Mwanamuziki Kahanga Dekula Vumbi anayefanya shughuli zake za kimuziki nchini Sweden katika klabu ya kimataifa ya Fashing Jazz Club amerejea bongo kuja kuwashika upya mashabiki wake wote popote walipo.
Vumbi, ambaye anatisha katika kukung'uta gitaa la solo, amesema amekuja kuzindua Albam yake ya 'Rumaliza' (kitu cha mwisho Baabkubwa) na atashirikiana na wanamuziki nyota kibao katika onesho litalofanyika kesho walo la maafisa wa polisi la ostabei, dar.
Amewataja wanamuziki wataompa taffu na ambao alishawahi kupiga nao muziki katika bendi tofauti enzi hizo kuwa ni mafumu Bilali Bombenga, Kanku Kelly, King Mallu, Tshimanga Kalala Asosa 'mtoto mzuri', Issa Nundu na wengine wengi.



Mtengeneze na video/dvd ya hiyo zingzong ya wakongwe ktk Bwalo la oysterbay n.k halafu tunataka haraka tuwaone ktk YOUTUBE.
ReplyDeleteHilo zoezi la video/dvd sio kubwa wahamashishe pia na King Kiki, Kasaloo n.k wawepo, Dekule wewe ni mzoefu wa sayansi na technology.
Maquiz na Safari sound za wakati huo, tunasikia ktk audio tu kwenye www.nukta77.com,www.bongoradio.com,
www.eastafricantube.com n.k sasa tunataka tuwaone ktk video pia.
Inatia moyo sana kuona wanamuziki wetu wakikumbukana,bado wana ushirikiano wa pamoja,hakika ni jambo la kutukuzwa sana!Huo ndiyo Utanzania halisi.Utanzania ni kama Upupu.Ukisha kuvaa mwilini au kugusana nao ni vigumu sana kuuondosha kabisa kabisa!Ukarimu,upendo,ushirikiano na mshikamano katika shida na furaha ni moja ya tunu za utamaduni wa kitanzania!Hata utoke Congo DRC au Afrika ya Kusini au Namibia au Kenya na Uganda au Rwanda na Burundi lakini ukisha gusana au kuuvaa Utanzania kamwe hautakutoka kimawazo,kitabia hata kifikra na kimatendo!Kuna Mpiga Solo mwingine mahiri sana Kawelee Mutimwana alishapiga na Bendi nyingi za hapa DSM pamoja na TANCUT ALAMSI ORCHESTRE YA IRINGA,mara ya mwisho nilisikia anapiga muziki wake katika Jiji la London!Siyo mbaya sana ikiwa na yeye siku moja akikumbuka kurudi hapa nyumbani DSM kuja kukumbushia zile za zamani na kupata hewa mpya ya mawazo mapya ya kuanzia tena huko London!Hata vijana wengine hapa nyumbani watapata nafasi ya kujifunza jinsi ya kuzama katika Muziki wa Kimataifa kwa faida ya nchi yetu na bara zima la Afrika.Mwisho wa yote sote tuna kazi moja ya kuendeleza Utamaduni wa Afrika!Tunasubiri kwa hamu siku ya siku ambayo hata yule Gwiji wa Solo la BID SOUNDO Nguza Viking na Pappi Kocha na Nguguze watakapo toka jela na kurejea maisha yao ya uraiani na kuendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania katika jukwaa la kimataifa la Utamaduni wa Afrika!Mungu awabariki nyote!Binadamu aliumbwa.Na sote ni dhaifu mbele ya Mungu.Lakini sisi sote ni Watoto wa Baba Mmoja,Mwenyezi Mungu Muumba wa Vyote!Hakimu ni Mungu peke yake!
ReplyDeleteKawele Mutimwana a.k.a Fingerprints makao yake kimuziki jijini london ni Club Afrique(Jesse Malongo) East London. Kikosi chake ni mchanganyiko wa wacongo na watanzania.
ReplyDeleteHapo kuna magwiji wengi wa muziki akiwemo mpiga saxaphone maarafu toka enzi za Jamhuri Jazz jina Rama na pia kina Moses waliokuwa kundi maarufu la Muungano Group Vijana Social Club DSM.
Kwa sasa Kawelee Mutimwana anatamba na CD maarufu kwa jina la 'Alama za Vidole' na bendi yake ya No Tshuna Tsha yenye nyimbo kama 'kwenu ni kwenu tu', 'Adam na Eve' kwa lugha ya kiswahili. Recorded at K Music Production
Butamu, Butamu, angalia Bongo hiyo shemeji yangu, usijiwachie tu.
ReplyDeleteSasa Vumbi ndiyo yupi hapo?.Balozi uandishi wako una walakini.Unafikiri kila mtu anawajua hao jamaa.
ReplyDeleteMdau , Washington Dc.
Jamani spaghetti Gullmarsplan pale stockholm UPO??????
ReplyDeleteKama alivyo shauri mpenzi mmoja wa miziki ya bakongotanzanie au bakulutu mimi pia naungana naye kuwashauri hawa ndugu zangu kina King Kiki,Assossa,(Nguzza Viking),Dekula Vumbi,Kanku Kelly,Mafumu Bilali Bombenga,Kyanga Kasaloo,na wakongwe wote waliokuwamo ndani ya Marquies,Safari Sound,DeLa Capitalle,BomoaBomoa,na nyinginezo ambazo kwa bahati mbaya sana siwezi kuzikumbuka hapa mara moja,kwamba wakongwe hawa wafanye chini juu watayarishe na kushoot DVD angalau mbili zilizoshiba za nyimbo zote zilizotamba sana enzi hizo za miaka ya Themanini,pamoja na CDs zake siyo kwa ajili ya biashara tu bali kwa faida ya vizazi vijavyo pamoja na kuweka kumbukumbu ya mchango mkubwa sana ambao nyie Mafahari wetu mlipata kuifanya hapa nchini wakati wa uhai wenu.Kila mmoja wenu aweke ubinafsi pembeni na kuiangalia Fani hii ya Muziki inakwenda wapi!Leo nyote mpo lakini miaka michache ijayo DVDs zenu zitaacha kumbukumbu nzito katika kila Familia hapa nchini Tanzania.Mauzo ya DVDs hizo nabashiri yatakuwa makubwa sana.Ili kukwepa Wizi wa Hakimiliki Producer wa DVD hizo anaweza kumalizia Mixing na Production nchini Ufaransa au Ujerumani au Uingereza na mauzo yake yakafanyika Dunia nzima.Hili ni wazo tu.Kwa hakika tulio wengi tumekuwa tukihangaika sana kuzitafuta nyimbo zenu katika CDs na DVDs lakini bila ya mafanikio yeyote.Changamoto hiyo kwenu.Najua siyo kazi rahisi kiasi hicho lakini Linawezekana.Sasa hivi tuna wajasiriamali wengi ambao nina hakika wanaweza kuthubutu.Kama zipo recording za wanamuziki maarufu kama Ndall Kasheba na wengineo ambao hatunao tena hapa duniani ni muhimu vilevile angalau nyimbo zao chache nazo zikajumlishwa katika hayo matoleo ya DVDs za Kihistoria.Nitashukuru sana iwapo nitasikia maoni ya wahusika wenyewe katika hili kama King Kiki na kina Assossa.Wengine wote kama Issa Nundu,Kabea Baddu,nk wote bila kukosa katika hiyo Grand Produzionne!
ReplyDelete