwuwapatia maisha bora watanzania. Kama nimenukuu vibaya nisamehe lakini ujumbe unaamaanisha hivyo. Ili kufika katika lengo hilo, nakuombea kwa mungu akupe moyo wa ujasiri ili usiwaonee haya mafisadi kwani hawa ni sawa na magaidi wa uchumi wetu. Tumia siku ya leo kufikiria malengo yako uliyojiwekea ktk kuutumikia umma wa watanzania yamefikia wapi.
ReplyDeleteHAPPY BIRTH DAY JAKAYA MRISHO KIKWETE.
Happy birthday Mr President!
ReplyDeleteNow do us all a favor, Have the guy arrested and charged for stealing millions with his phony Richmond scam! This brings a lot of pain to even think of as a Tanzanian.
Thanx.
Mtanzania in USA.
Happy Birthday Mr President
ReplyDeleteNakutakia heri na baraka katika siku yako ya kuzaliwa
HAPPY BIRTHDAY Mr. President, Inshaallah M.Mungu atakujaalia kila la kheir leo, kesho na mtondogoo, Utuongoze kwa salama na amani kwa kipindi chote utakacho jaaliwa, akupe kinai ya dunia ili nawe usiwe fisadi, akujaalie ucha Mungu na umri mrefu. Amiin.
ReplyDeleteMichuzi,
ReplyDeleteMarehemu ni AZIZA SABURI (R.I.P)
na siyo AZIZA "SABUNI".
many happy returns Mr President..God bless!
ReplyDeleteHappy Birthday Mr President!!
ReplyDeleteBaada ya pongeti za birthday nakupongeza kwa dhati kabisa kwa utendaji wako wa kazi, usiku, mchana, sikukuu na siku za mapumziko wewe unachapa kazi tu baba, wanazungumzia au kujifanya kukupangia wewe namna ya kufanya kazi, au usafiri lini ndani au nje ya nchi wanaonyesha jinsi walivyo na ufinyu wa akili. Hawakumbuki kama umekuwa foreign affairs minister for 10 years, you have seen the whole world during the 10 years as foreign affairs minister, you made thousands of friends presidents and senior ministers/citizens, sasa yote unayoyafanya sasa ukiwa rais ni kwa manufaa ya watanzania wote.Umetumikia Tanzania tangu utoto wako dhat means you have touched every district of this country during your youth age, sasa unayoyafanya ni kwa manufaa ya taifa hili. Wanaouliza Rais anasafiri sana naamini kabisa hawajawahi kupanda ndege wakaona uchovu wa safari ndefu nadni ya ndege unavyokuwa. Baba chapa kazi wanaosema tuwasikilize na lakini haiwezekani kutenda kama wanavyofikiri ama wanavyotaka wao, yao ni maoni zaidi yatasikilizwa na kufanyiwa pale maoni yanapoonekana kuwa ya msingi!!
MWENYENZI MUNGU AKUJALIE AFYA, NGUVU, HEKIMA NA BUSARA KATIKA KAZI YAKO YA KULIJENGA TAIFA NA KUWATUMIKIA WATANZANIA.
Happy Birthday your excellency Mr. President of the United Republic of Tanzania.
ReplyDelete1. May God protect you from all harmful and evil intentions.
2. May God rewards you with more wisdom so that you lead your people wisely.
3.May God give you strength and courage to lead your country to a better future.
4. May God protect your country from all natural disaster and calamities
I wish you a happy birthday and many happy returns, may you blows a 100 candles.
Happy Birthday uncle!, Mr President!
ReplyDeleteMay Allah bless you, amen!
Nuru, uk
EPI BATHADAI TU YUU MISTA PREZIDENTI
ReplyDeleteHappy Bdai Mr. president. still Looking GOOD.
ReplyDeleteI WISH UTENDAJI WA KAZI WA RAIS KIKWETE UNGEKUWA UNAENDANA NA PERSONALITY YAKE. TUNGEKUWA MBALI SANA. OHHH..I ONLY WISHED!
ReplyDeleteHAPPY BDAY MR. PRESIDENT!
Anon wa October 07, 2008 4:57 PM...good questions!
ReplyDeleteLakini nadhani hilo la mafisadi kuwa wengi zaidi katika awamu halina evidence. Mimi nadhani ni kuwa ule mfuniko mkubwa umefunuliwa na sasa wananchi wanaona vitu kwa uwazi zaidi. Its a shame ile awamu ya ukweli na uwazi iliyopita haikuwa na ukweli wowote na uwazi. Kama mnakumbuka nadhani amiri wa enzi zile alishasema "..achane sifa za kike" or something along that line wakati watu wanauliza uliza maswali.
Mimi naona kumekuwa na uwazi zaidi katika awamu ya JK japo ukweli bado unatukwepa kwepa.
Many happy returns JK
mtoto
On this August Ocassion,every Tanzanian should reflect back on his personal Balance Sheet and his Net Worth and revisit the deree of crushing poverty among our rural compatriots and synthesise the economics of balance an under Dollar daily household income to make ends meet,AND BY THE SAME PERCENTAGE INCREASE WISH OUR EXSTINGUISHED PRESIDENT A HAPPY BIRTHDAY AND ETERNAL LIFE!
ReplyDeleteHizo ni salamu zangu kwako eeeeeh eeeehhh
ReplyDeleteAngalia mlipuko wa bei ulivyo juu maradufu kuliko mwenzio wa Masasi
Angalia gharama za maisha ya Mtanzania zilivyopanda
Ulizungumza vizuri sana siku ulipohutubia Bunge kwa mara ya kwanza kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lakini kumbe changa la macho
Hizo ni salamu zangu kwako eeehhh eeehhhh!!!
Sikufundishi kazi kaka ....
Mwenzio aliitwa kifimbo, akafuata ruksa, halafu "This country is very poor"
Unajua unaitwa nani hivi sasa ..?
Hizo ni salamu zangu kwako eeeehhh
Sasa nimeng'amua kuwa Mwalimu hakumaanisha hujawa tayari kiumri mwaka uleeee kumbe kumbe alihisi maji ni marefu haya
unilete viatu ukienda kwa Bush tena
wawekezaji watakujaje ikiwa miundo mbinu duni ... aje kuwekeza na umeme akuwekee, barabara akujengee inaingia akilini kweli ?
Tutengenezee miundo mbinu kwanza ili kiwe kivutio ndipo tuanze kualika wawekezaji
Hizo ni salamu zangu kwakoooo eeehhh eeehhh
Ulinishanga uliposema, nakunukuu
..." Tunapambana na ukimwi ili watanzania wasife kwa ukimwi ...eeh ikiwa basi kifo kitatokea basi kiwe labda ni malaria auuu...."
Nikacheka sana yaani wasife kwa ukimwi lakini wafe kwa maradhi mengine ...ha ha ha ha
Wewe kweli ni prezidaaa
Hizo ni salamu zango kwakoooo eeeeehhhhh !!!!!!! x 4
Happy birth day