naibu waziri wa habari, utamaduni na michezo mh. joel bendera akipokea vifaa vya michezi toka kwa afisa uhusiano wa tigo jackson mmbando kwa ajili ya michuano ya kombe la mbunge wa moshi vijijini mh. cyrill chami (kulia juu)

Naibu waziri wa habari na utamaduni na michezo Mh. Joeli Bendera akisalimia wananchi kabla ya kuzinduliwa mashindano ya soka ya kombe la mbunge wa moshi vijijini, Dk. Cyrill Chami katika viwanja vya Ushirika, Moshi, mwishoni mwa wiki
Mbunge wa Moshi vijijini ambae pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, biashara na Masoko Dk. Cyril Chami akiongea wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo
Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro, Mh. Mohamed Babu, akisalimia wananchi
Mchuano mkali wa wachezaji wa timu za Kombania ya Sekondari ya Tambarare na Kibosho ambapo Kombainia yaTambarare ilichapwa 2-1.

Mwishoni mwa wiki Serikali imesema wadhamini waliopo katika medani ya soka hapa nchini wamekua wakisaidia kukua kwa kiwango cha soka.

Hali hiyo kujitokeza kwa wadhamini inachangia wachezaji kucheza kwa bidii ili kuwafanya waweze kunufaika kwa ufadhili husika.

Naibu waziri wa habari na utamaduni na michezo Bw, Joeli Bendera amesema hayo wakati akizindua rasmi mashindano ya soka kombe la mbunge wa Moshi vijijini lililodhaminiwa na kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo mwishoni mwa wiki iliyopita mkoani moshi kwenye viwanja vya Ushirika.

“Ninawapongeza wadhamini pamoja na waandaaji wa Kombe la Mbunge wa Moshi vijijini kwa kujitoa kushirikiana na wizara ya michezo ili kuendelea kuibua vipaji.

“Jitihada hizi za kuibua vipaji zilishapewa kipaumbelea na kampuni ya Coca Cola kupitia Copa Coca Cola ambapo hivi sasa ishara ya kupata wachezaji wazuri kwenye Timu ya Taifa inaonekana.

“Mimi nikiwa kama kiongozi wa serikali mwenye dhamana ya michezo nitaungana na Tigo na Coca Cola waliodhamini mashindano haya ya Mbunge wa Moshi Vijjijini, nitamtuma mtaalamu mmoja kwenye kila mechi itakayokuwa inafanyika katika mashindano haya ya Kombe la Mbunge wa Moshi vijijini ili aweze kuendelea kutoa maelekezo na mafunzo ya jinsi ya kuinua michezo kitaifa” alisema Mh Bendera.

Nayo kampuni ya Simu za Mkononi ya Tigo inayodhamini michuano hiyo kupitia Afisa Uhusiano wake Bw Jackson Mmbando ilikabidhi vifaa vya michezo zikiwemo jezi na mipira kwa ajili ya mpira wa miguu, netball na volleyball kwa timu 16 pamoja na fulana na kofia zilizotumika kwenye uzinduzi huo kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari 42 za moshi vijijini.

Afisa uhusiano huyo wa Tigo alisema michuano hiyo ni sehemu ya makakati wake wa kuibua vipaji vya soka vilivyopo mashuleni.

JACKSON alisema Sisi kampuni ya kampuni ya Tigo mwaka huu mwezi agosti tulianzisha kampeni maalum kwaajili ya kuinua na kuboresha kiwango cha elimu ya michezo pamoja na elimu ya Afya kwa kuchangia sekta hizo kwa kujitolea misaada ya vifaa vya kufundishia pamoja na kudhamini makongamano pamoja na midahalo ya wakufunzi wa sekta ya elimu kwa lengo la kuwawezesha kukutana na kupeana changamoto ili kuimarisha elimu Tanzania.
Leo hii Tigo tumedhamini mashindano haya ili kutimiza dhamira yetu ya kuendeleza na kuboresha michezo kuanzia ngazi ya chini kabisa kwa kuzingatia kuwa michezo hivi sasa nchini Tanzania ni ajira ya kudumu. Hivyo tunawaomba waalimu wa michezo kukubaliana na changamaoto zilizopo ndani ya mashindano haya na kuwaandaa vijana kushiriki kila wanapohitajika.

Pia tunawasihi wanafunzi wote kuitumia nafasi hii kuimarisha vipaji vyao ili waweze kuwa wachezaji wazuri na kuliwakilisha Taifa letu katika mashindano ya Kimataifa.

Awali Mbunge wa Moshi vijijini ambae pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, biashara na Masoko Dr. Cyril Chami amesema kupitia kombe lake hilko wanatumai vipaji vipya vitaibuka.
“Uwezekano wa kuinua vipaji upo, kwa kupitia mashindano haya! hivyo ninawashukuru wadhamini wetu Tigo na Coca Cola kwa ushirikiano wote kuanzia tulipoanza maandalizi haya ya Kombe la Moshi vijijini” , alisema Mh. Chami.

Jumla ya Shule 42 zilizoko moshi vijijini zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ya kombe la mbunge wa Moshi vijini kwenye mashindano yatatakayodumu kwa miezi sita.

Mashindano hayo yaliyozinduliwa rasmi kwa mchezo kati ya timu za Kombania ya Sekondari ya Tambarare na Kibosho ambapo kombania yaTambarare ilichapwa 2-1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Duh! watu wasuojua mpira bwana utawajua tuu. Huyo mjomba mwenye T-shirt nyeupe na bukta ya bluu/grey anavyorukaruka anaweza kusababisha ajali kubwa sana kwa wenzake. Ananikumbusha zamani wakati tuko shuleni Tanga school, tuulikuwa na mchezaji kama huyu alikuwa anaitwa Elisante "chagaboi" Simpa.

    ReplyDelete
  2. Kaka TIGO, toka ameondoka Kevin Twisa, naona wamekosa personality identity. Jamaa tulimzoea, akisimama unajua TIGO wanataka kusema nini. jamaa aliwakilisha BRAND safi sana. Sasa hivi personality zinazo appear hazina mvuto kabisa mtu wangu.Uongo???

    ReplyDelete
  3. Namkumbuka Mohamed Babu miaka ya 70 alipokuwa RDD Mkoa wa Mara. Huyu bwana alikuwa anajua kila kijito na mabonde. I feel proud of him.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...