JK akimakaribisha Rais Seretse Khama Ian Khama wa Botswana mara tu alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi ya siku mbili leo.
Mtoto Sara Elias akimkaribisha kwa maua Rais Seretse Khama Ian Khama muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
JK akiwatambulisha baadhi ya mawaziri wake kwa mgeni wake Rais Seretse Khama Ian Khama muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Huyu rais ana uhusiano na Sir Seretse Khama?..., rais wa kwanza wa Botswana au ni majina tu? Huu mchezo wa urais inaonekana kila sehemu ni kurithishana tu. Basi powa..., Nico Mkapa upoooo?, anza kuwarm up nawewe tukukabidhi nchi baada ya JK. Maana inaonekana Kuwahi Kulala ikulu ni sifa nzito sana ya kuchukua urais sehem nyingi tu. Haya rais Nico tunakungojea 2015 au 2025. kazi kwako...

    ReplyDelete
  2. KARIBU MGENI

    ReplyDelete
  3. Ndiyo huyu ni mtoto wa Sir Seretse Khama, raisi wa kwanza wa Botswana.
    "Lieutenant General Seretse Khama Ian Khama (or Ian a Sêrêtsê; born February 27, 1953[1]) is the President of Botswana and the Paramount Chief of the Bamangwato tribe. He is the first born son of Sir Seretse Khama (the country's foremost independence leader who was President from 1966 to 1980) and Lady Khama."

    For more information go to this link; http://en.wikipedia.org/wiki/Ian_Khama

    ReplyDelete
  4. Oyaa mshikaji punguza kutegemea sana wikipedia, ina makosa kibao, angalia kwenye Tanzania au Zanzibar utaona. Mzee Ian Khama alikuwa Rais kati ay 1968 na 1980, siyo 1966.

    Ila mimi shida yangu moja: Hivi Rais wetu anakaa ofisini saa ngapi? Kurudi nyuma kiduchu tu, alikaa USA wiki karibu 2, akarudi akapokea wageni wengine akiwemo Rais wa Madagascar, halafu akaenda Mbeya, kabla hajamaliza siku 10, akaenda Tanga kwenye Mwenge, aakarudi Mbeya kumaliza ziara, sasa yuko Arusha anampokea mgeni na kwenda Monduli. Anakaa ofisini saa ngapi jamani?

    ReplyDelete
  5. Anonymous wa October 21, 2008 8:29 pm, tafadhali usipotoshe uma. Botswana ilipata uhuru wake tarehe 30 September 1966, na raisi wake wa kwanza wa uhuru alikuwa Sir Seretse Khama. Wewe hiyo ya Sir Khama kuwa raisi wa Botswana toka 1968 umeipata wapi? Tupe source maelezo yako.

    Go to this link you will find the same information as the one found in the wikipedia; http://africanhistory.about.com/cs/biography/p/bio_khama.htm

    ReplyDelete
  6. Anony wa 8:29PM, kwani hujui siku hizi duniani kuna concept mpya ya flexible working hours?

    ReplyDelete
  7. Mimi sina source, nilisikia mtaani wakisema kuwa Botswana ilipata uhuru mwaka 1968. Sikwenda shule kama wewe, naokotaokota data tu kila mahali. Lakini huwezi kubishia pointi yangu kwamba wikipedia haiko sahihi wakati wote, usidhani ni ujanja kuijua hiyo. Kuna wikileak pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...